Kauli hii inamhusu yupi kati ya mke na HG?

Napata tabu kukuelewa coz,unawaza mbili kabla ya moja,faham sio kila mwanamke ni mke,nimezungumzia mwanamke,pili nimezungumzia HG ambae nae ni mwanamke lakini ni mke mtarajiwa kama akitaka,sasa unaposema sieleweki nami nashindwa kukuelewa,mke na HG majukumu yao ni tofauti,and so elimu pia,DA vipi?

Hebu hebu jipange upya "HUELEWEKI"
 
Kaka Eiyer,
Bila kuishi na mume utalea familia????, Ukijua namna ya kuishi na mume ndio familia yenyewe.
Unaposema "Kama ni hiyo inamfaa HG Kwa sababu HG ndiye anaelea familia"
"Lakini kama ni wote taifa litapata hasara kwa wanawake wengi kwani wataelimishwa halafu hawataitumia vyema elimu yao! .
Hapo mwanamke unakuwa hukumpa jukumu lolote, huyo Dada yeye anamlea mume?????


Kumlea mume kuna maana gani?Kama ni kumpikia,kumfulia,kuhakikish nyumba inakua safi na hata kununua aina ya chakula nyumbani huyo atakua Dada,tofauti na haya ni yapi majukumu ya mke kwa mumewe?
 
Mwanamke kwa maana ya jinsia ya kike aliyekua huwa hafundishwi bali hufundwa

Anayefundishwa ni Msichana tena darasani. Anafundisha Hisabati, maarifa, sayansi kimu, Jografia na ndugu zao..... Ili apate maarifa ya dunia ili atakapokuja kuwa Mwanamke aisaidie jamii wakiwemo wanaume kuleta maendeleo ya familia yake na taifa kwa ujumla.

Baada ya kusema hayo, Nawasalimu wanawake wote wa MMU.
 
Babu,inatakiwa tuanze na wale wanaosema ukimuelimisha "mwanamke"umeelimisha jamii nzima!
 
Kumlea mume kuna maana gani?Kama ni kumpikia,kumfulia,kuhakikish nyumba inakua safi na hata kununua aina ya chakula nyumbani huyo atakua Dada,tofauti na haya ni yapi majukumu ya mke kwa mumewe?

Mbona majukumu ni mengi tu kaka yangu yanayomuhusu mke,
Hivi bila kukaa vizuri na mumeo, kumsikiliza ushauri wake,
kupanga maisha yenu ya baadae, kuratibu mikakati yote ya nyumbani,
bashasha na Mashamsham yanayohitajika kwa mke kumfanyia mume,
hicho chakula kilichopikwa na dada kitalika????????????
huo usafi ndani ya nyumba utaonekana, kwanza baba watoto ndo huyooooo nyumbani hatorudi mapema
.
 
Tausi,hebu niambie majukumu ya mke kwa mumewe halafu tujadili mengine!
 
Nimejiuliza swali hili baada ya kuchoka kusikia vimbwanga vya ma-HG,kauli yenyewe ni kuwa;UKIMUELIMISHA MWANAMKE UMEELIMISHA JAMII NZIMA,kwanza ni elimu ipi?Pili,sasa ni yupi kati ya hao wawili?HG au MKE?Au ni elimu ya malezi?Kama ni hiyo inamfaa HG Kwa sababu HG ndiye anaelea familia kwa ulimwengu wa sasa!Au ni wanawake wote?Lakini kama ni wote taifa litapata hasara kwa wanawake wengi kwani wataelimishwa halafu hawataitumia vyema elimu yao!

...dahhh,....nimejitahidi sana kujaribu kukuelewa, ila kwa hili Eiyer ni halali yako kuchanganyikiwa...
maana ushaweka na hitimisho mbili zinazokinzana vile vile.
 
Swali lako halieleweki kwa sababu:

Unamaanisha nini kumsomesha "MKE"????
Unamaanisha nini kumsomesha "Maid" aka "Dada"???

Naona kama huelewi wanapomaanisha kumsomesha Mwanamke.

Napenda nikwambie hawamaanishi kumsomesha "Mke" huyo tayari
anakuwa amesomeshwa na wazazi wake wanachomaanisha
kumsomesha mwanamke ni wale "Mabinti" "Wasichana" ambao bado
hawajaolewa sasa wewe mwenzetu umekuja na ya kumsomesha "Mke"??

Siku njema
kwa kuongezea tu Dena zipo familia nyingi ambazo HG anaendelezwa kielimu kama evening class za 'o' level au veta kujifunza ufundi stadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom