Kauli dhidi ya Malawi: JWTZ wamshushua Lowassa!

huyo mwenye mamlaka yupo wp?

Alienda Marekani, akapita Dar kubadili nguo, akaenda Kampala kwenye mkutano kujadili amani ya Congo, then akaunga Ghana kwenye mazishi na kutembelea mashamba ya nanasi.
 
Okay. So you mean kwamba Jakaya kaliinstruct Jeshi lim-burst lowasa? kama ni kweli safi sana na ninawithdrawal kauli yangu ya udhaifu, lakini kwanini asifanye hivyo mwenyewe? ataendelea kujificha nyuma ya wasaidizi wake mpaka lini?
Jamani, mwacheni atuwakilishe kwenye misiba
 
Tuna tatizo kubwa sana na uongozi wa bunge letu; hawa wenyeviti wa kamati za bunge sio wasemaji wa bunge!! Msemaji mkuu wa bunge ni Spika , hawa wenyeviti wanatakiwa kureport shuhuli zao kwa Spika na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa tamko kwa niaba ya bunge. Uongozi dhaifu wa bunge ndio umewafanya hawa wenyeviti wajitwalie madaraka ambayo si yao!! Nature abhors a vacuum!!!

naungana na wewe,katika bunge hili naona kamati zimekuwa zikisikika kusema ambayo mwenye mamlaka ya kuzungumza sio wao!wenyeviti wamekuwa wazungumzaji wa masuala ya wizara zilizo chini ya kamati zao.
 
becareful with arab leaders. They start war and use blacks to fight. Then iran sells you weapons and he gets your money. Gues who will win???
 
Hivi hamjui Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania ni nani?

Hakuna Mwanajeshi wa chini yake anaeweza kuliongelea taifa kisiasa bila amri na au idhini yake.



Hivi amirijeshi mkuu wetu ni yupi vile? Yule bubu au ni Yule kiziwi?
 
LOWASSA ni mkurupukaji wa siku nyingi na always ukurupukaji uwa una mgharimu ila ndo hivyo maskini HAJAJITAMBUA laiti na MALAWI kama kungekua na wakurupukaji km huyu nadhani saivi tungekua tiari tunaongerea habari nyingine...Kauli ya LOWASSA ilikua ni kubwa sana as if na upande wa pili tiari wameshapeleka vifaru hatuitaji VITA na wala MALAWI hatudhani km wanahitaji vita zaidi ya maendeleo! Ukipitia blogs nyingi za malawi tunaonekana km sisi ni wagonvi, hatujaelimika na warmongering! hongera JWTZ kwakuona mbali sio huyu mkurupukaji kwanza wote wanasali kanisa moja kwa TB JOSHUA
 
LOWASSA ni mkurupukaji wa siku nyingi na always ukurupukaji uwa una mgharimu ila ndo hivyo maskini HAJAJITAMBUA laiti na MALAWI kama kungekua na wakurupukaji km huyu nadhani saivi tungekua tiari tunaongerea habari nyingine...Kauli ya LOWASSA ilikua ni kubwa sana as if na upande wa pili tiari wameshapeleka vifaru hatuitaji VITA na wala MALAWI hatudhani km wanahitaji vita zaidi ya maendeleo! Ukipitia blogs nyingi za malawi tunaonekana km sisi ni wagonvi, hatujaelimika na warmongering! hongera JWTZ kwakuona mbali sio huyu mkurupukaji kwanza wote wanasali kanisa moja kwa TB JOSHUA

pole kutokujua makundi yaliyopo ndani ya JWTZ,ni kama CCM ilivyo. Huyo mwenye mamlaka yupo wp na ametoa tamko gani,JWTZ hawana utendaji mzur kijeshi,mbona wanaruhusu ndege za Kijeshi kutoka nje ya nchi kuja kuchukua wanyama hapa nchini tena mbaya zaidi na ndege yao pia inahusika, Lowassa amewapa moyo watanzania kuliko huyo Jk aliyenyamaza. Mnadhimu mkuu wa Jwtz ameficha TRILIONI 3 nje ya nchi mbona hawaziongelei au wao haziwahusu? Kama kweli ni Jeshi la Watanzania basi lifanye kasi yk na si ujinga
 
kusema jeshi lipo fit kwa kupigana, wanakanusha nini kwani hawako fit? JK anawaza safari, bora EL amedhubutu hata kuwatishia no matter tuna nguvu ana la!

Amiri Jeshi mkuu hatakiwi kusema tupo tayari ni kusema vijana kazi ianze!

Good, hebu mwambie huyo mnafiki aliyetumwa na CCM. Mkwara wa Lowasa umesaidia sana. Wewe unategemea JK angesema, angesubiri mpaka watu wachukue Ruvuma yote, Iringa, Mbeya, labda wangeanza kutaka kuiteka Morogoro ndiyo angewaita Wazee wa DSM kuwaeleza msimamo wa serikali.Si ndivyo anavyofanya. Acheni unafiki enyi vibaraka wa JK, TZ ina watu makini wengi sana. Yaani EL, Membe na Sitta wameleta heshima ya nchi.Acheni ubishi wa kijinga.
 
kama Membe alikwisha toa kauli ya serikali kulikuwa na haja gani ten EL kurudia kauli ileile? Mjukumu ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge hayajulikani? Kama yanajulikana, na kama amevuka mipaka ni nani wa kumuonya dhidi ya upotofu huo? Kamati hiyo inawajibika kwa nani? EL hajaliamrisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenda vitani, kwa nini JWTZ wanaona wajibu kabla kuulizwa au kuelekezwa chochote? Kusema Jeshi letu ni imara kunawza kufanywa na mtu yeyote hata asiye na madaraka yoyote wala uhakika wowote wa kauli hiyo, je ni kosa? Je ikiwa atasema Jeshi letu ni dhaifu atakuwa sahihi?
Kauli hiyo ikisemwa na EL au JK kutabadili ukweli wa hali halisi ya Jeshi lilivyo?
 
Ni tamko zuri kutoka jeshini. Lowasa amezidi, na kila anapopata nafasi amependa kutoa matamko ya ki-rais. Lakini na wewe JK, mbona kila kitu unataka kuongea wa mwisho mwisho?
 
President-Banda-arriving-at-the-function.jpg


President Joyce Banda, "I shall die for the people of Malawi. I shall die for the land of Malawi".

Kama ni kweli kuwa Raisi na Amiri Jeshi Mkuu wa Malawi, Joyce Banda, amewahi kutoa kauli yoyote ile kuhusiana na huu mzozo wa mpaka kati yetu na Malawi, basi lazima tukiri kuwa tuna tatizo, tena kubwa, la kiuongozi. Tamko lolote linalotolewa na Raisi wa nchi yoyote ile dhidi ya nchi nyingine, na hasa kama kuna mgogoro wowote ule kati ya nchi hizo mbili, linahitaji majibu (response) ya Raisi wa nchi husika. Pamoja na hilo tendo lolote la uchokozi kama la uvamizi linalofanywa na nchi moja dhidi ya nchi nyingine, linahitaji onyo na tamko zito linaloweza kutolewa tu na Raisi na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi husika.

Mpaka sasa ni mwaka moja toka aliyekuwa Raisi wa Malawi, Bingu wa Mutharika kuipa ruhusa kampuni ya Uingereza inayoitwa Surestream Petroleum kufanya utafiti kwenye Ziwa la Nyasa/Malawi bila kujali kuwa sehemu ya Ziwa hilo ni Tanzania. Si mara ya kwanza nchi yetu kuvamiwa na wale wenye macho ya husuda...mwaka 1978, Idi Amin, Raisi wa Uganda aliivamia Tanzania na kuteka eneo la Kagera na kuliita sehemu ya Uganda. Tamko la kumtaka Amin ayaondoe majeshi yake haraka, kama nakumbuka vizuri, halikutolewa na any Tom, Dick & Harry, lilitolewa na Raisi na Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika awamu hii tumeshuhudia ndege ya Kivita ya nchi fulani ikiingia nchini na kuteka baadhi ya wanyama wetu, kuwapakia na kuwasafirisha nje ya nchi. Mpaka dakika hii ninapoongea sijasikia tamko la Raisi na Amiri Jeshi Mkuu wetu akilaani kitendo hicho wala akichukua hatua sahihi kama kwanza kutoa onyo kwa hiyo nchi na pili kuwahakikishia wananchi usalama wao dhidi ya huo uvamizi. Nachelea kusema kwamba kukosekana kwa uongozi thabiti dhidi ya vitendo kama hivyo labda ndiko kumewapa Malawi jeuri ya kuvamia nchi yetu kama vile wanaingia nyumbani kwao...wapo pia Wazungu, Wachina, Wahindi, Wasomali...
 
Mgogoro haujatanzuliwa, jeshi linajiingiza kwenye mipasho na wanasiasa khaa..!? Kumbe hata huyo joyce angejua udhaifu huu wa jwtz asingeziondoa ndege za utafiti ziwani! Watu wanachimba biti kwa adui nyie mnaleta uleledada hapa? Kwa kauli gani mzito aliyotoa edward hapo mpaka muanze kuweweseka? Au mnaogopa vitambi mlivyo navyo mtaumbuka mtanange ukianza? Mie sijui sheria ila hata kama hilo ni la kweli sidhani kama huu ni muda muafaka kuyazungumza hayo!
 
Ukiqa daifu na mzembe siku moja utaona jirani yako yupo chumbani anasaidia kumuua nge, au kubadili balbu.
 
Back
Top Bottom