Kauli Cheshi za KAKOBE

Let me be neutral, ningependa kujua ni kwa nini umeme wa 132kv unaotoka mtera na kidatu umetengewa njia yake na karibu yake hairuhusiwi kujengwa makazi ya watu, lakini huu wa 132kv kutoka ubungo (kama kweli ni 132kv) unapitishwa karibu na makazi ya watu? au si 132kv? na kama ni 132kv hamwoni kuwa serikali inawatendea vibaya wakazi wote katika barabara hiyo na wala si kakobe na waumini wake ambao kwanza hawaishi eneo hilo?

mkuu, hapo inategemea unazungumzia ukaribu wa namna gani? kuna vipimo vya kitaalamu..umbali ambao kitaalmu na kisheria huruhusiwa kujenga/kuishi hapo kwa umeme huo.

na kabla ya mradi huo ilifanyika tathmini ya athari zake (if any) , serikali na wadau wakajiridhisha kuwa its okay, mradi ukaendelea. tatizo kakobe anadai kuwa huo umeme unge interfere na matangazo yake ya Tv sijui na redio...ambayo huko TCRA wala hawajapokea maombi ya kitu kama hicho

la muhimu ni kwamba maeneo yote ya mikocheni kuna matatizo makubwa ya umeme kuwa mdogo na kazi haziendi huko ila kwa mbinde

na ukichunguza kakobe tangu enzi hizo alikuwa na mattaizo na TANROADS kwa sababu alikuwa/yupo kwen road reserve. kwenye road reserve huruhusiwi makazi ya watu...na ndipo miradi kama hiyo huwa inapita!
 
My friend, Kakobe and his follower just did worship the so called gods..........Daniel said, and I qoute "Your Majesty, we don't need to defend ourselves. 17The God we worship can save us from you and your flaming furnace"

Kakobe defended himself, he used his followers to fight Tanesco guys from erecting the poles.

Got that?!!! Tofautisheni kati ya matendo ya kiuanaharakati na will of God.[/QUOTE

Imani ya mtu ni swala gumu sana kwa m2 mwingine kulielewa!!
But do you know why Kakobe didnt like the poles zipite pale?
Just make your own research and you will just know kwamba serikali imetumia mabavu!!
 
mkuu Jossey

research imeshafanyika na watu wa BICO. kama kuna upande mwingine hatuujui kama unavoimply hapa, then kindly hebu tuambie kwa nini unadhani Kakobe kaonewa..tena yeye tu pale kwenye kaeneo kake wakati umeme unapita sehemu nyingi tu zinazofanana na hizo?
 
[/QUOTE

But do you know why Kakobe didnt like the poles zipite pale?
[/QUOTE]

Sisi Hatujui tueleze wewe
 
SIKU moja baada ya serikali kuamua kupitisha waya za umeme wa kilovoti 132 karibu na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe, amesema anaamini umeme hautawaka kwa nguvu ya Mungu kwa vile hakuna nguvu zitakazopita hapo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema ameshangazwa na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuutangazia umma kuwa ameridhia umeme huo kupitishwa kwenye kanisa hilo.
“Nakwambia hata wakipitisha umeme huu hapa… hautawaka kwa vile nguvu ya Mungu itashinda nguvu ya umeme lakini kibaya nimesikitishwa na Waziri Ngeleja kuutangazia umma eti nimekubali umeme upitishwe hapa, nasema siyo kweli jamani,” alisema Askofu Kakobe.
Alisema yeye mwenyewe hana uwezo wa kukataa maamuzi yaliyofikiwa na serikali ndiyo maana hadi jana hakukuwa na muumini hata mmoja ambaye alikuwa akililinda eneo hilo.
“Huu ni uonevu wa hali ya juu, sijakubaliana na maamuzi hayo kwa kuwa vipimo vyote vilivyotolewa havikuwa vya kweli na kama ningekuwa nimeafiki basi ile siku Waziri Ngeleja alivyotoa taarifa yake ningeshiriki katika hicho kikao,” alisema Askofu Kakobe.
Alisema hivi sasa amegundua hawatakiwi kupinga upitishaji wa umeme huo kimwili kama walivyokuwa wamefanya huko siku za nyuma bali ni kutakiwa kukaa katika maombi.
Alisema ni hatari kukatalia utawala ambao hauna hofu ya Mungu kwa kuwa hauwezi kudumu na mara nyingi unakosa kutenda haki, hivyo jamii nzima inatakiwa kuondoa tofauti zao na kuwa na sauti moja ili kukemea unyanyasaji unaofanywa na utawala.
Alisema hivi sasa amepata taarifa za uhakika kuwa baadhi ya watu wamepewa taarifa kuwa wanatakiwa kuhama katika eneo hilo kupisha upitishaji wa nguvu hiyo ya umeme kitendo ambacho kinampa ishara kuwa kuna mpango wa kanisa lake kuvunjwa.
“Kwa sasa jamii haiwezi kunielewa, lakini ukweli ni kuwa serikali hii imedhamiria kuvunja maeneo hayo kwa kuwa hakuna mradi kama huu unaofanyika ukaruhusu jirani kuwa na vizuizi kama majengo” alisema Askofu Kakobe.
Alisema amesikitishwa na Waziri Ngeleja kutoa maelezo kuwa hata kituo cha televisheni ambacho anatarajia kuanzisha hakitaweza kukidhi vigezo.
“Unawezaje kusema eti hatuwezi kukidhi vigezo vya kuomba usajili, inawezekana labda wameshafikia hatua ya kutaka kutunyima kibali maana wanatoa kauli hizo ambazo zinaweza kuwa ni dalili njema,” alisema Askofu Kakobe.
Askofu Kakobe alipingana na madai yaliyotolewa na Mshauri Mtaalam wa Kampuni ya BICO, kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatakiwa kuepukana na kona kali kwenye waya na kutounganisha sehemu yoyote kati ya nguzo namba 18 na 19.
Akitolea mfano, alisema kuna maeneo mbambali yaliyopitishiwa umeme kama huo, ingawa unatofautiana kwa ukubwa wake, ambao umewekwa kona ikiwemo maeneo ya Mwenge na katika kijiji cha Tanangozi kilichoko Iringa karibu na makaburi ya Kiyeyeu.
“Huu ni uwongo! Wanafikiri hatuna uelewa wa masuala hayo ya umeme? Si kweli kuwa kunaweza kutokea madhara iwapo kutawekwa kona kama wangepitisha upande wa pili; mbona karibu na kaburi la Kiyeyeu kule Iringa nguzo zimevushwa upande wa pili?” alihoji Askofu Kakobe.
Juzi Waziri Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari kuwa mgogoro uliodumu kwa siku 77 kati ya serikali na Askofu Kakobe umemaliza kwa askofu huyu kukubali umeme huo kupitishwa eneo la kanisa lake.

SORCE Tanzania Daima.

Kama kweli atafanikisha hilo hapo kwenye red,
Bila shaka Kakobe atauziilishia uma kuwa yeye kweli ni mtumishi wa mungu wa ukweli.
 
Huyu ni Mshirikina hana lolote, Ngoja tuone atachotambia. Mi nahisi ataendelea kuumbuka
 
Hivi alipata wapi hivi Vipimo? Hapa lazima tukubali kwamba kama kweli alidanganya na ikathibitika Mbele yake Mwenyewe basi Credibility yake itakuwa imeshuka sana sema tu Waumini hawawezi kumweleza

Cheki hii Link

https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/52878-serikali-imemshindwa-kakobe.html
Mkuu, hawawezi kuthubutu! kama anawaambia keni hapo nje wanakaa, hata mvua ikinyesha, au jua likiwaka vipi nyie kaeni tu.....sijaona kichaa cha namna hii.
 
mkuu Jossey

research imeshafanyika na watu wa BICO. kama kuna upande mwingine hatuujui kama unavoimply hapa, then kindly hebu tuambie kwa nini unadhani Kakobe kaonewa..tena yeye tu pale kwenye kaeneo kake wakati umeme unapita sehemu nyingi tu zinazofanana na hizo?

There is more Than the eye can see!!
Kaizer Kakobe amekua na ujasiri wa kusimama. Watanzania wengi ni waoga na hawajui haki yao. Ndio maana amesimama mmoja ambaye ni kakobe.
Hata kama alikua yeye alikua wrong. Its good that ameeleweshwa from those BICO guys. But kulingana na kauli zake ni kwamba hajaridhika na maelezo yao. coz kama measurement zinaonyesha kuwa there is no harm there was no need for him to Curse the project.
Gosh!! am just becoming more confused!!! Sorry Am lacking words
 
Mkuu Unafahamu unachozungumza?

mkuu, ndiyo sababu nikasema niwe neutral ili nipate ukweli maana yanayosemwa yanawasha masikioni. Huwezi hata kujua expert ni nani, mwanasiasa ni nani, na mkuu wa dini ni nani. Wote wamekuwa wataalamu mpaka jamaa wa dini akaamua kudanganya kuhusu TV na radio ambayo hata application hana. Sorry if it offended anyone. Thanks
 
There is more Than the eye can see!!
Kaizer Kakobe amekua na ujasiri wa kusimama. Watanzania wengi ni waoga na hawajui haki yao. Ndio maana amesimama mmoja ambaye ni kakobe.
Hata kama alikua yeye alikua wrong. Its good that ameeleweshwa from those BICO guys. But kulingana na kauli zake ni kwamba hajaridhika na maelezo yao. coz kama measurement zinaonyesha kuwa there is no harm there was no need for him to Curse the project.
Gosh!! am just becoming more confused!!! Sorry Am lacking words

Kama Waumini wake Wataalamu ( Naamini wapo) wangekuwa na Ujasiri wa Kumwelewesha tangu Mwanzo may be angeelewa lakini naamini na wao walikuwa wanakesha Kulinda kitu ambacho hata wao hawakiamini!
 
Watu wamekesha kwa miezi miwili mizima na mwisho wa siku umeme unapita.
Angekuwa na macho ya kiroho, angeona kuwa kamwe huwezi kushindana na serikali.
Kwa jinsi baadhi ya waumini wake wanavyomwamini huyu bwana wako tayari kufanya chochote atakachowaambia au kuwaagiza. Sasa ikitokea siku moja SHETANI akimwingia tusije kushangaa kuona mambo yaliyofanywa na KIBWETERE wa Uganda yakiwatokea waumini wa KAKOBE.
 
Mkuu, hawawezi kuthubutu! kama anawaambia keni hapo nje wanakaa, hata mvua ikinyesha, au jua likiwaka vipi nyie kaeni tu.....sijaona kichaa cha namna hii.

mkuu,"Religion is the opium of people" -Samora Marcel

Si ajabu pengine, yumkini, inawezekana hata wewe kama ungekuwa muumini wa pale, either ungekaa miezi hiyo yote au ungedefend cause kwa nguvu zote.

Mambo ya dini acha kabisa. Ulishawahi kujiuliza kwanini watu wanaua wengine (wanaowaona) in the name of god ambaye wala hawajawahi kumwona?
 
Kwa jinsi baadhi ya waumini wake wanavyomwamini huyu bwana wako tayari kufanya chochote atakachowaambia au kuwaagiza. Sasa ikitokea siku moja SHETANI akimwingia tusije kushangaa kuona mambo yaliyofanywa na KIBWETERE wa Uganda yakiwatokea waumini wa KAKOBE.

Naamini huko hatuwezi kufika Mkuu!
 
There is more Than the eye can see!!
Kaizer Kakobe amekua na ujasiri wa kusimama. Watanzania wengi ni waoga na hawajui haki yao. Ndio maana amesimama mmoja ambaye ni kakobe.
Hata kama alikua yeye alikua wrong. Its good that ameeleweshwa from those BICO guys. But kulingana na kauli zake ni kwamba hajaridhika na maelezo yao. coz kama measurement zinaonyesha kuwa there is no harm there was no need for him to Curse the project.
Gosh!! am just becoming more confused!!! Sorry Am lacking words

unajua hapa tunasahau kitu kimoja..hoja ya kusimama kutetea 'haki' basi hiyo haki iwepo! Kakobe pale hajaweza kuprove kwamba ana HAKI...ina maana yeye ndo alikuwa anatudanganya na mikutano yake na waandishi akibase kwenye vipimo vyake..sasa vipimo halisi vimemwumbua...!

kwa hiyo ni kwamba alijifanya kichwa ngumu tu, na huenda alitaka atumie hii kujipatia umaarufu kwa 'kuishinda ' serikali
 
Back
Top Bottom