Katuni niliyoipenda

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Mgomo Mlimani Na Katuni Iliyosahauliwa

Na maggid mjengwa,

UKISIKIA mtu amegomea jambo, unachotakiwa kuuliza ni kipi kilichomfanya agome. Maana, kugoma kuna maana pia ya kupinga. Wajibu wetu iwe ni kuhukumu hoja zinazotolewa na anayegoma.
Mathalan, kama mahabusu wanapofika mahakamani wanagoma kushuka kwa madai kuwa wanakerwa na foleni za magari, basi, hoja yao hiyo itakuwa haina nguvu. Lakini, kama wanadai, kuwa wanagoma kwa kuwa kesi zao zinacheleweshwa na za wengine zinaharakishwa, basi, hapo kuna hoja inayotakiwa kujibiwa.

Historia ni mwalimu mzuri sana. Ili tuweze kuyaelewa yanatokea leo, na ili tusije tukashangazwa sana na kitakachotokea kesho, basi, ni busara tukaangalia na kujifunza kwa kilichotokea jana.

Profesa Issa Shivji ni mmoja wa wanazuoni mahiri nchi hii imepata kujaliwa kuwa nao. Katika hili la mgomo wa Chuo Kikuu, nimelazimika kuyapitia tena maandiko yake. Hakika, baada ya kusoma kitabu chake; Intellectuals At The Hill- kwa maana ya Wasomi wa Mlimani, nimebaki kutingisha kichwa. Kwani, yanayotokea Chuo Kikuu leo na sababu ya kinachopelekea yatokee ni yale yale aliyoyaandika Profesa Shivji katika mkusanyiko wa insha zake kwenye kitabu hicho.

Sikuishia hapo, nimelisoma pia jarida linalotolewa pale Chuo Kikuu. The Hill Observer ( Toleo Na 004, Aprili 2007). Hata baada ya kupitia jarida hilo, bado nikabaki kutingisha kichwa na kujiuliza; iweje tahariri ya jarida hilo nayo inajaribu kuuliza na kujibu maswali yale yale ambayo yameulizwa na Profesa Shivji kwenye kitabu chake?

Tahariri ya The Hill Observer inasema; Please, no more sleeping universities. Kwamba Vyuo Vikuu visilale. Yanayoulizwa na wasomi hawa ni pamoja na; Vyuo Vikuu vinaufanyia nini umma? Je, vyuo vyetu vinafanya ya kutosha kuunga mkono umma?

Lakini Profesa Shivji, kupitia maandiko yake anatabanaisha juu ya hali kama hiyo kwa kuiangalia historia ya harakati za wanafunzi wa vyuo vikuu. Shivji anaandika; wakati wavuja jasho, wafanyakazi na wakulima wa nchi hii wakitahabika katika hali ngumu ya kiuchumi, wasomi wetu wapo katika usingizi mzito. ( Intellectuals At The Hill, Uk. 56-57)

Mbali ya migomo mingine, Shivji anatutolea mfano juu ya mgomo wa mwaka 1971. Ni pale Rais wa Serikali ya wanafunzi wakati huo (DUSO) alipofukuzwa chuoni hapo. Bwana huyu aliitwa Akivaga, raia wa Kenya. Akiwa Rais wa DUSO alipata kumwandikia barua ya wazi Makamu wa Mkuu wa Chuo Bw. Pius Msekwa akimshutumu kwa urasimu na kutokuwa na mashauriano na wanafunzi juu ya maamuzi muhimu chuoni hapo.

Tunasoma pia, juu ya Jarida la Cheche. Hili ni jarida la wanafunzi kwa wakati huo lililopata umaarufu mkubwa hata nje ya mipaka. Lilikuwa ni jukwaa la kujenga hoja nzito nzito. Waziri Zakia Meghji alipata kuwa mmoja wa wahariri wa jarida hilo. Mwingine aliitwa Karim Hirji, huyu alikuwa mwanaharakati aliyepata kuhamishwa kwa nguvu na serikali. Alipelekwa akaishi kijijini huko Sumbawanga. Kosa lake ni kuandika makala kwenye Jarida la Cheche akikosoa sera za Ujamaa a Kujitegemea. Sijui ni kwa muda gani alitumikia “kifungo” hicho cha kuishi kwa nguvu Sumbawanga, mbali kabisa na Dar Es Salaam.

Hivyo basi, tunaona, kuwa vuguvugu la wanafunzi wa vyuo vikuu kuhoji mamlaka na hata kuendesha migomo ni suala la kihistoria na litaendelea kuwepo. Kwamba ni kitu cha kawaida, na kuwa wasomi wana wajibu wa kuhoji mamlaka kuu kwa nguvu za hoja. Kibaya katika hili ni kufanya vurugu na hata kutumia lugha chafu kama matusi.

Kwa mfano, naukumbuka mgomo ule wa Chuo Kikuu wa mwaka 1990. Ulinikuta nikiwa sijamaliza hata Kidato cha Sita. Naikumbuka hotuba ya Rais wa Awamu ya Pili, Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi. Kwa kawaida Mzee Mwinyi huongea kwa sauti ya upole sana, lakini siku ile alionyesha dhahiri kuwa amekasirishwa. Akafika mahala akatamka; Vijana wamenitukana matusi ya nguoni. Mtu mzima akitamka hivyo, basi , haulizwi ni matusi gani? Ndipo pale Mzee Mwinyi aliposhindilia msumari wa moto na kuufanya umma pia uwe upande wa serikali. Askari wa FFU walifika Mlimani, Chuo kikafungwa, vijana wakakurudishwa makwao na kusababisha usumbufu na bila shaka hasara kwa taifa.

Mwaka 1990, msanii Ibrahim ”radi” Washokera alichora katuni yenye kuwaponda wanafunzi. Wengi wa wanafunzi waliogoma na kufukuzwa hawajaiona katuni hii, na kuna baadhi yetu tulioisahau. Ilikuwa ni katika gazeti la Mfanyakazi la tarehe 26.5.1990. Katuni iliwaonyesha wanafunzi wakiwa wamekaa mezani wakila chakula na kudai kuwa fedha za posho na mahitaji mengine haziwatoshi. Walidai ziada hiyo huku serikali ikiwalipia ada yao kwa 100% . Upande wa pili alichorwa mzazi kabwela akiwa amesimama na mtoto wake. Kabwela yule aliyeishi kwa kima cha chini cha mshahara aliuliza; ” za kwangu je?”

Hakika, ilikuwa ni kuonyeshwa upande moja wa shilingi katika kile ambacho twaweza kukiita ”anti-students propaganda”- Propaganda dhidi ya wanafunzi. Kwamba wanafunzi wanapenda anasa wakati kuna wengi wenye hali ngumu. Hatukupata kujua madai mengine ya msingi ya wanafunzi wale. Serikali iliweza kushinda kirahisi vita ile ya propaganda ikisaidiwa na vyombo muhimu vya upashaji habari. Tulikuwa na redio moja na magazeti ya Chama na Serikali.

Miaka 17 imepita tangu mgomo wa mwaka 1990. Kuna wenye kuhitaji kukumbushwa umuhimu wa kusoma alama za nyakati. Wakati umebadilika. Ibrahim Washokera angeambiwa akae tena chini achore katuni juu ya mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu leo, basi, angekutumia katuni ile ile, lakini kwa kufanya kinyume chake.

Kutakuwa na mabadiliko katika ile meza ya wanafunzi wale waliokuwa wakila chakula. Mahala pale sasa kuna wengine ambao si wanafunzi. Hawa yawezekana kuwa ni warasimu wanaokula na kufurahia raha za maisha. Yule mzazi Kabwela sasa ni mzee na mtoto wake sasa yuko Chuo Kikuu.

Mtoto yule anaambiwa na walioka meza ya chakula; ”rudi nyumbani ukatuletee 40% ya ada”. Wanaosema haya nao walipata kuwa wanafunzi kutoka familia masikini za Makabwela wa nchi hii. Serikali ya wakati huo, kwa kutambua mazingira magumu na umasikini wa wazazi wao, kwa fedha za walipa kodi, iliwalipia mpaka nauli zao za kutoka vijijini kwao kwenda Chuo Kikuu.

Yawezekana kabisa, kuwa mzazi wa mtoto huyu anayerudishwa nyumbani hakuwa hata na uwezo wa kulipa ada ya 70,000/= kwa mwaka kwenye Shule ya Sekondari ya Serikali. Atafanya mazingaombwe gani ya kuweza kukusanya 40% ya ada wakati kwa mwaka mzima anashindwa kuwa na akiba hata ya elfu hamsini? Na je, tunafanyaje, itakapofika Mei 16 na bado kukawa na watoto wa Makabwela watakaoshindwa kulipa ada hiyo?
 
Viko vyanzo vingi vya katuni za kisiasa zenye kuibua mjadala. Tuziletapo JF thread hii yaweza kuwa pahala husika.

katuni_01.gif
katuni_02.gif

katuni_03.gif
katuni_04.gif



Leteni nyingi zaidi toka vyanzo mbalimbali ili tucheke huku tukipata ama kutoa ujumbe.

JJ
 
JJ

Asante sana. Hii ni burudani tosha kabisa . . . na zile za wanaotuhumiwa kufanya ngono zembe tuwekeeni ili wasiwe wanajirahisisha kiasi hicho na wajue kwamba jamii inawamulika kila mahali .. kama ambavyo Mwanakijiji ameamua kula nao sahani moja huko bungeni (Dodoma)
 
Kuna kikatuni chahusu vigogo na ajali hizo wanazozipata.
 

Attachments

  • Ajali za wakubwa.doc
    44 KB · Views: 386
Jamani madaktari kwa mtindo huu mbona tutakoma. Hivi kuna hatari kubwa kwamba kuna siku mimi na mwanangu wa miaka kumi tukilazwa hapo mnaweza kumfanyia upasuaji wa ujauzito mtoto wangu just kwa kujifanya mmechanganyikiwa kwa majina yetu.
 

Attachments

  • WaKichwaMguuKichwa.doc
    38.5 KB · Views: 178
Naamini kuwa kama ni ubunifu kwa kipindi hiki cha bajeti basi kipanya kafanya ubunifu mkubwa na haswa kumkumbusha waziri juu ya lile fungu la kwenda mkoa kuitetea.


 
People died, this is ill advised, unfocused, unoriginal and not funny.
 
Huyo Toto tundu atasikia basi?......Au ndo sikio la kufa??..... Kama angekuwa na akili ya kukubali kufundwa basi hii ilikuwa jando tosha. Labda kawekewa kijinga cha moto matakoni, ....hawezi kukaa chini!!

Inanikukumbusha mbaaali saana! Mtoto wa namna hiyo aliitwa kware, .....hafugiki wala hakamatiki!
 
Hebu post kauni ya kisiasa inayokuvutia....

mimi naanza na hii

controversial%20cartoon.jpg


sasa sijui hii harusi iliingia NYANI yupi maana media wamekuwa HOSTILE kuliko
 
Back
Top Bottom