Elections 2010 Katu Kikwete Hakushinda 2010 nani anabisha?

PHP:
Ndiyo ustaarabu wa kikristo huu? Kutukana wenzio hivyo? Mhhh poleni sana, inaoneshwa umeguswa kweli mpaka unapoteza utu wako, inakuwa hakuna tofauti baina yako wewe na mnyama kwa maneno machafu yanayokutoka.

Suala la ukristo linatoka wapi......................kama JK aliiba kura aliiba kura hakuna cha udini hapo kwa mwizi wa haki ya kimsingi ya wapigakura..................................
 
Mkwere ni klasmonta wa ikulu anahakikisha wafanyakazi pale hawapigi kelele wakipiga anampelekea ticha Rosti tamu.
 
Huu upuuzi kaongelee kanisani, kule ndio kuna muda wa kusikiliza upuuzi kama huu, Alelujaaaa, Amen

ndio maana Tz hatuendelei. Wajinga wengi na hawajijui. Bila shaka ni mtoto wa Makamba aliyempata wakati mwalimu
 
kumbe ulikuwa hujui?
mla nyama ya binadamu haachi hata siku moja, akkipata nafasi anakula tena kama kawaida
hivyo yanayotokea ni matokeo ya yaliyojiri
mtayaona mengi zaidi ya hayo
 
Ukweli jamani upo pale pale kuwa Mkwere 2010 hakushinda, na dhambi ya wizi daima watz tutaona matokeo yake........
umesema Mla haliwa mbona naona jamaa haliwi? anaendelea kula tu?
hii misamiati wakati mwingine sio kweli
progress.gif
 
mkuu hivi hujui wakimaliza pale kwa Husna Mubarak tunaingia kwa Kiwete wewe hujui tuu? walimaliza kule Tunisia goma likalegezea Misirii sasa macho kwa Mkwere ndo kuliwa kwenyewe huko, muone husna anavyoliwa mkuu maana alikula...
 
Mkwere ni klasmonta wa ikulu anahakikisha wafanyakazi pale hawapigi kelele wakipiga anampelekea ticha Rosti tamu.

Na EL ndo head Boy nini? hahaha kumbe mkware cheo chake bado kidogo hivyo kwa linchi letu? hahahhaa mchakachuaji yule, sasa wabongo tukiandamana kama Misri sijui monitor atahandle?
 
Mkwere ni klasmonta wa ikulu anahakikisha wafanyakazi pale hawapigi kelele wakipiga anampelekea ticha Rosti tamu.

PHP:
Ndiyo ustaarabu wa kikristo huu? Kutukana wenzio hivyo? Mhhh poleni sana, inaoneshwa umeguswa kweli mpaka unapoteza utu wako, inakuwa hakuna tofauti baina yako wewe na mnyama kwa maneno machafu yanayokutoka.

Suala la ukristo linatoka wapi......................kama JK aliiba kura aliiba kura hakuna cha udini hapo kwa mwizi wa haki ya kimsingi ya wapigakura..................................

Mkware ni mwizi na katwe mwizi hamna ustaarabu kwake hata siku moja...ni mwizi wa nchi yetu tena zaidi ya mvunja maduka ila huyu ni jambazi tena zaidi ya jambazi sugu....
 
Wataka matokeo ya rais yapingwe

Kiongozi Mkuu wa Mpango wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya katika kusimamia Uchaguzi 2010 Tanzania, David Martin, akionyesha vitabu vya majumuisho ya matokeo ya uchaguzi jijini Dar es Salaam jana.

Jumuiya ya Ulaya (EU) imeshauri serikali ikubali mgombea binafsi ili kila raia awe na haki ya kuwania nafasi ya uongozi bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
Vile vile, imeshauri sheria zifanyiwe marekebisho ili watu wasioridhishwa na matokeo ya urais wawe na fursa ya kuyapinga mahakamani.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi kutoka EU katika uchaguzi uliopita, David Martin, wakati akisoma ripoti ya pili ya uangalizi ya timu hiyo, baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Alisema EU inaona kuna umuhimu wa kuifanyia marekebisho Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) kwa kuwa zimekuwa zikilalamikiwa sana na wananchi.
Aidha, timu hiyo ilisema makamishna wa NEC wasiteuliwe na rais wala wasiwe watumishi wa serikali.

Martin alisema serikali iondoe mfumo wa viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri na watendaji wa kata kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Alisema timu yake ilibaini kuwa mchakato wa upigaji kura haukuwa huru na haki, walibaini kasoro na kutoa mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha chaguzi zijazo.
Alipendekeza NEC ichapishe kwa wakati majina ya wapiga kura na kuyasambaza kwenye vituo vya kupigia kura, kuhakikisha kunakuwepo vifaa vya kupigia kura, kupata idadi kamili ya vituo, idadi ya majimbo na kwamba timu yake haikuridhishwa na mchakato mzima wa upigaji kura.
Aliongeza kuwa mapendekezo mengine ni pamoja NEC kuangalia mipaka ya majimbo ili kujua kama yanaendana na idadi kamili ya wapiga kura waliopo eneo hilo.
Martin ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la EU, alisema wanatoa maoni na mapendekezo ili demokrasia ikue na kushamiri katika chaguzi zijazo nchini.
Aliwapongeza wananchi, vyama vya siasa, serikali pamoja vyama visivyokuwa vya kiserikali kwa namna ambavyo wanajihusisha katika mjadala wa kuandika katiba mpya nchini.
Aliwataka Rais Jakaya Kikwete pamoja na Spika Anne Makinda, kuchukulia ripoti yao kama sehemu ya mchakato wa kuhakikisha katiba mpya inapatikana nchini ambayo itakidhi mahitaji ya Watanzania.
CHANZO: NIPASHE
 
EU: Matokeo yarasi yapingwe mahakamani Send to a friend Friday, 11 February 2011 21:04 0diggsdigg

Elias Msuya
JUMUIYA ya Ulaya(EU) imetoa ripoti yake ya mwisho kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana na kuitaka Serikali iandae sheria itakayowapa haki wananchi kupinga matokeo ya urais mahakamani.

Kadhalika jumuiya hiyo imependekeza kuruhusiwa kwa wagombea binafsi, kwa maelezo kwamba kuwalazimisha wagombea kupitia kwenye vyama kunawanyima baadhi ya wananchi haki yao ya demokrasia ya kuchaguliwa.

Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi wa EU, David Martin, jijini Dar es Salaam jana, imetoa mapendekezo 30 yanayokosoa mwenendo mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa ajili ya kuboresha mazingira ya uchaguzi ujao.

Tamko la EU limekuja wakati nchi ikiwa katika vuguvugu kubwa la mabadiliko, ambapo tayari Serikali imekubali kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Katiba inayotumika sasa imekuwa ikilalamikiwa kuwa haikidhi mazingira ya sasa na kwamba ni kikwazo cha utekelezaji wa demokrasia nchini.

Uchaguzi uliopita ulimpa ushindi wa asilimia 61 Rais Jakaya Kikwete wa CCM, huku ulipingwa vikali na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliyepata asilimia 27 akidai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ikishirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa ilivuruga matokeo hayo.

Kufuatia hali hiyo, wabunge wa chama hicho walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge Rais Kikwete alipokwenda kuzindua Bunge la 10 mjini Dodoma mwezi Novemba mwaka jana, wakipinga taratibu zilizomwezesha kiongozi huyo kuingia madarakani.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 41 (7), mgombea urais akishatangazwa kuwa rais, hakuna mahakama yoyote inayoruhusiwa kuchunguza kuchaguliwa kwake na kipengele hicho ndicho kilisababisha Chadema kususia hotuba ya Rais kama hatua ya kukata rufaa kwa umma.

Mwaka jana Mtanzani, Denis Maringo, alifungua kesi mahakamani akitaka kipengele hicho kirekebishwe ili matokeo hayo yapingwe.

Taarifa ya EU iliyosomwa na Martin jana inaonyesha kuwa tayari wameshawasilisha mapendekezo hayo kwa viongozi wa Serikali ya Muungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Mgombea binafsi
Kuhusu suala la wagombea binafsi, jumuiya hiyo imerejea wito wake wa kutaka haki ya wananchi kugombea kama wagombea binafsi iruhusiwe badala ya utaratibu uliopo sasa wa wagombea kulazimika kupitia kwenye vyama vya siasa.
Kesi kuhusu mgombea binafsi ilifunguliwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma mwaka 1993 na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) na Mchungaji Christpher Mtikila na ahakama hiyo kupitia kwa Jaji Kahwa Lugakingira ikaruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi.

Hata hivyo Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi hivyo alifungua kesi hiyo ya kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda tena.

Lakini Serikali iliendelea kukata rufaa hadi mwaka 2010 Mahakama ya Rufani ilipotengua uamuzi wa Mahakama Kuu ambayo katika uamuzi wake ilisema mahakama haina uwezo wa kutengua kifungu cha katiba hivyo kuifanya Serikali kuibuka kidedea.

Mapendekezo ya mengine ya EU
Mapendekezo mengine ya EU ni pamoja na kupunguza kipindi cha kampeni kutoka miezi mitatu hadi mwezi mmoja, kwa maelezo kuwa kipindi hicho kinawachosha wapiga kura na kuvigharimu vyama vya siasa visivyo na uwezo kifedha.
Ripoti hiyo pia imesema kuwa NEC na ZEC zilikosa uwazi katika shughuli zao hasa katika hatua ya kujumlisha kura za wagombea.

"Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa EU umesikitishwa na kutokuwepo kwa uwazi kwa tume hizo upande wa Bara na Visiwani," alisema Martin.

Alisema kuwa tume hizo zilipaswa kuchapisha na kusambaza nyaraka na vifaa vyote vya uchaguzi kwa wakati mwafaka, orodha za vituo vya kupigia kura, orodha ya majimbo na taarifa za matumizi ya fedha wakati wa kampeni.

Kuhusu tume hizo za uchaguzi, ripoti hiyo imependekeza kuwa, zisitawaliwe na maafisa wa Serikali hasa katika ngazi za mikoa ambapo hutumika watumishi wa Serikali wakti kitaifa makamishna wa tume wakiteuliwa na rais.
Badala yake Martin ameshauri ushirikishwaji wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi na asasi za kiraia katika tume hiyo.

Jumuiya hiyo imerudia wito wake wa kutaka haki ya wananchi kugombea kama wagombea binafsi iruhusiwe badala ya utaratibu wa sasa wa wagombea kulazimika kupitia kwenye vyama.

Pia imependekeza kuwepo kwa uwazi zaidi kwa vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na kuruhusiwa kufika kwenye maeneo ya uchaguzi siku ya kupiga kura.
 
kwani waangalizi wa kimataifa hawakuona madudu yaliyofanywa na NEC?
wanajua sana kila kitu kilichofanyika.:clap2:
 
Is too late but is a good start. hawa jamaa nawaamini maana usipotekeleza mapendekezo yao wanazima Misaada.
Na TZ ni nchi tegemezi hapo ndipo tutakwisha.
mkwere lazima akubaliane nao ingawa wabongo ni mafundi wa kuchakachua, lakini tutaona mabadiliko kadhaa.

Hongera EU maana wasimamizi wetu walijipendekeza kwa kusema eti uchaguzi ulikuwa huru na haki kumbe siyo.

Nadhani ni mwelekeo mzuri
 
Diplomatic response siku zote haikuambii kuwa wewe uliiba. Ila inakuambia ufanye uruhusu chaguzi zijazo zipingwe mahakamani. Kama uchaguzi ulikuwa huru na wa haki wasingethubutu kusema hivyo. Kwa kuwa uchaguzi ulichakachuliwa vyama vya upinzani vilikuwa viende mahakamani ila katiba ikabana.
 
“Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa EU umesikitishwa na kutokuwepo kwa uwazi kwa tume hizo upande wa Bara na Visiwani,” alisema Martin.

Alisema kuwa tume hizo zilipaswa kuchapisha na kusambaza nyaraka na vifaa vyote vya uchaguzi kwa wakati mwafaka, orodha za vituo vya kupigia kura, orodha ya majimbo na taarifa za matumizi ya fedha wakati wa kampeni.

Kuhusu tume hizo za uchaguzi, ripoti hiyo imependekeza kuwa, zisitawaliwe na maafisa wa Serikali hasa katika ngazi za mikoa ambapo hutumika watumishi wa Serikali wakti kitaifa makamishna wa tume wakiteuliwa na rais.
Badala yake Martin ameshauri ushirikishwaji wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi na asasi za kiraia katika tume hiyo.

Jumuiya hiyo imerudia wito wake wa kutaka haki ya wananchi kugombea kama wagombea binafsi iruhusiwe badala ya utaratibu wa sasa wa wagombea kulazimika kupitia kwenye vyama.

Pia imependekeza kuwepo kwa uwazi zaidi kwa vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na kuruhusiwa kufika kwenye maeneo ya uchaguzi siku ya kupiga kura.

ndo wizi mkubwa zadi hata ya ufisadi
 
Is too late but is a good start. hawa jamaa nawaamini maana usipotekeleza mapendekezo yao wanazima Misaada.
Na TZ ni nchi tegemezi hapo ndipo tutakwisha.
mkwere lazima akubaliane nao ingawa wabongo ni mafundi wa kuchakachua, lakini tutaona mabadiliko kadhaa.

Hongera EU maana wasimamizi wetu walijipendekeza kwa kusema eti uchaguzi ulikuwa huru na haki kumbe siyo.

Nadhani ni mwelekeo mzuri
Mkwere hana shida maana terms zote kachakachua so atayekuja ndo kiama atakiona
 
Diplomatic response siku zote haikuambii kuwa wewe uliiba. Ila inakuambia ufanye uruhusu chaguzi zijazo zipingwe mahakamani. Kama uchaguzi ulikuwa huru na wa haki wasingethubutu kusema hivyo. Kwa kuwa uchaguzi ulichakachuliwa vyama vya upinzani vilikuwa viende mahakamani ila katiba ikabana.

kila ukibana lazima utaachia tu ngoja hawa jamaa EU tuone kiama chao maana hawacheki na mutu
 
Mheshimiwa Kikwete alishinda tena alishinda kirahisi sana,naelewa kuwa mnaishabikia Chadema,inawezekana kabisa hamna hata shahada ya kupigia kura seuze kujiandikisha ,hivyo mpo sawa na wale ambao wakienda kwenye mikutano kwa wingi na kujenga tamaa kwa viongozi wa Chadema kuwa wanakura nyingi .kumbe ni washangiliaji tu.

"....Haya mambo nilisha yazoea, hata ukini-provoke siprovokiwi...kwi kwi kwi kwi ..."
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom