Katoliki wasogeza mkutano wa CUF

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Na Asha Bani

MKUTANO mkubwa wa hadhara uliokuwa ufanywe na Chama cha Wananchi (CUF) katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kesho, umeahirishwa kutokana mkutano wa kimataifa wa uponyaji unaoendeshwa na Kanisa Katoliki, jimbo la Da es Salaam.


Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho jana, ilisema kuwa mkutano huo umeahirishwa baada ya majadiliano ya muda mrefu kati yao, Kanisa Katoliki na mamlaka za wilaya ya Ilala.

“Tumekubaliana kuwa Wakatoliki waendelee na mkutano wao wa kimataifa wa uponyaji ambao utachukua takriban mwezi mzima.


Maombi yetu na yao yalifika pamoja sasa kilichofuata ni kukubaliana na kwa sababu chama chetu hakina makuu tumekubali kuwapisha wenzetu kwa sababu itakuwa vigumu wao kukatisha mkutano wao halafu waendelee tena,” alisema Mtatiro.


Alisema kuwa walitizamia kupata kiwanja kingine lakini utafiti umeonesha uwanja huo wa Jangwani ndiyo pekee unaoweza kuhimili shughuli za chama chao kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa hiyo wanasubiri Wakatoliki wamalize kisha watafanya mkutano wao.


Mtatiro aliongeza kuwa kwa sasa wanaendelea na operesheni mbalimbali na wiki ijayo watakuwa mkoa wa Morogoro kwenye baadhi ya wilaya.


Hivi karibuni vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA vimefanya mikutano ya kuhamasisha uhai wake jijini Dar es Salaam iliyofanyika kwenye viwanja hivyo vya Jangwani na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi.

 
Nadhani huo Mkutano wa CUF ukifanyika Mh. Mwenyekiti ataacha unazi wake kama alioufanya kule kwenye Mkutano

Arusha...
 
kama ingekuwa CDM wamekutana na mishe hizi za kanisa basi wangelisema ,watu wa kanisa wametumwa na serikali ikishirikiana na chama tawala.

Ila waungwana wa CUF wamelipisha kanisa lifanye kazi yake bila ya mvutano. Na bila ya shaka yeyote ile hawa mashoga wawili CCM na CDM wamefurahi sana na kupata afuweni maana safari hii CUF wanakuja na mshikemshike wakimix crusader na jihadi kuiondoa CCM na vikaragosi vyake kwenye utawala na kusimika uongozi wa kumkomboa Mtanzania.
 
Mnaiga ....... kwa tembo, Mtapasuka. Isiwe jadi ya kwenda Jangwani hata kama hakuja hoja za msingi za kuwapa Watz. Najua mnataka kufanya kama CDM walivyofanya. Kuweni wabunifu katika vyama vyetu tusiwe kama CCM.

Asanteni mno
 
Kutokana na maelezo hayo, title ilitakiwa isomeke "CUF wasogeza mkutano wao", na sio "Katoliki wasogeza mkutano wa CUF"
 
kama ingekuwa CDM wamekutana na mishe hizi za kanisa basi wangelisema ,watu wa kanisa wametumwa na serikali ikishirikiana na chama tawala.

Ila waungwana wa CUF wamelipisha kanisa lifanye kazi yake bila ya mvutano. Na bila ya shaka yeyote ile hawa mashoga wawili CCM na CDM wamefurahi sana na kupata afuweni maana safari hii CUF wanakuja na mshikemshike wakimix crusader na jihadi kuiondoa CCM na vikaragosi vyake kwenye utawala na kusimika uongozi wa kumkomboa Mtanzania.

Hapo kwa Red ulimaanisha mtatumia mikakati wa Kidini!!
 
Msituzuge eti.viwanja vingine vidogo!!! Toka lini CUF ikajaza Mae be yanga?Ebu fanyeni tune.
 
Nduguzangu, taarifa inasema vingine nyi mwaongelea udini, mbona huku uswailini hizi tofauti hazikuwepo kwa nini mnapenda kumwagilia miche ya sumu badala ya matunda
 
Back
Top Bottom