Katika sifa hizi lazima na wewe ulikuwa nazo:

Hiyo namba 7 hiyo. Enzi hizo kukiwa na baridi unaenda kuoga unanawa mikono, miguu na kichwa, wazazi walipositukia mchezo, ikawa kila nikimaliza kuoga wanaangalia tumbo kama lina hali ya usafi. Nikabadili na kuongeza tendo la kulowanisha tumbo. Tehe tehe tehe, enzi hizo we ziache ziwe hivyo tu.

hahahahah umeniacha hoi mkuu...
 
jikoni hudokoi unaonja, si unajua mpishi lazima aonje? mradi hashibii humo humo?

3,4,5,6, na 7 sijafanya, ila la kikojozi mpk miaka 10 mi nlikua kikojozi, tena wakati mwengine hata nikishighulishwa na michezo basi siwahi fika chooni mara najikojolea kwenye puru.
Kudokoa mpk leo, ha ha heh, bt nadokoa nkipika mwenyewe jikoni
 
hahahahah cantalisia inaelekea walikuwa wanakuenjoy sana, maana walijua tu huyu leo kilio atakachoshusha si mchezo...


No tatu nilikomaa nayo mpaka nikiwa fom tuu,
Na mama alikua anajua kbs bila nguo mpya siku ya sikuuu hata lipikwe pilau sitakula ni kilio mwanzo mwisho,
Mara nyingi walikua wanatununulia alafu yangu wanaificha na kunambia hawakupata zaizi yangu eti kwa vile nilikua mnene hapo ndio nilikua naachia bonge la kilio mpaka wanaitoa na kunikabidhi!!
 
No. 4 sijawi ila mengine yote ilikuwa mchezo/mtindo mmoja....

sababu za kutokuteleza no. 4 ni kwamba nilikuwa napenda sana shule.
 
kwa maelezo haya inaelekea ulikuwa unapenda sana kucheza kwenye mvua wewe.....ukirudi nyumbani umelowa chapaaaaaaa

Nilikuwa naogopa kucheza kwenye mvua kwa sababu mama alikuwa mkali sana. Nikifanya upuuzi tu nikirudi home lazima nichee viboko.
 
kipindi hicho mchafu kama nini kila siku dada wa nyumbani lazima afue nguo zangu za shule kisa mpira akabuni kamtindo hako kila ukirudi home kama ni msafi basi anakupa sh 20 kwa ajir ya shuleni kesho we nilikuwa bonge la msafi mpaka nikapewa cheti kumbe siri ya mafanikio ni sh 20 toka kwa dada
 
3, 4 na 6 hizo sikupitia kabisa, zingine zote kama kawa! Ila namba 8 hiyo naikumbuka mpaka leo! Babaangu alinichapa kikatili sana tena kwa mpira, jirani na nyumba yetu kuna jamaa alikuwa akitengeneza 'kobazi' (aina fulani ya kandambili zinazotengezwa kwa matairi ya gari) ndipo alipochukua kipande hicho cha mpira, akanicharaza nacho mpaka mwili wote ukavimba vimba! Kimsingi yeye ndiye aliyenisababishia hayo kwani mama alisafiri na yeye aliondoka mapema bila kuniandalia chai, njaa kali + umri mdogo = .....!!
 
Hajambo GC..
Yule nliekuona nae siku ile mzima? Hukunipa hata utambulisho..mh! Btw haukuwa unakimbia shule utotoni wewe?!

Amyner.. May my mother's soul RIP!

Alinilea pasipo kunipigapiga hovyo.. Lakini alinitune nikawa mtoto aliyelelewa vema kabisa..

Imagine nilikuwa nalia siku nayoumwa na kuambiwa nisiende shule,naona kama masomo nayakosa,na nitaachwa mbali na wenzangu! Nikipoteza penseli naogopa kupokea ya mtu mwingine akinipa,ntaandikia tu kuiacha,siwezi kurudi nayo nyumbani!

Ningeulizwa umeitoa wapi,ukipoteza useme...usipende kuchukua cha mtu..n.k.

Hivyo yaani..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom