Katika mikasa ya Biblia, Mungu ameshawaua watu 2,800,000, wakati Shetani ni Watu 10 tu!

Umeielewa Thread lakini... ?? Chanzo kikubwa Cha Mungu kuwaangamiza Binadamu ni Dhambi .. Kwahiyo Mungub Amewaangamiza Zaidi Watu wengi Kulingana Na Dhambi zao ..Ndo Kichwa Cha Thread na Picha.. Hakuna Anayemlaumu Mungu ni Muuaji

Kubadili maneno na lugha (kuangamiza km) hakuondoi maudhui ya mada kwamba "Mungu ni muuaji".
 
Kwani nini Maana Ya Maneno haya

MUNGU ANATOA NA MUNGU ANATWAA JINA LAKE LIMIDIWE MILELE,,,,

Unataka kuyaeleza yaeleweka kwa jinsi unavyotaka wewe na ufahamu wako wa kibinadamu! Hata kwa ufahamu huo, sentensi hiyo ni nahau/msemo ambao unahitajika kutafakuriwa kwa umakini na kina.

Kwa ufupi "maneno hayo" ni hitimisho la sisi binadamu la kukubali adhabu ya mauti aliyopewa Adamu na kurithiwa na sisi.

Narudia tena, maneno na maandiko ya Biblia ni maono na maonyo na Biblia si kitabu cha hadithi, japo kimesheheni hadithi. Hadithi zilizomo ni za kiiamani kumkumbusha binadamu wajibu wa kuwa mwadilifu, mtiifu, mwenye heshima ili apate utufu baada ya kifo chake.

RGforever, wewe je? Lakini kama huna imani, Biblia ni kitabu kama vitabu vingine, japo kwa ukweli kimesheheni masuala ya kisayansi ambayo elimu ya sayansi ya binadamu hajifikia.
 
Unataka kuyaeleza yaeleweka kwa jinsi unavyotaka wewe na ufahamu wako wa kibinadamu! Hata kwa ufahamu huo, sentensi hiyo ni nahau/msemo ambao unahitajika kutafakuriwa kwa umakini na kina.

Kwa ufupi "maneno hayo" ni hitimisho la sisi binadamu la kukubali adhabu ya mauti aliyopewa Adamu na kurithiwa na sisi.

Narudia tena, maneno na maandiko ya Biblia ni maono na maonyo na Biblia si kitabu cha hadithi, japo kimesheheni hadithi. Hadithi zilizomo ni za kiiamani kumkumbusha binadamu wajibu wa kuwa mwadilifu, mtiifu, mwenye heshima ili apate utufu baada ya kifo chake.

RGforever, wewe je? Lakini kama huna imani, Biblia ni kitabu kama vitabu vingine, japo kwa ukweli kimesheheni masuala ya kisayansi ambayo elimu ya sayansi ya binadamu hajifikia.

Unamaana Gani Unaposema Si Kitabu Cha Hadithi ila Kimesheni Hadithi Za Kiimani au Ikishakuwa kiImani Si Hadithi

Maandiko ya kwenye Biblia ni Masimulizi Ambayo Yalikuwa yanasimuliwa Kutoka Mtu mmoja Mpk Mwingine mpaka Pale Tulipopata Uwezo Wa Kuyaandika..
 
Kama unadhani ni kweli aliwaua basi ni haki yake maana ndiye aliyewaumba.

Ni kama vile wewe unavyoamua kubomoa kibanda chako ulichojenga mwenyewe kwa maana ni Mali yako hukupewa na mwengine.

Ova and out
 
Apollo: ni siku mpya na kumekucha salama.

Mjadala tutauendeleza baadaye, ngoja tufanye kazi kwanza. Ila imani inabaki imani tu, hakuna ushahidi ila rohoni mwako mwenye kwa jinsi ileile ulizaliwa mwenyewe utakufa mwenyewe na utahukumiwa mwenyewe.

Siku na kazi njena

Asante. Kazi njema ndugu.
 
"RGForever" ni Biblia gani uliyonayo au unasoma!

Mauti ni adhabu aliyopewa Adamu kwa kutokutii amri ya Mungu kwa udanganyifu alioufanya Shetani kwa Hawa.

Kitabu cha Biblia cha "Mwanzo 3:19 - kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi".

Hivyo si kweli dai lako kwa kuwa mauti ni dhambi ya asili kutoka kwa binadamu wa kwanza Adamu na Hawa
Kwa hiyo paka, chura, mende, njiwa, na wanyama wengine wote wanakufa kwa kosa alilolifanya adam?
 
Mungu ndo anayeuwa watu siku zote bana, mnabisha nini? Shetani hana mamlaka ya kuua labda Mungu aruhusu, hivyo hakuna watu waliouawa na shetani kwenye biblia bila Mungu kuruhusu, jamani kwani kufa s ni lazima au tumesahau,,,, umeumbwa kwa udongo utarudi kwa udongo hakuna la kujitetea,,,,, bwana alitoa bwana ametwaa, mbona imekaa vizuri tu
Kama ndio hivyo basi mungu anaroho mbaya sana kwasababu kuna watu wengine huwa anawauwa vibaya mno harafu kwa mpigo.
 
Mtoa mada, MUNGU si mwanadamu na hajadiliki wala kufikirika, nawashangaa mods wanaiogopa ccm kuliko Mungu, uzi wa kuikosoa ccm unafutwa fasta, lakini uzi wa kishenzi Kama huu wa kumjadili Mungu unaachwa, eti watu wanamchambua Mungu, this is more than crazy.
Unamaana Gani Hajadiliki?au kufirika.... Hao wachungaji wanaposema Tusome Biblia ili kumjua na kumfahamu Mungu wanamaana Gani... Au mnapochambua maandiko huwa mnatafuta nini
 
Ni maswali mazuri ambayo hayawezi kujibiwa kwa ufahamu wa kidunia.

Mungu alimwadhibu Adamu kwa kutenda dhambi ya asili (Mwanzo 3:3 - lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa".

Katika adhabu zote alizowapa binadamu kwa dhambi (tafsiri ya asili maana yake binadamu hakumbwa na dhambi) aliyotenda Adamu, ni MAUTI.

Hivyo kubatizwa, kwa Wakristo huondolewa tu hiyo dhambi lakini siyo zile adhabu alizopewa Shetani (Mwanzo 3:14-15) Adamu (Mwanzo 3:16-19).
Tunabatizwa kuondolewa dhambi ya asili,but adhabu.zetu zinakuwa pale pale??

Mkuu ebu jaribu kufafanua,km kifo n adhabu ya kosa ya dhambi ya Asili..hv sasa nmebatizwa na kuondolewa hiyo dhambi ..sasa inakuwaje napewa adhabu.kwa kosa ambalo sina??

Yaan nasamehewa kosa ila adhabu pale pale...n km msamahama.batili.hv
 
Kama unadhani ni kweli aliwaua basi ni haki yake maana ndiye aliyewaumba.

Ni kama vile wewe unavyoamua kubomoa kibanda chako ulichojenga mwenyewe kwa maana ni Mali yako hukupewa na mwengine.

Ova and out
Kwahiyo ni haki kuua mwanao sababu umemzaa??
 
Week hii tumepokea mashtaka mengi sana ya taasisi ya 'Kiungu', na Kwa kuwa tuhuma hizi hazijathibitishwa mpaka sasa,na kwa kuwa inaonekana kuna nguvu kubwa sana inatumika kumharibia sifa ndugu shetani basi itamkwe wazi kwamba mashtaka yote yanayoelekezwa kwa ndugu huyu yasitishwe mara moja hadi pale itakapothibika bila kuacha shaka kwamba mtajwa ndiye aliyesababisha dunia isiwe sehemu tulivu ya kuishi,aidha pia katika kipindi hiki Shetani arudishiwe mamlaka yake chini ya jopo maalum la kuangalia mienendo yake!
 
wokovu ndo unaondoa dhambi,nani kakuambia kubatiza watoto ni sahihi?
Hv unafahamu.kwa.wakristu wanabatizwa??

Hv unajua maana.ya wokovu,na nani anae thibitisha kuwa ww tayar huu mwokovu???

Au unazan kwenda kanisankwa.walokole,kuimba pambio, kusoma.biblia sana basi.ww ndio mwokovu.....??

Wapi wameeandika kuwa kubatiza wtt sio sahihi??

Pamoja.na.iman zenu.ndan kitabu kimoja bado mwajichanga??

Jaribu.soma.kitabu kinaitwa biblia.vizur,sio kile walicho punguza vitabu..no..soma.biblia yote iliyo kamilika na tafuta nn maana ya dhambi ya asili na vipi biblia husema kuhusu kuondolewa hiyo dhambi ya asili

Hapo ndipo utajua smtym huyu mungu mnae mwabudu n.jinsi.gan alivyo mafia ya boko haramu
 
Back
Top Bottom