Katika kupambana na uhalifu,Polisi zingatieni yafuatayo:-

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Polisi muimarishe yafuatayo ili kudhibiti uhalifu Nchini:-
1. Muimarishe Polisi Jamii na muwaimarishe kimbinu na kizana.
2. Polisi muwe wasiri kwa taarifa mnazopata kutoka kwa raia wema.
3. Muweke wazi njia za kupata taarifa kutoka kwa wananchi kama namba za simu na barua pepe na namna nyingine mtakayoona inafaa kupatia taarifa.
4. Muitikie/mfanyie haraka wito kutokana na taarifa mnazopata.
5. Mtoe motisha kwa watoa taarifa zenye kufanikisha lengo.
6. Mjichunguze nyie wenyewe ili kujiridhisha kuwa wote mu wamoja kwani huweza kuwepo wasaliti miongoni mwenu.
7. Raia wema wanawapa taarifa sahihi muwape namba ili muweze kuwatumia katika kazi zenu.
KILA MMOJA AONGEZEE MAONI YAKE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom