macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,770
- 39,555
Dopas!Asante kwa post yako.
Nampongeza Zito.
Chadema ni lazima ilifanyie kazi suala la kupata matukio ya mikutano ya kampeni. Tukitegemea vyombo vya ccm hatuambulii kitu. Tazama picha za wapinzani anazotela michuzi, ovyooooooo. Afadhali angeacha tu. Linganisha na za ccm anazoleta.
Wiki tatu zilizopita tulilalamika kuwa michuzi haleti habari kwa uwiano sawa wengine wakamtetea. Lakini ukifuatilia habari za kampeni huhitaji kuambiwa kuwa ameegemea kwa upande gani. Kwa hakika yupo mpiga debe wa ccm 99%. Fuatilia habari na picha anazotuma utaona.
Kwa maoni yangu michuzi aache kuleta matukio ya kampeni ya vyama vya upinzani. Aambatane na ccm na Jk wake, kuliko kutuhadaa.
Blog ni ya Michuzi na yeye ndie anayeamua aweke nini na aache nini! Kama yeye anaona CCM ndio wanamlisha unafikiria atawaumbua? Ushauri wangu ni kwa watu wengi kadiri inavyowezekani waanzishe blog ili kuwe na ushindani. Hii itawafanya wale wenye kuegemea ufisadi kama Michuzi wafe kifo cha mende kwani wakikosa watu wa kutembelea blog zao watazifunga. Hapa JF kuna waandishi wa habari wengi tu na wanaweza kuifanya hii kazi ya kummaliza Michuzi.....