Katika hili la waraka, TUKTA sio walewale waliokosa?

Nono

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
1,536
643
Kwanza kabisa, naunga naunga mkono waraka wa Kanisa (hakuna swali hapa).
Ila, kauli ya viongozi wa TUKTA inakatisha tamaa kiasi kikubwa na kuonyesha jinsi viongozi hawa wanavyojipenda wenyewe kuliko Watanzania na vizazi vijavyo. Iweje leo hii waone sababu ya kuandaa waraka baada ya kuambulia ongezeko la 4000 kwenye mishahara yao? Je, wafanyakazi wakiHONGWA hiyo 315,000 wataacha uchafu uendelee kama kawaida? Je, hi sio njia ya kutafuta nafasi ambayo wanashtuka leo kuwa waliachwa nje? Wako wapi siku zote kukemea maovu yote yanayoendelea? Hii nchi imekuwa ya makundi ya maslahi tu!
TUCTA yaikamia CCM 2010
TAMKO lililotolewa na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), huku wakitangaza kuunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki, linahofiwa kuweza kukisambaratisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi mkuu mwakani, baada ya serikali kuongeza sh 4,410 kwenye mshahara wa kima cha chini.
……………………Huku akishangiliwa na wafanyakazi walioshiriki maandamano hayo, Mgaya alisema vyama vya wafanyakazi havikuhusishwa kuandaa ongezeko hilo kama yalivyo makubaliano ya TUCTA na serikali, bali limetolewa kinyemela, hatua aliyotahadharisha kuwa ni hatari, kwani inawagonganisha viongozi wa TUCTA na wafanyakazi.
………………..Alisema TUCTA inaitaka serikali ilipe sh 315, 000 kama kima cha chini kwa mwezi, vinginevyo hawataiunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao.
……………………………………….."Tunapenda kuitahadharisha serikali kwamba kupuuza suala la mishahara ya wafanyakazi ni jambo la hatari sana na kwa vyovyote vile, litaigharimu kwenye uchaguzi mkuu mwakani," alisema.
…………………."Wafanyakazi wote tumeungana chini ya umoja wetu kudai haki kwa amani, hizo zote ni ishara za watu kuchoka, wanajua jinsi wakubwa wanavyoitafuna nchi kwa ufisadi, wananchi hao wakiungana na waraka wa Kanisa Katoliki, CCM imekwisha," alisema mfanyakazi, Musa wa mkoani hapa.
………………………."Sisi wafanyakazi ni waelewa na ni wasomi, endapo tutaamua kwa nguvu kusimamia msimamo wetu kuungana na waraka huo, itakuwa hatari kwa CCM, kwani inaweza kusambaratika, maana laana ya kuwadharau wafanyakazi itawatafuna," alisema.
Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=8791
 
Haya yote ni matokeo ya utawala usiojali maslahi ya watu wa chini na wa kati. Haiingii akilini kwamba mishahara ya wachache ambao ni wa-Tanzania kama wengine kuwa juu hata uwiano wake haulinganishiki kabasa wakati linapokuja suala la kununua mahitaji bidhaa zote zinabei sawa na haziwapi unafuu walio wa chini. Hali hiyo kwa vyovyote ikiendelea kwa muda mrefu huleta matabaka ya walio nacho na wasionacho. Mwanzoni mwa hatua hiyo watu huwa wazito kudai haki yao, na itafika muda hawatavumilia tena na hivyo kuanzisha vita kwa kutumia silaha ambayo wataona ni mwafaka kwa wakati huo.

Hivyo umoja wa wafanyakazi kupitia TUCTA uko kwenye vita na mfumo wa utawala wa Serikali ya Tanzania kwa kutowajali kwa muda mrefu hatua iliyosababisha wawe wenye maisha ya chini kwa muda mrefu. Wanaona silaha yao iliyo hatari na imara kuuangusha mfumo huu wa Serikali ni kutumia Waraka kuuunga mkono Waraka uliotolewa mapema na Wakatoliki maana wanaona kwa kufanya hivyo kwa asilimia kubwa watakuwa wamemlenga adui utosini.

Nani alaumiwe katika hili? TUCTA katika Waraka wao wamesema Serikali pamoja na wao walikubaliana kwamba, kunapotokea suala la kuongeza mishahara inabidi pande zote mbili zikae pamoja na kujadili namna ya nyongeza tarajiwa. Pamoja na makubaliano hayo Serikali imeongeza mishahara (TUCTA wanasema siyo nyongeza ila ni kuwadhalilisha watu wa kima cha chini na kati) pasipo kuwashirikisha TUCTA kwenye mchakato huo. Sasa nani alaumiwe hapa? Je, ni Serikali kwa kutowashirikisha TUCTA na kutoa nyongeza ya mshahara ambayo hata bajeti ya siku moja ya mkazi wa Dar es Salaam haimtoshi kukidhi mahitaji? Au ni TUCTA walaumiwe kwa hatua yao ya kuchukizwa na Serikali kwa kuwadhalau na kuwatukana kwa kuongeza nyongeza kwa mshahara wa mwezi isiyozidi sh. 4,000? Jibu hapa kwa maoni yangu ni Serikali inapaswa ilaumiwe zaidi.

Jana wakati nachangia hoja moja katika forum yetu hii niliongelea mazoea machafu ya Serikali yetu kutosamini wataalam waliopo. Wakati huo huo wanatumia bilioni nyingi kila mwaka kuwakopesha vijana wasome ili kuupata utaalamu huo kwa manufaa ya nchi. Lakini manufaa hayo hayawezi kupatikana kwa vile Serikali ambaye ndiye mlezi na mwajiri mkuu wa wahitimu huwa hawasamini. Masuala mengi ndani ya nchi yetu hufanywa pasipo uchambuzi wa kitaalamu kitu ambacho ni hatari sana. Utafikiaje maamuzi fulani pasipo kufanya uchambuzi wa kisayansi ili kujua faida na hasara za uamuzi husika?

TUCTA wako kwenye vita na Serikali juu ya kutowajali kwa muda mrefu, hivyo wasifundishwe silaha ya kumpigia adui yao. Wao kama maamuzi yao yamefanywa kwa uchambuzi zaidi na kuona waraka huo utakuwa mwafaka kuleta mabadiliko kwa wakati huu, waachwe wafanye kazi yao.

Ndugu Nono wakati anaandika hoja yake ameiweka kuwa ya jumla mno pasipo kufafanua hasa ni nini kinachopelekea TUCTA (yeye ameandika TUKTA) awepe lawama na kuonekana kama tu wakurupukaji. Ni ombi langu kwa wachangiaji wa watoka hoja tuwe tunajitahidi kutoa ufafanuzi zaidi juu ya tunachokiongelea ili hata wachangiaji wengine wachangine wakiwa na maana halisi ya hoja husika.

NB: Kupanga nyumba Dar es Salaam sasa hivi ni kuanzia sh. 150,000 kwa nyumba ya kawaida tena vyumba wiwili na sebule. Je, mshahara wanaopewa watumishi wa kima cha chini ni halali kuwafanya waishi Dar es Salaam? Kuna haki hapo?
 
Kwanza kabisa, naunga naunga mkono waraka wa Kanisa (hakuna swali hapa).
Ila, kauli ya viongozi wa TUKTA inakatisha tamaa kiasi kikubwa na kuonyesha jinsi viongozi hawa wanavyojipenda wenyewe kuliko Watanzania na vizazi vijavyo. Iweje leo hii waone sababu ya kuandaa waraka baada ya kuambulia ongezeko la 4000 kwenye mishahara yao? Je, wafanyakazi wakiHONGWA hiyo 315,000 wataacha uchafu uendelee kama kawaida? Je, hi sio njia ya kutafuta nafasi ambayo wanashtuka leo kuwa waliachwa nje? Wako wapi siku zote kukemea maovu yote yanayoendelea? Hii nchi imekuwa ya makundi ya maslahi tu!

Katika uchaguzi mkuu wafanyakazi ndio hutumika kama wasimamizi wa vituo na makamishna ngazi mbali mbali, Ni wazi basi kuwa wizi wa kura unaofanyika wao wanahusika moja kwa moja.
Hayo ndiyo malipo kwa kazi yenu nzuri ya kusaidia wizi wa kura.
MNAPASWA KUBADILIKA!!
 
Katika uchaguzi mkuu wafanyakazi ndio hutumika kama wasimamizi wa vituo na makamishna ngazi mbali mbali, Ni wazi basi kuwa wizi wa kura unaofanyika wao wanahusika moja kwa moja.
Hayo ndiyo malipo kwa kazi yenu nzuri ya kusaidia wizi wa kura.
MNAPASWA KUBADILIKA!!

Hili nalo ni tawi lingine la CCM. Siku zote walikuwa wapi ndo leo wanakumbuka waraka? UFISADI wote huu unaoimbwa kukicha wamefanya nini kuwahamasisha wafanyakazi? Wanaonekana kwenye MEI MOSI tu! Hata na hii fedha wanayokata wafanyakazi wanaifisadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom