Katika Hili kweli PINDA Kapinda kwelikweli.

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
1,017
256
Nashindwa kuelewa kwamba ni uzembe au ulevi wa madaraka au ndio uwezo wake wachambua mabo ulipofikia. Pinda anawezaje kuwambia watu haohao, siku hiyo hiyo, wakati huohuo na sehemu hiyo hiyo, kauli mbili zinazo pingana na kutaka watu wote waamini kuwa yuko sawa. Akizungumzia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha Bungeni Pinda alidai, ''Kwa hesabu za kawaida hata mtoto wa darasa la saba anjua kuwa CCM yenye wabunge 16 haiwezi kushindwa na Chadema yenye wabunge 14.'' Lakini Pinda huyo huyo analiambia bunge, Uchaguzi wa naibu meya ulifanyika na diwani wa TLP ambaye yuko mmoja tu aliwashinda wabunge 16 wa CCM, tana kwa kura zote 17!!. Sipendi kuamini kuwa PM ni kihiyo lakini kwa uelewa huu, bora aende akaendeleze ukulima wake huko Katavi.
 
Kumbukeni alishakiri kwamba Mafisadi wana nguvu sana kuliko serikali yake.....

sasa huyu ni Waziri Mkuu kweli au kivuli?
 
Kwa upande wake, mshtakiwa huyo aliomba apunguziwe adhabu kwa madai kwamba ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pamoja kusumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu sasa.
 
Mbona sielewi! au channels zimeingiliana?
 
Kwa upande wake, mshtakiwa huyo aliomba apunguziwe adhabu kwa madai kwamba ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pamoja kusumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu sasa.
Njaa mbaya!!
 
Back
Top Bottom