YanguHaki
Senior Member
- Oct 11, 2010
- 129
- 9
Kuondokana na maneno yanayoweza kutuvunjia amani katika taifa kama "tangazeni kisha wao wataenda mahakamani" tuliyoyasoma humu jamvini napendekeza kwenye chaguzi zote nchini matokeo ya uchaguzi yatangazwe kama kawaida lakini kuwe na chombo ambacho sio mahakama chenye mamlaka ya kusikiliza malalamiko ya wagombea. Kitengue ushindi kama kitajiridhisha kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi au kimthibitishe mshindi kama hakuna malalamiko yoyote. Hiki chombo kwanza kitasaidia kuondokana na gharama kwa serikali kuendesha kesi nyingine zisizo na kichwa wala miguu tunazozisikia kwenye vyombo vya habari. Mahakama ibakie kama chombo cha rufani kwa mlalamikaji na pia kesi isizidi miezi mitatu kumalizika toka kuapishwa kwa mbunge.