Katika CHADEMA haiwezekani kuwa na makundi ya urais

Dec 27, 2011
27
38
Wakuu,
Nimeona habari hii iliyopostiwa na Samson Mwigamba yule Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, kwenye mitandao ya wanabidii na mabadiliko. Nimeona niyaweke hapa maelezo yake ili tuyajadili:

Soma kwanza Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 katika sura ya saba ibara ya saba:

VII. SURA YA SABA
7.0 NGAZI, UONGOZI NA MAJUKUMU YA VIKAO

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea wa Urais na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.
Kwa wenye kumbukumbu iliandikwa kwenye magazeti kadhaa mwaka juzi kwamba Kamati kuu ya CHADEMA ilitumia kampuni ya utafiti ya nje ya nchi ambayo iliwasilisha utafiti wake kwa kamati kuu ulioonyesha kwamba kwa wakati huo mwanachama ambaye wananchi walikuwa wakimkubali zaidi kwenye nafasi ya urais ni Dr. Willibrod Slaa na kamati kuu ikampendekeza kwa baraza kuu ambalo nalo lilimpitisha na hatimaye akapitishwa na mkutano mkuu. Kwenye CHADEMA hakuna mtu kukurupuka huko na kuchukua form ya kugombea urais. Hiyo ilifanyika mara moja tu mwaka 2005 na haitarudiwa tena. Ndiyo maana tunasema haiwezekani Mbowe, Slaa na Zitto wapambane kwa ajili ya urais wa 2015.
Wote wanajua kwamba ni utafiti tu ndio utakaomwibua mmoja wao kugombea na kwa hiyo wanachokifanya sasa ni kupiga kazi ya kulisaidia taifa. Atakayetakiwa na wananchi (si wanachama maana utafiti unacover watanzania wote si wanachadema tu na kimsingi chama kinatafuta mtu atakayekubalika kwa watanzania) ndiye atakayeteuliwa na vyombo husika. Hizi zingine ni propaganda tu wala hakuna ugomvi wa urais ndani ya CHADEMA. Kikombe hicho cha makundi ya Lowassa, Sitta na Membe, yanayokitesa chama tawala sisi CHADEMA Mungu alishatuondolea kwa kutupatia ufunuo wakati tunabadilisha katiba mwaka 2006. Endeleeni kuparurana tu wenyewe huko kwenye Chama Cha Magamba (CCM) msitake kuwalaghai watanzania kwamba hata CHADEMA wanaparurana.
 
Hapo lazima uangalie yafuatayo:

a. Tender process ya kupata kampuni kufanya utafiti

b. Kina nani watakaopitisha (wajumbe) kwa kampuni? wangapi

c. Sample itakayotumika kuona mtu fulani anayefaa zaidi kuliko wengine

d. Methodology itakayotumika, etc

hizo zote ni areas ambazo zitaleta matatizo makubwa ki-demokrasia na ni oppportunity ya kuwepo upendeleo mkubwa katika kupata nafasi hiyo..

hope this is not true
 
Mambo ya kampuni tena kusaka mgombea. Hii inamaanisha kuwa wanachama na wasio wanachama lakini wanpenda chama hawaaminiwi.
 
Watu wa magamba mnaweweseka tu, yote hayo ni headache ya chama chenu kushindwa kutatua kitendawili cha "namna ya kumpata mgombea". Tupo hapa na natumaini JF itakuwepo for much longer tuone, kwanza uchaguzi wenu wa ndani this year then 2015 candidate nightmare.
 
CDU au sio?

vichwa vya waislamu viko kama tep ukirekodi kitu hata kama ni matusi kinarudia hivyohivyo mpaka siku kitakapofutwa na kurekodiwa kingine.
poleni ndiyo kazi aliyowaachia mtume pamoja na kumwomea ili amwone mungu kwani bila nyie watakatifu kuliko yeye hataionja pepo.
 
Back
Top Bottom