Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali afariki dunia

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali Bajoji amefariki dunia jana akiwa nyumbani kwao Kyela.

Aliumwa ghafla na juhudi za kumkimbiza hospitali hazikuzaa matunda. Inasemekana kafa kwa pressure.

Pole sana kwa ndugu na marafiki wa Bajoji.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, AMEN!.
 
Comarade Bajoji Zacharia,kijana na kiongozi wa muda mrefu wa Umoja wa Vijana wa CCM kabla ya kwenda Chama,tutakukumbuka daima kama mpiganaji na kamanda madhubuti wa timu imara......Mungu ailaze mahali pema peponi roho yako.
 
Poleni sana ndugu, jamaa, marafiki na wana CCM kwa kumpoteza Comrade Bajoji
 
Mkuu Mtanzania,

Hii taarifa imenishtua sana. Ninamwombea ndugu yetu Bajoji amani ya milele kwa Bwana. Ameni.
 
Mkuu Mtanzania,

Hii taarifa imenishtua sana. Ninamwombea ndugu yetu Bajoji amani ya milele kwa Bwana. Ameni.

Huwezi kumwombea mtu amani ya milele akishakufa. Huo ni kama usanii tu.
Hapa naomba faraja kwa wafiwa.
Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha kuondokewa ndugu yao.
 
Poleni sana ndugu, jamaa, marafiki na wana CCM kwa kumpoteza Comrade Bajoji

Nimewahi kufanya kazi na Bajoji kwa kipindi cha miaka 2,ni mtu wa mikakati ya ushindi ndani ya "Mtandao" wa Kikwete mwaka 2005 na mtu wa karibu na Nchimbi Emanuel na kundi lake.

Najua kina Makala na Nchimbi wamempoteza mmoja wa wapiganaji wao mahiri kwenye kambi yao ya "Agenda 2015". Poleni wafiwa na mungu awape subira!!
 
Huwezi kumwombea mtu amani ya milele akishakufa. Huo ni kama usanii tu.
Hapa naomba faraja kwa wafiwa.
Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha kuondokewa ndugu yao.

Kwani amani maana yake nini? Hivi hujui kwamba milele ina-imply beyond death?
 
Mungu hailaze roho ya marehemu mahala panapostaili kwa matendo aliyoyatenda hapa ulimwenguni. Amen
Poleni wana CCM
 
Back
Top Bottom