Katibu wa CCM auawa kinyama

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
561
422
KATIBU kata wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Iringa Vijijini, Patrick Ng’ara (40), mkazi wa kijiji cha Ilandutwa, ameuawa kinyama kwa kucharangwa mapanga akiwa nje ya nyumba yake usiku wa kuamkia jana.

Mauwaji hayo ya kinyama kwa kiongozi huyo wa CCM kata ya Mgama yamekuja siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa upande wa Tanzania Bara, John Chiligati, kuelezwa wazi wazi na diwani wa kata hiyo ya Mgama, Denis Lupala, kuwa hafai ndani ya CCM na ni mmoja wa waliotakiwa kuvuliwa gamba Dodoma.

Mjane wa marehemu Tumain Ndendia (36) alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 2.45 usiku wakati katibu huyo akitoka katika vikao vya chama.
Alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea yeye na mtoto walikuwa ndani wakijiandaa kulala na ghafla alisikia sauti ya kishindo nje mfano wa kitu kuanguka chini na baada ya kutaka kutoka alisikia sauti za watu wakishauriana kuingia ndani kufanya mauwaji.

Mtu kauawa kisa??????????????

Source: TANZANIA DAIMA.
 
UJAMBAZI UTAKOMA LINI...
WITO:
WANANCHI WENYE NIA NJEMA,TUUNGANE KUUTOKOMEZA UJAMBAZI KWA MAREFU NA MAPANA YAKE.....TUWEKE TOFAUTI ZETU PEMBENI NA TUMVAE ADUI POPOTE ALIPO....!
Leo ameanza Iringa kesho atakuwa wapi?
TANZANIA........UNITED WE STAND....!
 
UJAMBAZI UTAKOMA LINI...
WITO:
WANANCHI WENYE NIA NJEMA,TUUNGANE KUUTOKOMEZA UJAMBAZI KWA MAREFU NA MAPANA YAKE.....TUWEKE TOFAUTI ZETU PEMBENI NA TUMVAE ADUI POPOTE ALIPO....!
Leo ameanza Iringa kesho atakuwa wapi?
TANZANIA........UNITED WE STAND....!

Kweli ujambazi upo lakini kwa hili wala mimi naona kama imepangwa kabisa kwa sababu, we mtu kasemekana tu hafai halafu siku chache tu hayupo tena, inamaanisha nini???????
Nahisi kuna jambo hapo.
 
Dah! kataka katibu Mkuu Taifa avuliwe gamba yeye wakamvua roho! 2ko pamoja nao ndg wa marehemu pia 2natoa pole kwa wafiwa wote.
 
naona inakuwa ngumu kwa gamba kuvuka, so, wasio na magamba ndio watakao umia mwaka huu!
 
Hapa inatakiwa Chiligati atoe tamko la kulaani kitendo hichi, na kusii dola ifuatilie tukio hili/ sheria ichukue mkondo wake..

KATIBU kata wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Iringa Vijijini, Patrick Ng’ara (40), mkazi wa kijiji cha Ilandutwa, ameuawa kinyama kwa kucharangwa mapanga akiwa nje ya nyumba yake usiku wa kuamkia jana. Mauwaji hayo ya kinyama kwa kiongozi huyo wa CCM kata ya Mgama yamekuja siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa upande wa Tanzania Bara, John Chiligati, kuelezwa wazi wazi na diwani wa kata hiyo ya Mgama, Denis Lupala, kuwa hafai ndani ya CCM na ni mmoja wa waliotakiwa kuvuliwa gamba Dodoma.

[... ]Kifo cha katibu huyo kimetokea huku kukiwa na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao na wale wa wilaya, mkoa na taifa baada ya diwani wa kata hiyo Lupala kumvaa Naibu Katibu Mkuu Chiligati kuwa kati ya watu ambao walitegemewa kuvuliwa magamba ndani ya CCM

chanzo cha habari :
Tanzania Daima, jumamosi, 23 aprili 2011
 
Magamba mengine ni magumu sana kuyaondoa. Wanaodhamiria kuvua magamba ya wenzao inabidi wawe makini game lisiwageukie wao kama yaliyomkumba marehemu.
 
katibu pumzika kwa amani na mwanga wa milele bwana atakuangazia...
 
tutasikia mengi kuhusu haya magamba mwaka huu...time will tell,mafia wale mapacha watatu,we subiria tu,.!!
 
Huu sio ujambazi bt Mauaji ya Visasi, ndani ya Chama eneo lake kuna mambo hayapo sawa!
 
Kauawa Patrick Ng'ara. Aliesema Chiligati hafai ni Denis Lupala.

Msipende kuona mnavyotaka kuona hata kama CCM twaichukia.
 
Back
Top Bottom