Katibu wa BAVICHA Njombe Kusini afariki dunia!

Kila jambo lina majira yake, na kuna wakati kwa kila jambo. Familia, Ndugu, jamaa, marafiki na Wanacdm poleni.
Tuendeleze harakati za ukombozi.
 
Katibu wa Bavicha Jimbo la Njombe Kusini (Njombe Mjini) kwenye Mkoa mpya wa Njombe, Jackson Mtakimwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye Zahanati ya TANWALT mjini Njombe. Septemba 25 mwaka huu Mtakimwa alipata ajali ya Pikipiki aliyokuwa anaendesha na kupata majeraha ya mwilini na kichwani.

Alifikishwa kwenye Hospitali ya Wilaya (Kibena Hospital) ya Njombe ambapo alitibiwa majeraha hayo na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mtakimwa alikuwa ni mmojawapo wa Makamanda waliokuwa waende kusaidia Kampeni za Udiwani kwenye Kata ya Mlangali Wilaya ya Ludewa lakini aliachwa kutokana na hali yake kutotengemaa.

Juzi alianza kukohoa na kutoa damu (inawezekana alipata majeraha ya ndani kwa ndani wakati wa ajali) na alipelekwa kwenye Zahanati ya Tumaini Mjini Njombe ambapo matabibu walidai ana Typhoid hivyo kuhamishiwa kwenye Zahanati ya kiwanda cha TANWALT mpaka mauti yalipomkuta saa saba usiku wa kuamkia leo.

Jackson Mtakimwa atazikwa kesho kijijini kwao Igwachanya (Njia Panda ya Tosamaganga) kwenye Jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa.


Poleni wote kwa msiba huu. Tuchukue tahadhali tuwapo barabarani, pikipiki kama vyombo vingine vya usafiri zimekuwa tishio kubwa miezi ya karibuni na zinasababisha vifo kwa Watanzania wengi. Pumzika kwa amani katibu.
 
Back
Top Bottom