Katibu wa BAVICHA Njombe Kusini afariki dunia!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,042
33,527
Katibu wa Bavicha Jimbo la Njombe Kusini (Njombe Mjini) kwenye Mkoa mpya wa Njombe, Jackson Mtakimwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye Zahanati ya TANWALT mjini Njombe. Septemba 25 mwaka huu Mtakimwa alipata ajali ya Pikipiki aliyokuwa anaendesha na kupata majeraha ya mwilini na kichwani.

Alifikishwa kwenye Hospitali ya Wilaya (Kibena Hospital) ya Njombe ambapo alitibiwa majeraha hayo na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mtakimwa alikuwa ni mmojawapo wa Makamanda waliokuwa waende kusaidia Kampeni za Udiwani kwenye Kata ya Mlangali Wilaya ya Ludewa lakini aliachwa kutokana na hali yake kutotengemaa.

Juzi alianza kukohoa na kutoa damu (inawezekana alipata majeraha ya ndani kwa ndani wakati wa ajali) na alipelekwa kwenye Zahanati ya Tumaini Mjini Njombe ambapo matabibu walidai ana Typhoid hivyo kuhamishiwa kwenye Zahanati ya kiwanda cha TANWALT mpaka mauti yalipomkuta saa saba usiku wa kuamkia leo.

Jackson Mtakimwa atazikwa kesho kijijini kwao Igwachanya (Njia Panda ya Tosamaganga) kwenye Jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa.
 
Mungu akulaze mahali pema peponi kamanda,pole kwa wafiwa.
 
RIP Kamanda! Pole sana kwa familia na ndugu wa karibu. Poleni sana wanachadema wote na wote wanaopenda maendeleo ya Tanzania!
 
Mchango wako katika harakati za kuikomboa nchi hii unatambulika. Mungu akurehemu na akupokee katika ufalme wake
 
katibu wa bavicha jimbo la njombe kusini (njombe mjini) kwenye mkoa mpya wa njombe, jackson mtakimwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye zahanati ya tanwalt mjini njombe. Septemba 25 mwaka huu mtakimwa alipata ajali ya pikipiki aliyokuwa anaendesha na kupata majeraha ya mwilini na kichwani.

Alifikishwa kwenye hospitali ya wilaya (kibena hospital) ya njombe ambapo alitibiwa majeraha hayo na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mtakimwa alikuwa ni mmojawapo wa makamanda waliokuwa waende kusaidia kampeni za udiwani kwenye kata ya mlangali wilaya ya ludewa lakini aliachwa kutokana na hali yake kutotengemaa.

Juzi alianza kukohoa na kutoa damu (inawezekana alipata majeraha ya ndani kwa ndani wakati wa ajali) na alipelekwa kwenye zahanati ya tumaini mjini njombe ambapo matabibu walidai ana typhoid hivyo kuhamishiwa kwenye zahanati ya kiwanda cha tanwalt mpaka mauti yalipomkuta saa saba usiku wa kuamkia leo.

Jackson mtakimwa atazikwa kesho kijijini kwao igwachanya (njia panda ya tosamaganga) kwenye jimbo la kalenga, wilaya ya iringa mkoa wa iringa.

alale mahali pema, kazi yake ikumbukwe kwa vitendo lakini tuwe makini na vyombo vya moto
 
Back
Top Bottom