Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni)

ufisadi nilio uona ni huo wa kukodisha nyumba kabla ya huyo mtu hajaenda, kulikuwa na uharaka gani wa kutafuta hiyo nyumba na kuilipia? kuhusiana na mtu gani aende kati ya sawe na chale , inategemeana na serikali inataka kutimiza lipi ambalo mwanzo lilikuwa lina mapungufu, lakini kama ni ku-moderate cost sifikiri kama AMO ataliweza, kwani upeo wake kwa magonjwa makubwa ni mdogo, kwa Chale ingawa tutakuwa tuna mpoteza mtu mzuri lakini anaweza akaitumia hiyo nafasi kujifunza zaidi , ili akimaliza term yake anapelekwa mwingine kwa minajili ya kufanya hiyo kazi na kujifunza, labda tuambiwe hii pia ilikuwa ni nafasi ya sawe kufanya kazi na kujiendeleza, bila kupata machungu ya elimu yetu hapo muhimbili.
hiyo ni kawaida, popote unapotaka kuchukua nyumba huko nchi za watu inabidi ulipie deposit kwanza watu hawataki mchezo na biashara zao; na kwa nchi ni possible kuwa watataka ulipe pesa ya mwaka mzima.
 
1. MD wengi wakimaliza Tz they never practice, wapo2 tu, wengine ndo wanaingia ktk NGOs,
NGO zinazoajiri madaktari ni kama hizi zinazojishughulisha na care na treatment ya HIV/AIDS na kule wanatibu wagonjwa hivyo nashangaa unaposema hawa-practice.

wengine wengi wanaijiriwa kama watafiti..
Utafiti ni part muhimu sana ya fani ya udaktari - la sivyo hakutakuwa na advancement katika fani na katika masuala ya afya kwa ujumla - na hiyo pia ni ku-practice; ujue kabisa fani ya udaktari ina clinical na public health - na zote zina umuhimu.
na wanaopractice wengi wapoa MNH, KCMC na Bugando na private sector ktk hii miji!
Usitake kuniambia kuwa hospitali hizo zina proportion ndogo ya wagonjwa?! nitashangaa. Hospitali unazozitaja ni referral kwa hiyo zinahitaji zaidi ma-MD, kule kwingine unakosema, wapo AMO na CO wanahudumia zikiwashinda ndio wana-refer kwa hiyo hai-make sense MD kwenda kukaa kwenye dispensary ama health centre huko Busanda ama Muheza.
Hii sii tija kwa nchi at all.. nadhani kwa sasa wanamaliza kama 200-300 hivi tz..ila ukienda Baadhi ya mikoa kuna madaktari wasizidi 10! Huwa najiuliza: nchi inafaidika nini kutrain madktari ambao they dont want to practice??
Nchi ya kifisadi why should doctors care? ukikaa Dar kufanya biashara zako unakusanya milioni 1 ama 2 kwa mwezi; uende huko Nkasi, kusikokuwa na umeme, maji wala barabara halafu unapata laki 6 kwa mwezi ya nini? Wewe ndio waipenda nchi kuliko serikali au?
jamaa mmoja alienda kutibu mtwara baada ya intern, miezi sita ikapita bado hajapata mshahara ikabidi kuja kufuatilia Dar, kuja wizarani anaambiwa mtu anayeshughulikia masuala hayo yuko mkutano Arusha anarudi baada ya wiki 2, jamaa hana ndugu dar; mambo gani sasa hayo?

2. Kuwe na contract: wakimaliza intern, wapangiwe Wilayani wafanye huko kazi miaka 3-5 ndo wapata registration.
registration sio muhimu ili ku-practice udaktari Bongo, kwa taarifa yako mpaka manesi na ward attendants dar wanajiita madaktari na wanatengeneza hela hapo mjini.

3. Mikopo ya kusoma hupata bure na serikali: sasa sijui kwa nini serikali inawachia tu wote wako hapa Dar.
kwa taarifa mkopo sio hela ya bure, unatakiwa kurudisha. Na serikali ikikukopesha haiwezi kukulazimisha ukafanye kazi huko Shinyanga, au inaweza?

Tugefanya inventory toka 1990 kujua madaktari wangapi tumezalisha Tz.. na wako wapi kwa sasa.. wa je wanafanya kazi wapi..na kwa nini hawapendi kuwahudumia wananchi mikoani!
ni wazo zuri lakini kumbuka sababu ni hizo za maisha kuwa duni huko mikoani. kwani wewe uko mikoani? Kama uko Mwanza siku hizi Mwanza pia ni jiji! Na kama uko kwingine either ndio hivyo umeenda kwa hizo NGO unazoona zinaiba madaktari ama umepewa u-DMO, ama umeenda wilayani kwenu uwe karibu na your parents or something; tell us the truth.

Serikali iliongeza mishahara mara 2 wafanyakazi wa sekta ya afya 2006/07. Na July mwaka huu wataongezewa tena kiasi kikubwa!
Still not enough, kila kitu kimepanda bei - ngano, sukari, mchele, sembe, petrol; kwa hiyo tunarudi pale pale. Waongeze zaidi! At least 1.5m/mo kama take home.
 
Nchi ya kifisadi why should doctors care? ukikaa Dar kufanya biashara zako unakusanya milioni 1 ama 2 kwa mwezi; uende huko Nkasi, kusikokuwa na umeme, maji wala barabara halafu unapata laki 6 kwa mwezi ya nini? Wewe ndio waipenda nchi kuliko serikali au? jamaa mmoja alienda kutibu mtwara baada ya intern, miezi sita ikapita bado hajapata mshahara ikabidi kuja kufuatilia Dar, kuja wizarani anaambiwa mtu anayeshughulikia masuala hayo yuko mkutano Arusha anarudi baada ya wiki 2, jamaa hana ndugu dar; mambo gani sasa hayo?

Umesema ukweli kabisa....dada yangu yalimkuta kama hayo alipekwa wilayani miezi sita bila mshahara....akawa anasaidiawa na halmashauri yenye madiwani darasa la saba wengine la nne...sasa nini hiyo! Nilimwambia achana na wito wa UDr bongo haulipi...akaanza MBA sasa hivi yuko vizuri mambo ya wilayani anawaachia Old doctors wasiona malengo na maisha!
 
Kama Hansard zinavyoeleza, moja ya kazi kubwa za medical attache ni kuminimize rising costs. Then kuna umuhimu wa kupeleka daktari mwenye MD au zaidi. Sababu, inaonyesha hii kazi itakua na direct contact na madaktari bingwa wa India ambao wengi wa kwenye hizi hospitali zinazofanya medical tourism ni highly specialized doctors.

Hizi hospitali zinazofanya medical tourism zinatengeza pesa kwa principle kuu ya kumaximise service utilisation once mgonjwa anapokanyaga hospitali zao. Kwa maana hiyo kulimbikiza vipimo na madawa ambavyo vingine ni unnecessary kwa kutibu ugonjwa husika bali ni kama they do no harm.

In such as situation unahitaji daktari wa kuweza kuchallenge such indications professionally, na ndio maana hata health insurance companies kubwa zina medical directors ambao ni MD au zaidi kwa kuchallenge unnecessary/inappropriate vipimo au madawa ambayo yanaongeza gharama.

Mambo ya logistics za airport na kupokea wageni si kazi kuu ya medical attache, kuna maafisa ubalozi wengine wanaweza kuifanya hii. Medical attache anatakiwa apimwe kwa cost minimisation
per case, sio kwenda likizo india.

Ingawa kwa wasifu na ubingwa wa Dr Chale, naona anahitajika zaidi nyumbani kuliko huko ubalozini. Atafutwe mtu mwingine mid-career MD aliyepractice kazi yake, sio desk officer wizarani.

Kwa advancement ya tiba za kileo, AMO hana ubavu wa kuhold proffesional discussion na kumchallenge a seasoned super specialist wa India.
Mgonjwa anapelekwa India kwa kua mabingwa wetu wameshindwa, hivyo kimsingi DR Bingwa wetu hatakua na face ya kuchallenge treatment plan ya mabingwa wa India. Yeye itakua yake macho tu na wala hamna atayempa chance za kudiscuss anything - ATAAMBIWA ubingwa wako huko huko Madongo kuinama, Delhi si Dar.
Hivi ndio tumekubali kua sisi ndio basi tena, hatuwezi na wagonjwa wetu watatibiwa INDIA. Is it sustainable au ni ule ule ubinafsi wetu, bado hata wanasiasa wetu wakongwe hawana hata aibu ya kuendelea pima afya zao nchi za nje wakati hospitali zetu hazina hata dawa. Kweli wajinga ndio waliwao.
Huyo AMO, au DR-PHYSICIAN? au DR bingwa asiende INDIA, TUNAWAHITAJI SANA HAPA, badala yake commercial attache hapo Ubalozini anaweza fanya hiyo kazi, maana ni sehemu ya biashara.
Huyo Shein kuamuru apelekwa mwambana wa afya India ni yale yale tuliyozoea ya CCM leadership.
 
Japo wizara hio imeoza katika maswala yote, na any breath of fresh air is welcome.
Kumpeleka specialist india ni kumpoteza, na kupoteza mtu muhimu sana katika wahudumiaji wa afya tanzania.
Mimi nadhani, kwa kusoma hapa tu, ni kuwa huyo AMO hafai na huyo Chale ni overqualified.
Atafutwe mtu mwingine.
Hasara za ubalozini tumezizoea sana tu, hakuna neno. Naonea huruma familia ambayo ilishajitune kabla ya signature zote kukamilika.
Ila namfurahia Katibu mkuu huyu mpya, hii wizara ina Ma MD wengi, na wanatabia ya kujiona wasomi, na hawagusiki, they have forgotten the main objective ya masomo yao, yani kuzingatia afya ya watanzania wengi, hasa wa kipato cha chini. Nao wanadai mishahara midogo kama kawaida.
Wengi wa professionals ni myopic in their fields, kwa hiyo kama ni kazi inayohitaji communication skills, managerial skills inabidi watrain mtu ambaye anahang tu hana proffession tayari ambayo tumeishailipia kwa majasho yetu.
Mimi binafsi naona wizara zote zinahitaji decision makers ambao sio waoga wa watu, sio waoga kufanya big changes, na sio waoga kulogwa au kufukuzwa kazi na mkuu wa nchi.
Wanaojua management ya watu as a human resource ambayo kiukweli ndio capital kubwa sana wizara ya afya, inavyokuwa mismanaged, chaos ndio kama hivyo tena.
 
mama blandina nyoni ni mchapa kazi wa kweli ....tunatambua anapigwa vita wizara ya afya kwa sababu wanaona anaingilia ulaji wa wao...wengi pale wanapenda safari ..na posho zisizo na kichwa wala miguu...

pale wizarani kumekubuhu kwa ulaji...na hawapendi msimamizi wa karibu......ndio maana hapo nyuma kwa kigezo cha utaalamu madaktari hao hao wamekuwa wakinunua vipimo feki vya ukimwi ,dawa nk...kwa kigezo cha utaalamu,wakurugenzi wengi pale ni kikwazo na wamekaa sana hilo si siri......huyu kijana pia amejipachika kwenda india ili akapate commissions kwa kuongeza bei kwa waginjwa wanaopelekwa kutibiwa ......kama ameshatiliwa shaka ..ni wazi hasara ya pango la dola 25,000 si hasara ukilinganisha ...na commission ya dola 1,500 ambayo huyu kijana angetengeneza kwa kila ,mgonjwa anayepelekwa india.....na mjuwe huu ni mtandao ambao kuna wakurugenzi pale wantaka aende mtu wao ili ...commissions za wagonjwa zikitoka ...huyu aweze kuwawekea zao.....ni bora achukuliwe mtu mpya kabisa ....hata madaktari walio kigoma nao wanaweza kupewa kazi kama hizi ...sio wa mijini tu!!!

wizara ya afya ukiona panatulia ujuwe katibu mkuu anayekuwepo ameamua ku compromise ..au ameamua kuwaacha ma aluwatan wafanye watakavyo....kwani pia ukiwafuatilia sana .....wanaweza kusababisha mapungufu kiitaalamu ili katibu mkuu aonekane kazembea ....na ndicho wanachojiandaa kumfanyia mama nyoni!
 
candidate atakayefaa india lazima awe na degree yeyote ya pili ie MBA.,MPH...Etc ...sio surgeon ambao ndio tatizo kuu....degree ya pili ya utawala itamsaidia kuweza ku negotiate...vema na watoa huduma pale na degree yake ya udaktari itamsaidia kuchagua matibabu yanayofaa kwenye hosipitali inayofaa.....
 
AMO hawezi kuwa karibu sawa na MD labda yesu arudi. Usitake kumtetea kisa mlikuwa naye shule ya msingi.

Naweza kuunga mkono ulinganifu wa AMO na MD kwa mazingira yetu ya TZ, walichopishana ni vyeti tu. Nenda kwenye hospitali zetu, kama hawajakuambia kama wao ni AMO wala hutaweza kugundua kamwe. Hii ni kwa sababu, kiutendaji, AMO wanaachiwa kufanya kazi nyingi na hao ma-MD kuliko unavyoweza kufikiria. Pita kwenye hospitali za wilaya, huko ndio kabisa, hao ma-MD wala hawapo, ni AMO tu wanashikilia ukanda..
 
Namuunga mkono 100% Mama Nyoni manake mtu kama ni AMO sidhani kama is competent enough 4 the job ambapo kuna wagonjwa kama wa moyo wanaopelekwa india wanaoihitaji good briefing kwa maprof wa upasuaji and this need at least a postgraduate someone! Tanzania tuache mambo ya kupeana post bila ujuzi unaotakiwa kwenye kazi( competence), na mfano mwingine umetokea juzi hapa Midrand South africa manake Mama yetu Mongella wabunge wa AU wamemshambulia kwa incompetence na wanataka ajiuzulu na wachague upya!
 
Hii habari imekaa kimajungu sana. Mwanahalisi hawajatuambia sifa za huyo Sawe, kulinganisha na sifa zinazotakiwa kwa mtu kushika nafasi hiyo.

Maelezo ya mama Nyoni yanajieleza, mtu hakuwa na sifa. Sasa kung'ang'ania kuwa midhali pango limeshalipwa basi ndio lizuie kiongozi kurekebisha makosa!... Hivi tunataka viongozi wetu wasiwe na ujasiri wa kuchukua hatua kwa kuogopa kuandikwa magazetini?

Mwanahalisi can do better than that. So far mama Nyoni is right.

Kama Mama Nyini yuko right then Mkama deserve sticks and carrot principle to fall on him kwa gharama za uzembe wa kufanya maamuzi alizoitia serikali
 
Tafadhalini ndugu. Huyu mama Blandina Nyoni hana ufisadi wowote. Ninamshukuru sana kwanza kwa kuisaidia Wizara ya Mali asili kusafisha maana inanuka kwa ufisadi. Wengi walimchukia kwa sababu aliiingia anga zao za kufisadi na akabana kila njia za panya za ufisadi kule Mali asili mpaka wengine walitaka kuacha kazi!!!! Tena inasemekana mafisadi wa Utalii ndiyo walicheza sana hadi atolewe pale maana alishaanza mikakatiaya kuziba mianya yote maana tukianzia vitalu vya uwindaji, camping, etc huko ni Uozo mtupu. Kama kna mwenzetu ana ile adobe document ilikuwa ianelezea ufisadi Maliasili aiposti hapa ile tupate pa kuanzia.

Cha pili huyu mama alipelekwa Wizara ya Afya ili kinusuru. Kuna uchafu mwingi wa wizi wa madawa hewa kule MSD na mengine mengi. Watu hawafanya kazi zinazowapasa matokeo yake ni kukimbizana na projects tu. UKitaka hata docment kule Wizara ya afya ilikuwa ni lazima uteseke sana, ofisa mhusika hayupo anakimbizana na projects. Kazi pale ni za upendeleo sana wakati huo, kwani unakuta pengine kazi fulani inatakiwa ifanywe na idara fulani maana ina fall katika objectives na targets zao lakini unakuta inapigwa juu juu anapewa mwingine kwa kuwa tu ina pesa. Mama Nyoni naamini atakuwa ameshalifanyia kazi hili, ni kero sana.

Kwa mantiki hiyo, najua kuna watu wengi pale watakuwa hawamtaki huyu mama kwa maana anawazibia njia zao za kifisadi!!!! Kama Kikwete anataka ufanisi wa ile Wizara basi huyu mama ndiyo pake haswa!!! Big up Ms. Blandina Nyoni. You are tough, I beleive on you. Please, leta urgent reforms za utendaji na uwajibikaji Wizarani. Wengi tunakuaminia achana na wachache ambao sasa wangeukia media kutaka kukubomoa, thubutu.
 
Namuunga mkono 100% Mama Nyoni manake mtu kama ni AMO sidhani kama is competent enough 4 the job ambapo kuna wagonjwa kama wa moyo wanaopelekwa india wanaoihitaji good briefing kwa maprof wa upasuaji and this need at least a postgraduate someone! Tanzania tuache mambo ya kupeana post bila ujuzi unaotakiwa kwenye kazi( competence), na mfano mwingine umetokea juzi hapa Midrand South africa manake Mama yetu Mongella wabunge wa AU wamemshambulia kwa incompetence na wanataka ajiuzulu na wachague upya!


mmmmhhhh!!....kashfa bado zinaendelea tu!
 

...na mfano mwingine umetokea juzi hapa Midrand South africa manake Mama yetu Mongella wabunge wa AU wamemshambulia kwa incompetence na wanataka ajiuzulu na wachague upya
!

E bana eeeh, yule Mama wameshamshtukia huko? I knew that lady is in over her head.
 
Hii habari imekaa kimajungu sana. Mwanahalisi hawajatuambia sifa za huyo Sawe, kulinganisha na sifa zinazotakiwa kwa mtu kushika nafasi hiyo.

Maelezo ya mama Nyoni yanajieleza, mtu hakuwa na sifa. Sasa kung'ang'ania kuwa midhali pango limeshalipwa basi ndio lizuie kiongozi kurekebisha makosa!... Hivi tunataka viongozi wetu wasiwe na ujasiri wa kuchukua hatua kwa kuogopa kuandikwa magazetini?

Mwanahalisi can do better than that. So far mama Nyoni is right.

Hapa kuna vitu haviko wazi kwani haijaelezwa criteria zilizotumika kuwachagua na pia criteria zipi ziko mezani. Hivyo lazima hivyo viwe wazi.

Mwanahalisi wametoa taarifa hivyo kwa upande wao wameshangaa kuwa mtu ameteuliwa miezi nane baadaye ndiyo unafuta hiyo appointment yake huoni kuwa huo ni uzembe? Hivyo huyu mama laitakiwa afanye maamuzi haraka kama ni kweli ana zifa hizo anazopewa.

Mwanahalisi walifanya maojiano na wote kila mtu ameeleza japo Mkama hakujibu vizuri labda kwa sababu ya maamuzi ya huyo mama haya kumfurahisha lakini huyo mama naye alisema sawe hana sifa hakuingia ndani. Hivyo ilikuwa ngumu kwa mwanahalisi kupata vigezo vilivyotumika.

Imekuwa vizuri haabari imetoka labda next time maamuzi hayatachukua muda mrefu kama hivi.
 
1. Tafadhalini ndugu. Huyu mama Blandina Nyoni hana ufisadi wowote. Ninamshukuru sana kwanza kwa kuisaidia Wizara ya Mali asili kusafisha maana inanuka kwa ufisadi.

2. Wengi walimchukia kwa sababu aliiingia anga zao za kufisadi na akabana kila njia za panya za ufisadi kule Mali asili mpaka wengine walitaka kuacha kazi!!!!

3. Tena inasemekana mafisadi wa Utalii ndiyo walicheza sana hadi atolewe pale maana alishaanza mikakatiaya kuziba mianya yote maana tukianzia vitalu vya uwindaji, camping, etc huko ni Uozo mtupu. Kama kna mwenzetu ana ile adobe document ilikuwa ianelezea ufisadi Maliasili aiposti hapa ile tupate pa kuanzia.

4. Cha pili huyu mama alipelekwa Wizara ya Afya ili kinusuru. Kuna uchafu mwingi wa wizi wa madawa hewa kule MSD na mengine mengi. Watu hawafanya kazi zinazowapasa matokeo yake ni kukimbizana na projects tu. UKitaka hata docment kule Wizara ya afya ilikuwa ni lazima uteseke sana, ofisa mhusika hayupo anakimbizana na projects.

5. Kazi pale ni za upendeleo sana wakati huo, kwani unakuta pengine kazi fulani inatakiwa ifanywe na idara fulani maana ina fall katika objectives na targets zao lakini unakuta inapigwa juu juu anapewa mwingine kwa kuwa tu ina pesa. Mama Nyoni naamini atakuwa ameshalifanyia kazi hili, ni kero sana.

6. Kwa mantiki hiyo, najua kuna watu wengi pale watakuwa hawamtaki huyu mama kwa maana anawazibia njia zao za kifisadi!!!! Kama Kikwete anataka ufanisi wa ile Wizara basi huyu mama ndiyo pake haswa!!! Big up Ms. Blandina Nyoni. You are tough, I beleive on you. Please, leta urgent reforms za utendaji na uwajibikaji Wizarani. Wengi tunakuaminia achana na wachache ambao sasa wangeukia media kutaka kukubomoa, thubutu.

- Saafi sana Mkulu Maane, yaani huyu Mama Nyoni ni for president tu kuna huyu na Mapunjo kule Biashara, moto wa kuotea mbali sana.

Respect.

FMES!
 
Inawezekana kabisa huyo Dr. alimsaidia bwana kubenea kwenda Indi akipindi kile alipopatwa na maswaiba yale....

sasa yatamtokea Puani...JF ni mdomo mkubwa zaidi ya yote
 
Mama Nyoni gave us Epicor to run government accounting, a software package better suited for manufacturing and distribution industries. Its no wonder the current CAG Ludovick Utouh is uncovering gross misappropriations in government accounting.

Mama Nyoni and local vendor Softech have reaped a lot of money from this deal - 2006-07 alone they have made up to USD 8-9 million in just training alone. She personally recommended Epicor and the local vendor Softech to the Malawi, Lesotho and Gambia governments, using government letterhead!

Visit many of the governmental parastatals in Dar and many say it is a hassle to work with this software, upgrades and training are expensive, customer service very poor, and if you get it, very expensive. She is gone now from Hazina where she ruled with an iron fist - and there began a mini stampede away from Epicor.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom