Katibu mkuu wa CCM yuko wapi na anafanya nini?

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,326
5,266
Wakuu salaam,nataka nijue kinachoendelea huko chamani kwani naona kama nape ndio amekuwa msemaji,mfanya mikutano na kila kitu,nataka nijue alipo katibu wetu mkuu, jina nimesahau
 
Umetumwa na Nape kupima upepo kama katibu mkuu anakubalika. Wajanja tumeishakushtukia.
Mzee wa watu anakula pensheni muanze kumrudisha majukwaani kumwaga pumba za makomandoo wa Igunga?? Muacheni apumzike nyie endeleeni na propaganda zenu uchwara. Naskia Said Mwema ndio anaandaliwa kumrithi Mukama!!
 
Huyu Mzee ana busara sana,
hawezi kuharibu credibility yake kwa jamii kwa kusemasema ovyo ama kuupamba mzoga wa fisi (ccm)

kama hawamtaki wamtimue, ama vipi waendelee kumlipa kwa kukaa kimya. very interesting movie.
 
Yuko kwenye forced exile, wakuu wake hakupendezwa na tabia yake ya jazba na shooting first then take aim later!!
 
Yupo na Dk.Kafumu wameamua wajitulize wawaachie wenyewe na varangati zao. Hawataki kuingia kwenye historia ya kukizamisha chama chetu.
 
Huyu Mzee ana busara sana,
hawezi kuharibu credibility yake kwa jamii kwa kusemasema ovyo ama kuupamba mzoga wa fisi (ccm)

kama hawamtaki wamtimue, ama vipi waendelee kumlipa kwa kukaa kimya. very interesting movie.

mbona ameshaharisha mara nyingi tu
 
Mukama alilazimishwa tu kuingia kwenye ulingo wa siasa lakini jamaa ni kichwa sana. Atakuwa amechekecha na kuona kuwa ni bora akae kimya badala ya kubwabwaja majukwaani kama akina nepi na miguu.
 
Wakuu salaam,nataka nijue kinachoendelea huko chamani kwani naona kama nape ndio amekuwa msemaji,mfanya mikutano na kila kitu,nataka nijue alipo katibu wetu mkuu, jina nimesahau
Wengi tulikuwa na mategemeo chanya na Wilson Mukama, lakini kwa sasa anapwaya vibaya, hasikiki wala kukipigia chapuo chama kama inavyohitajika.
Kijana Nape anakwenda vizuri.
 
Huyu Mzee ana busara sana,
hawezi kuharibu credibility yake kwa jamii kwa kusemasema ovyo ama kuupamba mzoga wa fisi (ccm)

kama hawamtaki wamtimue, ama vipi waendelee kumlipa kwa kukaa kimya. very interesting movie.
anaheshima gani, huyu si aliwai kuropoka igunga kuwa Chadema wameingiza makomandoo toka libya au siye jamani.?
 
Mukama alilazimishwa tu kuingia kwenye ulingo wa siasa lakini jamaa ni kichwa sana. Atakuwa amechekecha na kuona kuwa ni bora akae kimya badala ya kubwabwaja majukwaani kama akina nepi na miguu.
.
Nasikia aliandika barua ya kujiuzulu ... amekataliwa ... na yeye kasusa (yupo kwenye mgomo baridi) ... hana moyo tena wa kufanya kazi yake
.
 
Umetumwa na Nape kupima upepo kama katibu mkuu anakubalika. Wajanja tumeishakushtukia.
Mzee wa watu anakula pensheni muanze kumrudisha majukwaani kumwaga pumba za makomandoo wa Igunga?? Muacheni apumzike nyie endeleeni na propaganda zenu uchwara. Naskia Said Mwema ndio anaandaliwa kumrithi Mukama!!
chemba ndio anataka kuwania hiyo nafasi
 
Inasemekana baada ya dhana aliyoiasisi ya kuvua gamba,dhana ambayo kijana Nape aliibeba na kutembea akiimba kila pembe kushindikana,Mzee Mkama aliomba kujiuzulu na hii ni kutokana na ugumu na uzito wa magamba yenyewe ndani ya chama. Ikumbukwe magamba hayo wanayajua vyema ndani ya chama na yenyewe yaliamua kujipanga vyema na kujizatiti hadi ndani ya bunge (kwenye kamati za bunge) na kuzidi kukitia chama hofu endapo wangeyavua. Mkama walimkatalia kujiuzulu kwa kuangalia upepo wa kisiasa unavyovuma ukikinzana nao,na kuona wakimkubalia basi upepo utawageukia zaidi na kuwa kimbunga. Wakamwambia asubiri uchaguzi wa chama ajitoe asigombee ili kuficha siri ya kushindwa kwa dhana ya kujivua gamba. Mkama nae akachagua kutokuwa tena mzungumzaji na mtendaji wa chama na ndio maana amekuwa kimya kama mnavyoona. Nape nae kaacha kuzungumzia magamba anachofanya ni kwenda na kile kijacho mbele yake,bila kuwa kimkakati. Mtayaona kwenye uchaguzi mkuu wa CCM.
 
anaheshima gani, huyu si aliwai kuropoka igunga kuwa Chadema wameingiza makomandoo toka libya au siye jamani.?

"umebugi step"
pita katikati ya hiyo mistari kwa utaratiiiiiibu utanielewa.
 
mbona ameshaharisha mara nyingi tu
Bajabiri usikonde, mropoko ulishatokea ni kweli, lakini je hukuona huko faida ya kuropoka kwake? Uharo hatari ni wa mgonjwa wa kipindupindu (nape)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom