Katibu Mkuu wa CCM, Kinana - LIVE on Azam TV na Tido Mhando

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,311
Anaongelea uteuzi uliopita wa urais ndani ya ccm.

Anasema viongozi kuondoka ccm hawajaanza leo toka mwaka 1995, 2000,2005,2010 na sasa.

Anahoji kama Lowassa anasema hakuna demokrasia ndani ya CCM je utaratibu uliotumika kumteua ndani ya Chadema ni wa kidemokrasia?

Anasema Lowassa sio wa kwanza kujaza watu kwenye mikutano anakumbusha Mrema 95,Slaa na hata Magufuli anajaza watu vilevile.

Anasisitiza utaratibu uliotumika miaka yote kumpata mgombea ndio huo huo umetumika na mwaka huu.!

Kuhusu rushwa kwenye chaguzi anakiri lipo kila ngazi na kila chama, anasema ndio maana unasikia kuna watu wameenda kununua vyama.
Anasema sio kila kiongozi anatoa rushwa anasema anamfano wa majimbo ambayo hawakutoa rushwa.

Kuhusu kukata wagombea anasema vigezo vingi vinatumika ikiwemo swala la rushwa , kukubalika kwenye jamii na mambo mengine.

Kuhusu Ilani anasema Ilani ya itakayozinduliwa leo itakua na ahadi nyingi zaidi kuliko zilizopita.

Kuhusu waliohama na kama wataisema ccm na ccm itasema yao, anasema swala la kuhama lisikuzwe sana ni jambo la kawaida.

Anasema viongozi wastaafu hawatamsaidia Magufuli kwenye kampeni labda pale tu itakapohitajika.

Kuhusu goli la mkono, anasema Nape alitafusiriwa vibaya na watu wenye malengo yao. Anasema tume ya uchaguzi ipo na taasisi mbalimbali zinazoshiriki kufanikisha uchaguzi.

Anasema uchaguzi ni mahesabu, na mwaka huu ccm kura zitaongezeka na kuna baadhi ya majimbo ya upinzani yatachukuliwa japo hata wapinzani wanaweza kuchukua ya ccm.

Anasema wabunge wa upinzani mwaka 95 walikuwa wengi 2000 na 2010 wakapungua 2015 ndio wakaongezeka hivyo hata mwaka huu wanaweza kupungua.

Anataja wabunge wa ccm wanaojenga hoja ndani ya bunge Lugola, Mpina,Filikunjombe, Lugola nk.

Anasema hakuna uchaguzi mdogo wala mkubwa , anasema hawamdharau mpinzani wao ila wamejiandaa vizuri.

Mkuu naomba update maana sioni azam 2

Mkuu apo alipomuuliza Lowasa kama ndani ya CCM hakuna demokrasia je yeye alivyopitishwa na CHADEMA ndio Demokrasia?

pana hoja hapa tena kubwa sana mkuu
 
Anadai hata 95 kuna watu waliondoka. Kwa hiyo hawatishiki
 
Anaongelea uteuzi uliopita wa urais ndani ya ccm.

Anasema viongozi kuondoka ccm hawajaanza leo toka mwaka 1995, 2000,2005,2010 na sasa.

Anahoji kama Lowassa anasema hakuna demokrasia ndani ya CCM je utaratibu uliotumika kumteua ndani ya Chadema ni wa kidemokrasia?

hyo Ni mnafiki na mzadiki. Atueleze kwanza Ni kwanini vyombo vyake vya usafiri vinatumika kubeba meno ya tembo ikimaanisha Ni muhusika wa kumaliza wanyama pori wetu.
 
Poor PR hao sisiemu, ni nani atamsikia? kwa nini kaenda Azam Tv badala ya kwenda chanel ambayo ni FTA??? maono mabovu timu ya PR!
 
hivi kwa nini ni wanaume tu ndo makada pekee wa ccm waliohama chama ca mapinduzi na kuingia ukawa je wanawake hawataki mabadiliko tena hawa ndo wangekuwa wa kwanza kwani ccm imewatenda vibaya sana ukiangalia leo wakina mama ndo wanapata tabu wakati wa kujifungua wanajifungulia chini wao ndo kilia siku wanakimbizana na mgambo jiji bt cjaona mmama yeyote akihama chama zaidi ya wakina baba
 
hyo Ni mnafiki na mzadiki. Atueleze kwanza Ni kwanini vyombo vyake vya usafiri vinatumika kubeba meno ya tembo ikimaanisha Ni muhusika wa kumaliza wanyama pori wetu.

Hawezi kujibu Swali asiloulizwa, Tido akiuliza atajibu bila shaka. Anahoji huyo alietoka Ccm kwa kuwa tu kanuni hazikufuatwa huko alipoteuliwa kanuni zilifuatwa? anasema Mapambano yanaanza watu washuhudie mpambano
 
Huyu Jangiri anajikanyakaga eti CCM imeleta maendeleo vituo vya TV kama AZAM ,dahhhh kweli wameishiwa sera,

TIDO kamtit jangira chama kile kile ilani zile zile
 
hivi kwa nini ni wanaume tu ndo makada pekee wa ccm waliohama chama ca mapinduzi na kuingia ukawa je wanawake hawataki mabadiliko tena hawa ndo wangekuwa wa kwanza kwani ccm imewatenda vibaya sana ukiangalia leo wakina mama ndo wanapata tabu wakati wa kujifungua wanajifungulia chini wao ndo kilia siku wanakimbizana na mgambo jiji bt cjaona mmama yeyote akihama chama zaidi ya wakina baba

Esta bulaya ni mwanaume?
 
Back
Top Bottom