Katibu mkuu nishati na madini kikaangoni kesho

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
kama busara haitatumika, kesho katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini huenda akapoteza kazi, hii itatokea baada ya bajeti ya wizara kusomwa bungeni kesho ijumaa. kuna jitihada zinafanyika kuwaomba wabunge hasa ole sendekea na wajumbe wengine wa kamati ya nishati wafunike kombe ili bajeti ipite ila wamekuwa ngangari wakisisitiza kuwa bwana maswi alikiuka sheria ya manunuzi hivyo lazima awajibike katika sakata la mafuta ya IPTL.

kwa mtizamo wangu, WIZARA YA NISHATI ni ngumu sana kuiendesha, ni pango na mnyororo wa wizi na ufisadi mkubwa, kuna watu wamefaidika, wanafaidika na kuna wanaotaka kufaidika na matatizo ya umeme hali ni tete ndugu zangu, na kwa taarifa yangu ya kiintelejensia ni kuwa immidiately baada ya bunge, mgao mkubwa wa umeme unakuja mtajuta wabongo , naionea huruma Nchi hiii.
 
Napenda kuwaambia watanzania kuwa tuangalie sana jinsi tunavyosalitiwa na baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamekuwa wakifanaya unafiki wa kujifanya wanapenda nchi yao na watu wao.
Deo mwanyika ni makamu wa rais kampuni ya barik gold mine na yupo kwenye mchakato wa kutafuta ubunge njombe kusini jimbo la spika makinda.
Leo anatoa zawadi za mipira kwa vijana njombe akijifanya anapenda sana vijana,lakini tujiulize kwa nini leo na sio jana???/hadi awe na nia ya kutaka ubunge ndio aje?na wapi anakozipata hizo pesa za kuhonga watu apate ubungeeeeeeeeee
njombe kumbukeni munaweza kutoa afadhali na kuweka potelea mbali.
 
zile taa zetu za chemli ambazo hatujazitumia kwa muda mrefu itatubidi tuzifute vumbi tayari kujiandaa na mgao
 
Ole sendeka yupi? Huyu mchumia tumbo? Huwa anaongea kwa jazba mwishowe anadanganyika kipuuzi labda useme mtu mwingine, Sendeka,kilango,manyanya,mwak,seleli wote bure tu ni sawa na togwa
 
hii wizara inakua nzuri kama wote wakielewana kwenye jinsi ya kula..ugomvi unakuja pale bodi inataka kupiga dili na watu ambao wizara haiwataki or vice versa..sa hapo ndo chokochoko inaanza..kwanini wizara na bodi wasikae pamoja na kamati ya nishati na madini wajadili kwa pamoja jinsi ya kutunyonya na kuimaliza kabisa tanesco bila kutokea ugomvi?
 
Hawa wabunge nao kila katibu mkuu hawamtaki??????????ni kwamba hawa makatibu wana gundu au wizara ndo ina gundu aisee
 
Nasikia baada ya bajeti kupita bei ya mishumaa itapanda, sababu ni mgao mkali unakuja...
 
JK akimuondoa Maswi kwenye wizara hiyo ndo kashemsha kabisaaa, jamaa anajitahidi kudhibiti mianya ya ufisadi ya vigogo tanesco
 
Napenda kuwaambia watanzania kuwa tuangalie sana jinsi tunavyosalitiwa na baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamekuwa wakifanaya unafiki wa kujifanya wanapenda nchi yao na watu wao.
Deo mwanyika ni makamu wa rais kampuni ya barik gold mine na yupo kwenye mchakato wa kutafuta ubunge njombe kusini jimbo la spika makinda.
Leo anatoa zawadi za mipira kwa vijana njombe akijifanya anapenda sana vijana,lakini tujiulize kwa nini leo na sio jana???/hadi awe na nia ya kutaka ubunge ndio aje?na wapi anakozipata hizo pesa za kuhonga watu apate ubungeeeeeeeeee
njombe kumbukeni munaweza kutoa afadhali na kuweka potelea mbali.

Afadhali yeye amekumbuka leo kutoa hiyo misaada, mbona wewe haukumbuki? Utampangia vipi kwamba angetoa jana? Una hakika alikuwa nazo? Unauliza amepata wapi pesa wakati tayari unatuambia anafanya kazi Barrick!! Unadhani bi Kiroboto ana hati miliki ya hilo jimbo? Au wewe ndio yeye? Au msemaji wake? Tunahitaji mabadiliko kila pande huyo bi Kiroboto wako amesha overstay
 
Ni Mbunge gani atamweka kikaangoni huyo katibu? Sijaona mbunge mzalendo katika bunge lile.
 
hii wizara inakua nzuri kama wote wakielewana kwenye jinsi ya kula..ugomvi unakuja pale bodi inataka kupiga dili na watu ambao wizara haiwataki or vice versa..sa hapo ndo chokochoko inaanza..kwanini wizara na bodi wasikae pamoja na kamati ya nishati na madini wajadili kwa pamoja jinsi ya kutunyonya na kuimaliza kabisa tanesco bila kutokea ugomvi?

Mh kweli watu wamechoka!
 
Ni Mbunge gani atamweka kikaangoni huyo katibu? Sijaona mbunge mzalendo katika bunge lile.

Sio mbunge tu, bali hakuna mtu yeyote aliye/asiye serikalini mwenye uzalendo, wote ni katika kujitafutia mkate wao wa kila siku pamoja na wajukuu zake.
Yesu alikuja ili tuwe na uzima, kisha tuwe nao tele.
 
Afadhali yeye amekumbuka leo kutoa hiyo misaada, mbona wewe haukumbuki? Utampangia vipi kwamba angetoa jana? Una hakika alikuwa nazo? Unauliza amepata wapi pesa wakati tayari unatuambia anafanya kazi Barrick!! Unadhani bi Kiroboto ana hati miliki ya hilo jimbo? Au wewe ndio yeye? Au msemaji wake? Tunahitaji mabadiliko kila pande huyo bi Kiroboto wako amesha overstay

Mkuu ukumbuke vyote hivyo anavyojidai anawapatia sasa akiingia madarakani atahakikisha amevirudisha na ziada zake then ndo aanze kula kwa kipimo na siyo aanze kuwatumikia
 
Sasa huku ni kukomba mboga. Hili shirika mbona kama ni ndoto ya mfalme mtafsiri hapatikani? Yani mpaka aje Yusufu wakubwa?
 
JK akimuondoa Maswi kwenye wizara hiyo ndo kashemsha kabisaaa, jamaa anajitahidi kudhibiti mianya ya ufisadi ya vigogo tanesco

Ni kweli mkuu. Halafu ikumbukwe kuwa hiyo kampuni iliyopewa tenda ya kusambaza mafuta ya PUMA, serikali inamiliki 51% ya share. Kwa upande wangu mimi naona ni uzalendo kwa Maswi kuipa kampuni hiyo tenda badala ya kuwapa hao matapeli wengine. Kikwete anatakiwa awe bold kwa hili. Ana watu wenye nina njema na TZ hapo wizarani kwa sasa i.e katibu mkuu na waziri wake ila kuna watu wamezibiwa ulaji wanapigana usiku na mchana ili hawa watu watolewe hapo. Too bad!
 
Napenda kuwaambia watanzania kuwa tuangalie sana jinsi tunavyosalitiwa na baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamekuwa wakifanaya unafiki wa kujifanya wanapenda nchi yao na watu wao.
Deo mwanyika ni makamu wa rais kampuni ya barik gold mine na yupo kwenye mchakato wa kutafuta ubunge njombe kusini jimbo la spika makinda.
Leo anatoa zawadi za mipira kwa vijana njombe akijifanya anapenda sana vijana,lakini tujiulize kwa nini leo na sio jana???/hadi awe na nia ya kutaka ubunge ndio aje?na wapi anakozipata hizo pesa za kuhonga watu apate ubungeeeeeeeeee
njombe kumbukeni munaweza kutoa afadhali na kuweka potelea mbali.

mkuu why Deo Mwanyika ni tajiri na pesa yake ni halali,kama nikuhoji basi hoja timing ya misaada yake lakini siyo utajiri wake.

Kama huna data zozote za ubadhirifu dhidi yake basi hupaswi kuhisi kwamba ni mbadhirifu.
 
Hatakiwi kuchomoka kesho. Mwenzake katolewa kafara....................................... Inatakiwa afuatie!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom