Katibu mkuu CHADEMA (Dr. Slaa) atoa tamko

Katibu wa chama cha Demokrasia Chaema bwana Willbrodi Slaa amesema wabunge wa Chadema hawataingia ktk vikao vya Bunge Kama Serikali haitomwachia mwenyekiti wa Chadema bwana Freeman Aikaeli Mbowe bila masharti yeyote magumu

Sourse ITV habari 8:00pm

sisi mbunge wetu hata kama asingepitia chadema tungemchagua, na kule bungeni hawakilishi chama bali anawakilisha wananchi kwahiyo sisi wananchi tuliomchagua ndio tunaweza kumwambia mbunge wetu aende au asiende bungeni na siyo Slaa. Huyu mzee vipi.
 
Mbowe kuachiwa ataachiwa tu tena kwa dhamana hiyo jumatatu,

Siungi mkono maandamano, na wabunge mnahitajika sana bungeni hii susia susia itatucost magamba yatapitisha bajeti za ajabu ohooo!
wewe mwenyewe ckuelewi kabisa,unajua nafasi ya Mbowe bungeni???? Bunge linaweza fanyika bila waziri mkuu???? changanya na zako sasa utaelewa kwa nini wasiende
 
Dr Peter Slaa, usije ukadhubutu ku boycot bunge, utakuwa umewapa zawadi kama ile ya Maalim kutuitambua serikali ya Amani, mpaka mwaka wa mwisho wa amani maalim alivutwa pembeni, akapewa mfupa, sasa mambo poa znz, lakini kwa miaka 9 amani alifanya alichokitaka.
Dr kama vipi wewe ni binadamu, ombeni msaada kwetu wananchi, hebu lieni kuwa mnashindwa kutusaidia kwa kuonewa ovyo na CCM, sisi tutajua la kufanya, jua jua jeshi la watu milioni 50 linalodhulumiwa na CCM & Co, sema nyinyi wakombozi hamtujulishi mkiumizwa, tutatumia kila njia ya kuhakikisha TUKIPIGWA KOFI MOJA, TUNARUDISHA KOFI MBILI ZA HATARI alisema MALCOM X
God Bless Baba Slaa, God Bless Baba Lowassa, God Bless Chadema, God Bless The City of Arusha!!!

Simbaa:Kiongozi bila kujali umejoin lini humu kulingana na status yako, aise nimekukubali mbaya mno! Nimekupa salute aise, umenena vyema kabisa, umeongea mambo ya msingi. Hoja yako naiunga mno kwa 100%.
Karibu sana JF, tunahitaji mawazo na fikra za namna hii Comrade.
 
sisi mbunge wetu hata kama asingepitia chadema tungemchagua, na kule bungeni hawakilishi chama bali anawakilisha wananchi kwahiyo sisi wananchi tuliomchagua ndio tunaweza kumwambia mbunge wetu aende au asiende bungeni na siyo Slaa. Huyu mzee vipi.
Think big
 
Simbaa:Kiongozi bila kujali umejoin lini humu kulingana na status yako, aise nimekukubali mbaya mno! Nimekupa salute aise, umenena vyema kabisa, umeongea mambo ya msingi. Hoja yako naiunga mno kwa 100%.
Karibu sana JF, tunahitaji mawazo na fikra za namna hii Comrade.

Mkono wa kulia unaunga mkono wa kushoto kwenye mwili ule ule na magamba yale yale
 
dr tusikubali kuingizwa mkenge na magamba, wao wanajua bajeti hii ni bomu na pingamizi kubwa litatoka CDM, ziara za mikoani mojawapo ya ajenda kuu ilikuwa ni kuipinga bajeti hii kama itaonesha dalili za kumwelemea mwananchi wa chini sasa tusipoingia bungeni na bajeti ikapitishwa na magamba & co kama ilivyo mtakuwa mmewasaidia nini wananchi.

KWA MARA YA KWANZA NAPINGANA VIKALI NA KAULI YA DR

Chadema wako wangapi bungeni na wanamagamba wanapitishaga hata hoja za kijinga eti wanawakomoa chadema. Kamawe hujui juzi tu mwenyekiti wa kamatio ya huduma za jamii amalishwa limbwata na kupewa bahasha na kushinikiza wabunge wapitishe makadirio ya bajeti ya wizara ya afya wakati makabrasha hawakupewa kwa wakati kama kanuni zinavyotaka. Wabunge wamelalamika na hata wa CCM akiwemo Dr Kigwangalla ambaye wazi wazi kasema chama chake cha magamba kimetumia ubabe kuwalazimisha wabunge kupitisha bajeti. Ni heri wasiingie bungeni kwani kama mkuu wa kutoa uelekeo wa nchi anafanyiwa ujinga nyie mnaingia kufanya nn? tena inasemekana wanataka kumpoison. walishindwa kwa kubenea sijui huyu..tunakoelekea kubaya
 
sisi mbunge wetu hata kama asingepitia chadema tungemchagua, na kule bungeni hawakilishi chama bali anawakilisha wananchi kwahiyo sisi wananchi tuliomchagua ndio tunaweza kumwambia mbunge wetu aende au asiende bungeni na siyo Slaa. Huyu mzee vipi.

Heshima mkuu, ila hapa umezungumza upuuzi. Una uwezo wa kumwambia mbunge wako kitu kulingana na chama hapo umedanganya. Halafu Dr. Slaa keshasema subiri kama wabunge wa CDM watakwenda halafu tuendelee na mjadala. Hapo ndipo utamuuliza Slaa na mbunge wako.
 
Cha muhimu ni kile tutakachofanya kesho hapa A-town wakati wa kumsindikiza jemadari wetu mahakamani.
 
Hivi kwani bunge ni la serikali au la wananchi? wasipoingia kuna effect gani? sio wao watapoteza nafasi zao za kutetea majimbo? mbona watafurahi bajeti kupitishwa bila kupingwa.
 
Hivi jamani, hizi taratibu zakushikana hasa weekend ndo utawala bora au kuna kun watu wanafanya kazi kwa maagizo from the top. you just imagine mwenyekiti wa chama makini anafanyiwa hivi..... what about mimi "rumpeni?" this is something to rethink.Hata hivyo kwann itokee wakati huu karibia na bunge la bajeti? why two weeks or three before bunge? HAPA KUNA NN? LETS PLAY FOR MBOWE.
 
Arusha kesho hapatatosha leo yenyewe ilikua ni patashika vijana wako tayari kwalolote lile wamechoka kuburuzwa
 
Mahakama yang'ang'ania Freeman Mbowe akamatwe



*Hati ya kukamatwa Slaa, Ndesamburo yafutwa

Na Said Njuki, Arusha

Majira

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imeagiza tena Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Bw. Freeman Mbowe baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili.

Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria katika mahakamani hapo Mei 27 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Charles Magesa alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na polisi.

Mahakama hiyo awali, iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini) wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayowakabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali Januari 5 mwaka huu.

Washtakiwa wengine ambao mahakama ilitoa hati ya kukamatwa ambao hata hivyo walijisalimisha mahakamani siku mbili baadaye ni pamoja na mchumba wa Dkt. Slaa, Bi. Josephine
Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.


Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani, hata Mawakili wao, Bw. Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini washtakiwa Bw. Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Bw. Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.

Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Bw. Nai Steven, Bw. Mathias Valerian, Bw. John Materu, Bw. Daniel Titus, Bw. Juma Samuel, Bw. Walter Mushi, Bw. Peter Marua na Bw. Erick Makona.

Hakumu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo hadi jana wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo.

“Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani,” alisema.

Bw. Ndesamburu alinusurika kwenye hukumu hiyo baada ya Mdhamini wake, Bw. Reuben Ngowi kuibuka mahakamani hapo na kutoa udhuru uliomkuta mshtakiwa huyo pamoja na yeye mwenyewe, ambapo Hakimu Magesa alikubaliana naye na kufuta amri hiyo, hivyo kuachiwa huru.

Katika hukumu dhidi ya washitakiwa wengine waliojisalimisha pamoja na wadhamini wao, walipewa onyo kali na kutakiwa kutorudia kosa hilo kwani kufanya hivyo ni kukiuka maagizo halali ya mahakama.

Alisema amepitia hoja za wakili wa upande wa utetezi, na kwa kuzingatia sababu zilizotolewa mahakamani, aliamua kufuta amri hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24, mwaka huu.
 
Bora CDM wasiingie bunge la bajeti ii iwe rahisi katika mikutano yao wapate agenda ya kusema. Nafikiri hiyo bajet itakuwa msumari kwa maeneo mengi.
 
nimechelewa kidogo news ya ITV sikuipata hii ya Rais wetu, nimekuta NAPE anasema gamba wamejivua sasa ni CCM Mpya, hivi huyu jamaa ana aklli kweli?

Anafikiri kwa kutumia tumbo siyo akili?
 
Back
Top Bottom