Katibu mkuu CHADEMA (Dr. Slaa) atoa tamko

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,558
7,156
Katibu wa chama cha Demokrasia Chaema bwana Willbrodi Slaa amesema wabunge wa Chadema hawataingia ktk vikao vya Bunge Kama Serikali haitomwachia mwenyekiti wa Chadema bwana Freeman Aikaeli Mbowe bila masharti yeyote magumu

Sourse ITV habari 8:00pm
 
Jamani hii imekaaje kwa wanachadema wenzangu?
 
Safi sana, mheshimiwa dr Slaa huo ndio ukombozi, kama vipi wajiue kabisa ili wananchi wapate uwakilishi mzuri.
 
Katibu wa chama cha Demokrasia Chaema bwana Willbrodi Slaa amesema wabunge wa Chadema hawataingia ktk vikao vya Bunge Kama Serikali haitomwachia mwenyekiti wa Chadema bwana Freeman Aikaeli Mbowe bila masharti yeyote magumu

Sourse ITV habari 8:00pm

nasikia kasema mengi, si hayo tu uliyoandika. Mwenye taarifa kamili atuwekee hapa. Alizungumza pia uhalali wa amri ya mahakama huku hakimu alishapata mawasiliano ya kutofika kwa Mbowe na pia kuwepo kwa shinikizo kutoka ngazi za juu za serikali katika suala hili.
 
mbowe ni kiongozi wa wabunge tumia mfano rahisi hapo kazini kiongozi wako kasulubiwa bila utaratibu wewe utaendelea na kazi huku unalalamika au utachukua hatua?
 
dr tusikubali kuingizwa mkenge na magamba, wao wanajua bajeti hii ni bomu na pingamizi kubwa litatoka CDM, ziara za mikoani mojawapo ya ajenda kuu ilikuwa ni kuipinga bajeti hii kama itaonesha dalili za kumwelemea mwananchi wa chini sasa tusipoingia bungeni na bajeti ikapitishwa na magamba & co kama ilivyo mtakuwa mmewasaidia nini wananchi.

KWA MARA YA KWANZA NAPINGANA VIKALI NA KAULI YA DR
 
nimechelewa kidogo news ya ITV sikuipata hii ya Rais wetu, nimekuta NAPE anasema gamba wamejivua sasa ni CCM Mpya, hivi huyu jamaa ana aklli kweli?
 
nimechelewa kidogo news ya ITV sikuipata hii ya Rais wetu, nimekuta NAPE anasema gamba wamejivua sasa ni CCM Mpya, hivi huyu jamaa ana aklli kweli?

Jamaa anajua kabisa wananchi walishakistukia vizuri chama cha magamba sema pesa walizokula kuja ktk mkutano watadaiwa na t-shirt,kanga na kofia za bure watazikosa.
 
Sijui rais kikwete anafikiria nini ktk hali kama hii. Kama anataka kuondoka madarakan ni bora aende kimya kimya,lakini ktk hali ya kuleta uhasama kati yetu itamletea matata makubwa sana.
 
dr tusikubali kuingizwa mkenge na magamba, wao wanajua bajeti hii ni bomu na pingamizi kubwa litatoka CDM, ziara za mikoani mojawapo ya ajenda kuu ilikuwa ni kuipinga bajeti hii kama itaonesha dalili za kumwelemea mwananchi wa chini sasa tusipoingia bungeni na bajeti ikapitishwa na magamba & co kama ilivyo mtakuwa mmewasaidia nini wananchi.

KWA MARA YA KWANZA NAPINGANA VIKALI NA KAULI YA DR

usiwe na wasiwasi juu yakupitisha bejeti kwafitna dr analijua, iungemkonocdm
 
Chama Cha Magamba baada ya kushindwa katika kampeni zao za "kujivua gamba" sasa wamekuja na kamata kamata ya Viongozi wa juu wa CHADEMA ili kuwatisha na kuwadhalilisha lakini wakati huo huo wameshindwa kabisa kuwakamata mafisadi wakubwa wanaoipeleka nchi mrama.

Inaelekea huu mkakati wa kuwadhalilisha Viongozi za juu umepata baraka za Viongozi wa juu wa chama cha magamba ndio maana bado wako kimya bila kutoa tamko lolote lile kuhusu kukamatwa kwa Mbowe. Inasikitisha sana kuona jinsi Mbowe anavyodhalilishwa na kumtisha kwa kosa ambalo si kubwa kiasi hicho ili tu kupumguza makali yake katika kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania katika nchi inayoongozwa na mafisadi.

Hii amani ya kizandiki tuliyonayo ikishapotea basi itakuwa vigumu mno kuirudisha na hakuna wa kulaumiwa ila Chama Cha Magamba. Yaliyotokea Misri, Syria, Tunisia ni ushahidi tosha wa jinsi amani ya nchi inavyoweza kupotea kirahisi na maafa makubwa kutokea na ni kazi kubwa sana kuirudisha amani hiyo.
 
dr tusikubali kuingizwa mkenge na magamba, wao wanajua bajeti hii ni bomu na pingamizi kubwa litatoka CDM, ziara za mikoani mojawapo ya ajenda kuu ilikuwa ni kuipinga bajeti hii kama itaonesha dalili za kumwelemea mwananchi wa chini sasa tusipoingia bungeni na bajeti ikapitishwa na magamba & co kama ilivyo mtakuwa mmewasaidia nini wananchi.

KWA MARA YA KWANZA NAPINGANA VIKALI NA KAULI YA DR

Upinge usipinge, CDM wawepo wasiwepo bajeti itapitishwa. Nakubaliana na Dr. na hapo itakuwa rahisi na tija kuwashitaki kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom