Katibu Mkuu BAVICHA amshindilia kaa la moto Mwigulu Nchemba na Nape

Mwigullu na Nape hivi sasa ndo threat kubwa kwa CDM nini? mbona watu wadogo sana hawa inakuaje wawe tishio kiasi hiki, hapo SANGARA hawajaunguruma. Hakika CDM ni dhaifu, kila siku Nchema, Nape. Siyo vipaumbele vya maendeleo.
Fanhamu Nape na Mwigulu ni viongozi wa CCM na si UVCCM. Hivyo kujibiwa na BAVICHA kama hivi ni kuonyesha jinsi walivyo sisimizi katika siasa za bongo. Bravoo BAVICHA kwa kuwaburuza hao vinyago
 
Amewataadharisha wananchi kuwa CCM inaandaa mauaji ya halaiki Tanzania kwa vitendo vyake hivyo waiogope kama ukoma.[/QUOTE] Nimeipenda hii kauli ya kufungia. CCM na kama kansa inayolitafuna tifa hili na sasa linkaribia kufa. Dawa yao ni ndogo hawa wendawazimu. Wasubiri 2015 tu.
 
Kutoka Ifakara:

Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi amemshukia vikali Mwigulu Nchemba na Nape kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mkamba.

Munishi amedai kuwa Mwigulu alikodi vijana kutoa Manzese na kuwapeleka Iramba ili kumuwinda John Mnyika na kuvuruga mikutano ya Chadema iliyokuwa inafanyika Singida lakini hawakufanikiwa baada ya wanannchi kuwadhibiti kisawa sawa.

Aliwaambia wananchi kuwa vijana hao ni sehemu ya vijana waliopewa mafunzo maalumu ya kudhuru watu kipindi cha uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka jana yaliyofanyika Iramba Singida na Uyui Tabora.

Katika mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na mwenyekiti wa BAVICHA John Heche, Munishi amemgeuzia kibao Nape Nnauye kwa kusema kuwa CCM ndio chama cha kigaidi kwa kuwa kimekuwa kikiendesha vitendo vya kigaidi dhidi ya wananchi akitolea mifano uvurugaji wa mikutano ya Mchungaji Msigwa yenye lengo la kutaka kudhuru wananchi kule Iringa, yaliyofanyika hivi majuzi Singida, umwagaji wa tindi kali kule Igunga, na vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na CCM kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru.

Amewataadharisha wananchi kuwa CCM inaandaa mauaji ya halaiki Tanzania kwa vitendo vyake hivyo waiogope kama ukoma.

Nilijua viongozi wa BAVICHA wana afadhali kumbe na wao ni kama viongozi wakuu wao. CDM nani amewaroga? nani anawatumia na kisha kuwaaacha? kwa nn mnatumia vichwa kufuga nywele badala yakufikiri ?

 
CDM mbona mnajinadi sana kwa kukiponda CCM? waambieni wananchi nini visuion na mission yenu. AU ndo msemo wa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza? CCM kimetulia CDM wanajiuza siyo? jiuzeni kwa bei halali basi siyo bei feki.

Mkuu mti wenye matunda ndio unao popolewa mawe, sasa CCM ndio mti wenye matunda. Haya hata mwalimu Nyerere aliyasema, kuwa viongozi bora watatoka CCM

 
CDM mbona mnajinadi sana kwa kukiponda CCM? waambieni wananchi nini visuion na mission yenu.
Mbona CCM nnaangaika sana kujihami dhidi ya anguko lenu linaloratibiwa na CDM kwa kutumia mbinu chafu? Mbona hamtekelezi ilani yenu ya uchaguzi badala yake mnakodisha majangili kuwadhuru viongozi wa chama makini CDM? Mbona mnaweweseka kwa kukodisha majangili kama anavyosema kamanda Munishi hapo juu? VIVA BAVICHA !
 
Nilijua viongozi wa BAVICHA wana afadhali kumbe na wao ni kama viongozi wakuu wao. CDM nani amewaroga? nani anawatumia na kisha kuwaaacha? kwa nn mnatumia vichwa kufuga nywele badala yakufikiri ?
Mbona na mimi nilidhani wewe ni afadhali kuliko magamba mengine kama wakina Nape lakini nashangaa kwani nini unafikiri kwa kutumia masaburi masaburi badala ya ubongo? Kweli CCM mmechacha.
 
CCM ni imara ndioyo maana wana JF mliotumwa hamlali, CDM wenyewe hawalali kila siku majungu, fitina na chuki. Hiyo ndo ishara ya Uimara wa CCM kwani kisingekuwa imara wabaya wake wasingetapatapa kwa maneno matupu.

Huitaji kuwa na Phd uweze kuelewa kifo cha ccm! We "kenge" uko mjini kwenye maji, hujajua huku vijijin kuna nini!! Hata kama unalipwa kwa kuchangia na kupiga debe, ukweli unabaki kuwa ukweli, that ccm is about to perish. Ma-monitor lizard kama nyie hamuwezi kujifananisha na wanadamu hata kidogo coz hamjapewa "utashi"
 
hivi huyu mchaga mdogo munishi yupo jamani???

huyu ndio anaandaliwa kuchukua uenyekiti wa chama,kama sio yeye ni mnyika mana ndio ndugu wa karibu kabisa na mh.mbowe.
 
mnyika - mjomba ake mbowe

munishi - mdogo ake mbowe

mnyika - katibu mwenezi wa chama

munishi - katibu wa bavicha

mbowe mwenyekiti wa chadema, so;

wakiwa kwenye kikao ni sawa na kikao cha familia au cha ukoo.
 
Nchemba na Nnape hawana lolote na wanachojaribu kufanya ni kutoa maelezo ya kuokoa maisha ya kitu kilichokwisha kufa(CCM).Watanzania hawana muda tena na ccm hata hao wanafiki wafanyeje too late,Mimi nafikiri watulie waanze kufikiria 2015 watakimbilia nchi gani maana lazima cdm ikiingia madarakani wapate cha moyo.
 
munishi hana ubavu wa kujibu hoja za mwigulu ,anatafuta tu aibu.

akamuulize kwanza kitila mkumbo na mnyika kwa nini wameua iramba then aende huko morogoro kuwaeleza hao wananchi.
 
Vigogo zaidi Chadema watiwa mbaroni Send to a friend
Friday, 20 July 2012 23:33
0digg

Waandishi Wetu
VIGOGO watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); Mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo na madiwani wawili, wametiwa mbaroni wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Wakati Dk Mkumbo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, akituhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigullu Nchemba, Diwani wa Kata ya Mabogini Wilaya ya Moshi, Albert Msando na Alex Umbella wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, wamehojiwa na polisi kwa makosa ya jinai.

Dk Mkumbo amepandishwa kizimbani jana akiunganishwa katika kesi inayomkabili Ofisa wa Sera na Utafiti wa chama hicho kikuu cha upinzani, Mwita Waitara Mwikwabe (37).

 
napenda sana kazi wanayoifanya bavicha wakati uvccm wako uhamishoni
 
mnyika - mjomba ake mbowe

munishi - mdogo ake mbowe

mnyika - katibu mwenezi wa chama

munishi - katibu wa bavicha

mbowe mwenyekiti wa chadema, so;

wakiwa kwenye kikao ni sawa na kikao cha familia au cha ukoo.



nani kasababisha maisha magumu kwa watz..........ni familia ya kikwete... Ndiyo maana hata kampeni zilifanyika kifamilia.........familia ya kikwete ndiyo inayosafiri sn duniani kuliko familia ya rais yeyote na kusababisha gharama kubwa ambazo no mzigo kwa watz.......chama gani kipo madarakani kwa miaka 50?....ni ccm na ccm ndiyo wanaoeneza chuki za udini na ukabila kwa watz........
 
CDM mnapoteza ulelekeo , vita ni dhidi na matatizo na si watu, they are just playing with ur minds and diverse ur attention..wamewakamata
 
mnyika - mjomba ake mbowe munishi - mdogo ake mbowe mnyika - katibu mwenezi wa chama munishi - katibu wa bavicha mbowe mwenyekiti wa chadema, so; wakiwa kwenye kikao ni sawa na kikao cha familia au cha ukoo.
Wanaofikiri kwa kutumia masaburi wako kazini sasa. Mufilisi wa mawazo hawa
 
Mwigullu na Nape hivi sasa ndo threat kubwa kwa CDM nini? mbona watu wadogo sana hawa inakuaje wawe tishio kiasi hiki, hapo SANGARA hawajaunguruma. Hakika CDM ni dhaifu, kila siku Nchema, Nape. Siyo vipaumbele vya maendeleo.

Naona unatekeleza hilo agizo hapo chini:
CHAMA CHA MAPINDUZI
KUHUISHA MTANDAO WA WANA CCM KATIKA VYUO NA MASHINA YA WAKEREKETWA
Kumetokea na sura tofauti katika hali ya kisiasa nchini hivi karibunikufuatia propaganda za CHADEMA kutaka kujipatia umaarufu na kujitafutia uhalalikwa njia ya kuichonganisha serikali na wananchi na kupandikiza chuki dhidi yaChama cha Mapinduzi. Hali hii imedhihirishwa na juhudi za makusudi zilizofanywana chama hicho za kupotosha ukweli, kutokuona ukweli na kung’ang’ania uzushikuwa ndio mtaji wao wa kisiasa bila hata kujali masilahi ya Taifa na misingi yautu iliojengwa kwa wananchi wake. Kwa mfano kumekwepo na upotoshaji wa kuwahakuna uthubutu wa serikali ya awamu ya nne, ubunifu, kubeza mafanikio nawakati mwingine kuropoka kuwa hakuna mafanikio yaliofikiwa tangia uhuru. Piakumekwepo na lawama kuhusu kupanda kwa gharama za maisha bila hata kuzingatiachanzo cha gharama hizo kinatokana na nini badala yake lawama zinatolewa kamavile bei zimepandishwa na Chama na Serikali na viongozi wake.Hii imesababisha baadhi ya wananchi kwa kutokujua ukweli kupotoka nawengine kushabikia nadharia bila kutaka ukweli na bila kujali madhara yaushabikiaji wa vitu vya kizushi kuwa una athiri umoja, aman, utulivu nahata shughuli za uzalishaji . matokeoyake tumekuwa tukishuhudia vitendo vya uvunjifu wa taratibu maeneotofautitofauti.Baadhi ya vitu vilivyochangia kukua kwa wimbi hili katika vyuo vikuu na maeneo mengine kamailivyoelezwa katika kikao cha baadhi ya wabunge vijana na viongozi na wanachamawa vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma ni

  • Kudhofika kwa UVCCM na vitengo cha propaganda vya CCM kwa ngazi zote kiasi cha kupungua kwa watu wa kukitetea chama na kuelezea mafanikio yaliopatikana kutokana na jitihada za serikali yake.
  • Kupungua kwa moyo kujitolea kufanya kazi za chama kwa wa CCM wakati usio wa uchaguzi na kuyaacha baadhi ya makundi kama vijana bila mawasiliano mpaka wakati wa Uchaguzi. Kukosekana kwa mikutano na wanachama kwa viongozi wa vijana Taifa hata ile isio rasmi kiasi cha kuwafanya wafuasi wa CCM vyuoni kuwa wapweke.
  • Kutokufanyika kwa semina za mara kwa mara kwa wanafunzi zinazohusu fursa hivyo kuwafanya wakate tama na kupotoshwa kirahisi kwa kauli za vitisho za wapinzani.
  • Kutokuwafanyia semina za mara kwa mara kwa wakereketwa wa CCM walioko vyuoni ili kuimarisha uhusioano na chama na serikali na kujua undani wa chama, sera na mafanikio yaliofikiwa na serikali ili kuwa na mwelekeo wa pamoja na kauli ya pamoja wanapoitetea serikali
  • Wanafunzi walio wana CCM kukosa mawasiliano hata ya kufikisha taarifa za siri punde kunapokuwepo na vuguvugu vyuoni na pia hakuna mtandao wa kuwafikishia taarifa hata wafuasi wa CCM kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuhusu malalamiko ya wanachuo.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa kauli za wahadhiri wanapoibeza serikali wanapofundisha na wakati mwingine kufanya kampeni za wazi wazi darasani kinyume na sheria za utumishi wa uma za kutokufanya siasa mahali pa kazi.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa vurugu wanazofanyiwa wafuasi wa CCM na wanafunzi wasiounga mkono migomo. Wakati mwingine wanafunzi wanafanyiwa fujo kwa kuvaa sare za CCM na kuzuiwa kutoka maeneo ya vyuo kwenda katika mikutano.

Kwa upande wa Mashina ya wakereketwa kumetokea malalamiko ya vijanakutotumika kwenye shughuli za kisiasa mpaka wakati wa uchaguzi. Pia kumekwepona malalamiko ya kukosekana kwa ufafanuzi punde chama au viongozi wakuu wanapokuwawamepakwa matope hivyo kuwafanya wafuasi wa CCM kuanza kuzomewa mitaaniwanakoishi kuwa wameshindwa kujibu.

  • Hii inawavunja nguvu wakereketwa wanapoambiwa kutokujibiwa malalamiko au matope yaliorushwa ni ishara ya ukweli.
  • Pia kimekosekana kitengo cha propaganda na kutawala vyombo vya habari hata vilivyo vya serikali kiasi kwamba hata panapokuwa pameandikwa habari ya CCM, wapinzani ndio wanakuwa wameiandika hivyo kuwa na madhara kwa Chama.

Mapendekezo

  • Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu na ofisi ya mnadhimu mkuu ziongezewe nguvu ili zifanye shughuli ya kwenda hatua zaidi ya wapinzani kwa kuwa na watu wanaoshughulikia mambo haya. Vinatakiwa viwepo vitengo vya propaganda kwa kila ngazi viwezeshwe na kuratibiwa ili viende sambamba na matukio makuu katika kalenda. Kwa mfano maadhimisho ya CCM yawe na midahalo ya wana CCM, wanavyuo wetu na wananchi kwa ujumla, siku ya akina mama iwe na midahalo, sikukuu ya mungano iwe na midahalo na yafanyike maandalizi na fursa hizo zitumike kukosoa wale ambao wamekuwa wakileta lugha zenye madhara kwa hatima ya mungano nk.



  • Kuwepo na kikundi maalum katika ofisi ya umoja wa vijana na wabunge vijana kushirikiana na ofisi ya Chama taifa, ofisi ya waziri anayehusika na mahusioano na uratibu na mnadhimu mkuu kushughulikia kupangua hoja za kizushi za upinzani na kutoa mapendekezo staiki kuhusu kutengeneza mtaji wa kisiasa kwa makundi mbalimbali ya jamii.
  • Kikosi hicho kiimarishe mtandao kwa wanavyuo wanaomaliza masomo wajulikane walipo na ikibidi wawezeshwe ili wafanye kazi ya kukisemea vizuri chama popote walipo na wawe chachu pale mahali pa kazi walipo.
  • Kitengo hicho kiratibu midahalo na kutafuta wana CCM wanaoweza kuwa na majibu mazuri zaidi kulingana na uhusiano wa maada husika na utalaam na uzoefu wa msemaji anaestahili kushiriki
  • Kuhamasisha wana CCM kushiriki midahalo kwa njia za simu na wakati mwingine kuwaweka wana CCM kimkakati kushiriki mjadala hiyo tokea sehemu mbalimbali maada inapokuwa na mvuto wa kisiasa, masilahi ya kitaifa na chama chetu
  • Kupitia mwavuli wa Ofisi ya mahusiano na uratibu kitengo kiwe na uwezo wa kujibu kila hoja kwa kupata ushauri, majibu stahiki na makubaliano tokea kwa wataalam na wakuu wa wizara husika inayoguswa na agenda.
  • Kikundi kihusike na kutembelea wanavyuo na kufanya mawasiliano ya uamzi wa chama na makusudio ya serikali kutengeneza wasemaji wa agenda za serikali ndani ya jamii.



  • Kikosi hicho kishirikiane na wabunge wa kila jimbo kutembelea shule za sekondari kwani hao ndio wanavyuo wajao na wapiga kura wa uchaguzi ujao. Ni vyema pia ifanye mikutano ya hadhara nchini kote punde zinapotokea kauli za kukishambulia chama chetu. Wahusike wanachama, viongozi wa wilaya, mikoa na wabunge kukanusha na kulaani kauli za uongo. Hili liratibiwe na ofisi ya chama makao makuu, mikoa, wilaya, kata na matawi.



  • Kitengeneze utumiwaji wa wataalamu wa fani mbalimbali kufanya mawasilianao kwa njia ya SIMU NA INTERNET kueneza sera za chama na kazi za serikali.
  • Kuwepo muda maalumu na kikundi maalumu cha wabunge wa kuandaliwa kupeleka hoja au kujibu hoja watakaoweza kufanya hivyo kwa hisia za juu kuleta msisimko wa kisiasa na kuwapa moyo wana CCM pote walipowasiwe wanyonge.
  • Kutengeneza mtandao wahadhiri watakaokuwa wanakisemea vizuri chama mahali pakazi
  • Kufanya tafiti za siri kuhusu misimamo ya wateule wa nafasi mbalimbali kwa chama ili kuepuka hujuma na usaliti wakati wa uchaguzi.
  • Kukutana na viongozi wa kidini kuwaweka sawa na kutambua kuwa chama kinawajali na kujua umhimu wao katika amani ya nchi
  • Kukosi pia kitakuwa kinahusika kutengeneza mtazamo wa pamoja kuhusu jambo linalohusu nchi na kutafuta watu maeneo tofauti kulisemea jambo hilo, mfano mambo ya kuzingatiwa katika katiba mpya.
  • Kuanzisha ofisi, matawi na kuratibu upatikanaji wa wana CCM kushika uongozi kwenye serikali za wanafunzi.
  • Kuhusu vijana wa kwenye majiji na mijini na miji midogo wasio na ajira, wizara ya inayohusika na biashara na wizara inayohusika na vijana iangalie namna ya kutekeleza mpango maalumu wa kuwarudisha vijana walioasi chama kwa madai ya hali ngumu ya maisha.
  • Kwa mfano wizara husika zinaweza kufanya sensa na kupata idadi ya vijana wanaoweza kutambulika na kukopesheka halafu watafutiwe supplier maalumu aagize kwa jumla pikipiki na bajaji halafu zikopeshwe kwa vijana badala ya utaratibu wa sasa wanaoajiriwa na kupeleka hesabu kwa matajiri wao, wapeleke hesabu kwa supplier na punde deni likiisha pikipiki zinakuwa za kwao. Lakini mpango huo ufanyike kimkakati ili uweze kuleta manufaa kwa chama.
  • Mfano wa mkakati ni kwanza kufanyika kampeni ya kukaa vikao vya ndani na vijana kila miji watakao pata kwa kila awamu watakuwa chachu.
  • Mfano wa pili ni kuwakusanya vijana ambao wana ufundi wowote wawezeshwe halafu wafanye kazi na serikali. Kwa mfano wanaoweza kutengeneza madawati wajulikane watengeneze madawati ya shule zote za misingi, sekondari na vyuo kwa ushirikiano na serikali.
  • Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi uwahusishe wananchi ili waone vinavyofanyika pamoja na wabunge kutumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa kinachotekelezwa kilikuwepo kwenye ahadi. Kwa mfano vitabu visigawiwe kimyakimya kwa kuwatumia watendaji wa sekta ya elimu kuwakabidhi waratibu na waratibu kuvifikishia ofisini bali kuwe kunafanyika mikutano inayohusisha wanafunzi na wananchi ili wajue hatua zinazochukuliwa. Ifanyike hivyo kwa huduma za afya, kwa maabara, umeme n.k kwa kadri itakavyowezekana.
  • Hii itapunguza wananchi kudanganywa mathalani walikuwa wanaambiwa wao ndio wamejenga shule za sekondari za kata sio serikali ya CCM lakini ukweli ni kwamba mchango wa wananchi kwenye ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, zahanati na vituo vya afya ni maboma peke yake na mambo yote yanayosalia ni fadha za serikali. Utaona kuwa fedha ya serikali ni kubwa lakini kwa kuwa zinatoka kimya kimya kwa njia ya akaunti wananchi wakiambiwa wamejenga wanadhani ni michango yao imefanya kila kitu.

“WE STILL HAVE THE CONTROL OF THE MATCH”
MUNGUIBARIKI CCM
MUNGUIBARIKI TANZANIA
MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB)

JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI

 
Mwigullu na Nape hivi sasa ndo threat kubwa kwa CDM nini? mbona watu wadogo sana hawa inakuaje wawe tishio kiasi hiki, hapo SANGARA hawajaunguruma. Hakika CDM ni dhaifu, kila siku Nchema, Nape. Siyo vipaumbele vya maendeleo.

Hapa ndo level yako ya kufikiri ilipoishia siyo??? Hebu tupatie vipaumbele vya maendeleo vya hao unaowatetea!
 
Back
Top Bottom