Katiba za Vyama vya Siasa

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Waungwana,

Kwa kuwa kila Mtanzania ana haki ya kujiunga na chama chochote kile cha Siasa, basi, kabla ya kujiunga na chama hicho, anayo haki ya kusoma na kukagua katiba za vyama vya siasa ili apate kuelewa, kukubali na/au kukataa sera za vyama hivyo. Kwa mujibu huo, anayo haki ya kupata nakala - iliyochapishwa au ikiwa kwenye mfumo wa tarakinishi - za katiba za vyama hivyo vya siasa.

Je, waungwana, wapi nitapata katiba za vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa hapa nchini?

./Mwana wa Haki
 
Nadhani CHADEMA wana katiba yao kwenye website yao. Sina uhakika na vyama vingine. Jaribu kuvi-google search.
 
Kuna wanachama hapa JF watumie PM nadhani watakusaidia,

CHADEMA wasiliana na Zitto ama Dr.W.Slaa
CUF wasiliana na Mwiba
CCM wasiliana na Kibunango ama FM ES
NCCR Mageuzi wasiliana na Waridi

Vyama vingine anayejua atakusaidia.
 
Back
Top Bottom