Katiba: Wananchi Waliwakilishwa-Dr. Kashilila Live on TBC!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi, wale wenye access na TBC, watch TBC -1 now, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila yuko live akiongelea mchakato wa katiba.

Dr. Kashilila amesisitiza kuwa sii kweli wananchi hawakushirikishwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Wananchi wameshirikishwa kikamilifu kabisa kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Kama kuna wabunge ambao walipaswa kuchangia lakini hawakuchangia, hao sasa ndio waliowakosesha haki wananchi wao na katiba ijayo itaweka kifungu cha kuwawajibisha wabunge wasio wawakilisha wananchi wao ipasavyo!.

Dr. Kashilila ameandamana na Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye amethibitisha wamepokea mapendekezo ya Jukwaa la Katiba kwa mara tatu tofauti na mawazo yao yamejumuishwa kwenye muswada huo!.

Endeleeni kufuatilia...
 
Nimeona na mwandishi mkuu wa sheria anasema wananchi walishirikishwa katika hatua zote na jk asingesaini muswada angeonekena amedharau wabunge wa chama chake cha ccm.
 
Me ndio maaana siishi kupigwa ban kwa mambo kama haya,huwa najikuta nimetukana kwa sababu ya hasira,hasa hawa magamba wananikera sana kwa mamboa yao kipuuzi,sasa ni mwananchi gani alieshirikishwa?labda wale wnanchi wa Msoga ndio walioshirikishwa.
 
Osca Elia, huyo Mwandishi Mkuu wa Sheria amesema kama muda ungeruhusu, angewaonyesha kifungu cha mabadiliko na yameletwa na nani!.
 
Me ndio maaana siishi kupigwa ban kwa mambo kama haya,huwa najikuta nimetukana kwa sababu ya hasira,hasa hawa magamba wananikera sana kwa mamboa yao kipuuzi,sasa ni mwananchi gani alieshirikishwa?labda wale wnanchi wa Msoga ndio walioshirikishwa.
Kichomiz, wale jamaa kule mjengoni ni wawakilishi wa nani?. Ukiondoa wale 'kula kulala, wa sadaka, wa sadakakawe na mapoozeo kibao, waliochaguliwa na wananchi ni wawakilishi wetu!. Chochote wachofanya mle ndani, wanafanya kwa niaba yetu!.
 
Tunao wabunge na kazi yao ni kutunga sheria hy ndo moja ya kazi yao, sasa wanapotutupia mpira wananchi cjwi wamesahau majukumu yao,. Kwani sheria ngapi zimetungwa kwa kushirikisha wananchi moja kwa moja?
 
Wanabodi, wale wenye access na TBC, watch TBC -1 now, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila yuko live akiongelea mchakato wa katiba.

Dr. Kashilila amesisitiza kuwa sii kweli wananchi hawakushirikishwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Wananchi wameshirikishwa kikamilifu kabisa kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Kama kuna wabunge ambao walipaswa kuchangia lakini hawakuchangia, hao sasa ndio waliowakosesha haki wananchi wao na katiba ijayo itaweka kifungu cha kuwawajibisha wabunge wasio wawakilisha wananchi wao ipasavyo!.

Dr. Kashilila ameandamana na Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye amethibitisha wamepokea mapendekezo ya Jukwaa la Katiba kwa mara tatu tofauti na mawazo yao yamejumuishwa kwenye muswada huo!.

Endeleeni kufuatilia...

mzee wa kifungu cha 87, znz ni nchi? If so katiba ya jamhuri imepambunua vp kuhusu ili.... If knw nothn abt this pls zip ur mouth i dnt need ur comment..
 
Pasco,

..huyu Dr.Kashilila ni Katibu wa Bunge wa ajabu kidogo.

..yaani ni tofauti kabisa na wale waliomtangulia kama Pius Msekwa, Mahamoud Mwindadi, na wengine.

..sikuwahi kusikia makatibu hao wakienda kwenye vyombo vya habari na kulumbana na wabunge.

..iliamuliwa kwamba mswada ukajadiliwe na wananchi na ziliteuliwa kanda 10. mswada ilikuwa upelekwe hata Unguja na Pemba ili wananchi waelezwe kilichomo, na waweze kutoa mawazo yao.

..sasa kwanini mswada haukupelekwa huko mikoani kwenye hizo kanda 10 zilizoteuliwa?

..wananchi walipaswa KUSHIRIKISHWA, siyo "kuwakilishwa" kama wanavyosema Dr.Kashilila na mwenzake.
 
Hawa jamaa bwana walikuwa watatu lakin hawaelez kitu kinachoeleweka......mswada uliandikwa kingreza hao wananchi walijadili vipi?,,wananchi waliomba uandikw kiswahili ili waweze kuchangia,,,vilaza wamefanya hivyo na kuendelea hatua nyingine....
 
Zanzibar ni NCHI.

Tanganyika ni NCHI.

Tanzania ni MUUNGANO.

Otherwise ni wishingfull thinking ambazo hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali.

topical go back 2 Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema nini Kuhusu Tanzania... Tanzania ni Muungano nakubaliana na wewe, Tanganyika ni nchi, na znz ni nchi nakataa... Niambie unaongea haya kwa mujibu wa katiba ipi... Katiba 2liyo nayo japo na mapungufu yake imeweka wazi " TANZANIA NI NCHI MOJA NA NI JAMHURI YA MUUNGANO" Sasa wewe umeona wapi duniani Kuna Nchi ndani ya Nchi, hii ni mpya duniani and shud b added 2 Guiness World Record..
 
Katibu wa bunge ni mwanasiasa wa chama gani ??

Napatashida kuelewa inawezekanaje mtu unataka kupata maoni ya wa toka mikoa 26 (population) halafu unachukua sample ya mikoa mitatu tu te kijieneo kuwakilisha nchi nzima Halafu unajisifu I conducted a research huu ni " uhuni " tu.

Haya ni mambo ya ajabu katibu kujibu hoja za wabunge ili hali mwanasiasa Spika yupo. Ndiyo maana hata CHADEMA wanasema Spika aliingilia kazi za kamati Sijui kwa kutokujua au ni makusudi mazima mazima

MUNGU WANGU INUSURU HII TANZANIA YANGU

Me ndio maaana siishi kupigwa ban kwa mambo kama haya,huwa najikuta nimetukana kwa sababu ya hasira,hasa hawa magamba wananikera sana kwa mamboa yao kipuuzi,sasa ni mwananchi gani alieshirikishwa?labda wale wnanchi wa Msoga ndio walioshirikishwa.

Kama mbunge wako hakukushirisha uende ukamkoromee mbunge wako huko, sheria imeshasainiwa, mtaifata mkitaka msitake, isuseni kama mnaweza, wewe unafikiri vibunge vyenu 23 ndio vinawakilisha wananchi wangapi wa Tanzania hii, msituchafuwe.
 
Hawa jamaa bwana walikuwa watatu lakin hawaelez kitu kinachoeleweka......mswada uliandikwa kingreza hao wananchi walijadili vipi?,,wananchi waliomba uandikw kiswahili ili waweze kuchangia,,,vilaza wamefanya hivyo na kuendelea hatua nyingine....

Tena sheria mpya, imeshaanza kutumika leo, bora muisome vizuri, isije ikawapeleka alikopelekwa Lema.
 
Katibu wa Bunge ameponda kwamba waliotoka nje bungeni walipoteza fursa ya kuwakilisha maoni ya wananchi. Hivi wale waliobaki ndio waliwakilisha maoni sahihi ya wananchi?

Hivi mipasho na vijembe vile ndio yalikuwa maoni ya wananchi?Hivi alichosema Lusinde ndiyo yalikuwa maoni ya wana Mtera? Huyu katibu wa bunge nae sifuri brain!
 
topical go back 2 Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema nini Kuhusu Tanzania... Tanzania ni Muungano nakubaliana na wewe, Tanganyika ni nchi, na znz ni nchi nakataa... Niambie unaongea haya kwa mujibu wa katiba ipi... Katiba 2liyo nayo japo na mapungufu yake imeweka wazi " TANZANIA NI NCHI MOJA NA NI JAMHURI YA MUUNGANO" Sasa wewe umeona wapi duniani Kuna Nchi ndani ya Nchi, hii ni mpya duniani and shud b added 2 Guiness World Record..

Katiba inasema "Tanzania ni Muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar" ambayo inategeneza United Republic of Tanzania..

Nyinyi bana mnapenda kuchafua hali ya hewa bila sababu..why? nia zenu nini kwanini mnapenda kuleta dharau hasa kwa nchi na watu zanzibar??
 
Pasco,

..huyu Dr.Kashilila ni Katibu wa Bunge wa ajabu kidogo.

..yaani ni tofauti kabisa na wale waliomtangulia kama Pius Msekwa, Mahamoud Mwindadi, na wengine.

..sikuwahi kusikia makatibu hao wakienda kwenye vyombo vya habari na kulumbana na wabunge.

..iliamuliwa kwamba mswada ukajadiliwe na wananchi na ziliteuliwa kanda 10. mswada ilikuwa upelekwe hata Unguja na Pemba ili wananchi waelezwe kilichomo, na waweze kutoa mawazo yao.

..sasa kwanini mswada haukupelekwa huko mikoani kwenye hizo kanda 10 zilizoteuliwa?

..wananchi walipaswa KUSHIRIKISHWA, siyo "kuwakilishwa" kama wanavyosema Dr.Kashilila na mwenzake.
Joka Kuu, mtangazaji alimuuliza Dr. Kashilila, ni kigezo gani walitumia kuwasikiliza watu wa Dar, Dodoma na Zanzibar tuu jee mikoa hiyo ndio wawakilishi wa waTanzania?.

Dr. Kashilila hakuwa na jibu zaidi ya kusema miswada kibao imepitishwa hivyo!. Akimaanisha muswada ule umepitishwa kwa mazoea tuu hivyo tutapata katiba ya mazoea!.
 
]Katibu wa bunge ni mwanasiasa wa chama gani ??

Napatashida kuelewa inawezekanaje mtu unataka kupata maoni ya wa toka mikoa 26 (population) halafu unachukua sample ya mikoa mitatu tu te kijieneo kuwakilisha nchi nzima Halafu unajisifu I conducted a research huu ni " uhuni " tu.

Haya ni mambo ya ajabu katibu kujibu hoja za wabunge ili hali mwanasiasa Spika yupo. Ndiyo maana hata CHADEMA wanasema Spika aliingilia kazi za kamati Sijui kwa kutokujua au ni makusudi mazima mazima

MUNGU WANGU INUSURU HII TANZANIA YANGU
[/SIZE]

Hivi wewe ulikuwa hujuwi kuwa wabunge wanawawakilisha wananchi? na muswada umepitishwa Bungeni? Na sasa si muswada tena ni sheria, au ulikuwa hujuwi hilo?

Back
Top Bottom