Katiba: Mtikila na Hoja ya Tanganyika

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
MWENYEKITI wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amewataka Watanzania kuunda katiba mpya itakayotambua serikali ya Tanganyika iliyokufa baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi za chama hicho, zilizoko Ilala Mchikichini, Mtikila alisema uhuru wa Tanganyika wa Desemba 9 mwaka 1961 uliporwa na Muungano uliovunja serikali ya Tanganyika na kuiacha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wito huo wa Mtikila nakuja siku kadhaa baada ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, kupitisha marekebisho ya katiba ya Zanzibar, inayompa mamlaka Rais wa Zanzibar kugawa mipaka ya visiwa hivyo bila kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Mtikila mabadiliko hayo yamevunja rasmi muungano na kwamba sasa ni wakati wa Watanganyika kutafuta upya uhuru wao.

"Hatimaye Wazanzibari wamejirudishia rasmi utaifa wao, kwa kurejesha rasmi hadhi yao kikatiba kwamba wao ni nchi kamili. Watanganyika wamebaki wakia wameduwaa," alisema Mtikila.

Alisema Muungano huo, haukuhusiana na mikakati ya Umoja wa Afrika uliopiganiwa na aliyekuwa Rais wa Ghana Kwame Nkrumah na waasisi wengine wa uhuru wa Afrika.

Alidai kuwa Muungano wa Tanzania, uliundwa ili kulinda maslahi ya taifa la Marekani katika kilele cha vita baridi dhidi ya dola la mwisho.
 
Wakuu! Toka mchakato wa katiba uanze, na mvutano uliopo. Pamoja na Zanzibar kubadilisha katiba ya visiwani, kuweka kipendele cha Zanzibar ni nchi, sijamsikia mwanaharakati wa siku nyingi, toka kipindi cha mwalim mpaka awamu ya Mkapa. Akipigania Tanzania bara kuwa ni Tanganyika. Mchungaji Mtikila a.k.a Mzee wa magabachori. Yuko wapi mtanganyika Mtikila? Je pale kwake llala bado anapeperusha bendera ya Tanganyika.
 
yupo humu jamvini, siwezi kutaja Id yake nitakuwa nimevunja sheria na kanuni za JF
 
Yuko anatafuta hela kwa kakobe,misukule na viongozi wengine wa dini....kwa kweli alikuwa mwanasiasa shupavu .makini, na anayeona mbali, lakini kaoteza mwelekeo
 
Labda anajiandaa upya kuipandisha Serikali kizimbani kuhusu suala la Mgombea Binafsi..
 
Kwa hili la Utanganyika nampa 100% ingawa CCM hawapendi lakini litawatafuna na ipo siku watasalimu amri
 
Wakuu! Toka mchakato wa katiba uanze, na mvutano uliopo. Pamoja na Zanzibar kubadilisha katiba ya visiwani, kuweka kipendele cha Zanzibar ni nchi, sijamsikia mwanaharakati wa siku nyingi, toka kipindi cha mwalim mpaka awamu ya Mkapa. Akipigania Tanzania bara kuwa ni Tanganyika. Mchungaji Mtikila a.k.a Mzee wa magabachori. Yuko wapi mtanganyika Mtikila? Je pale kwake llala bado anapeperusha bendera ya Tanganyika.

naye ni gamba tayari, na limemwelemea
 
Jifunze kutumia alama za uandishi au punctuation marks wakati unapoandika. Makosa ya kiuandishi yanaweza yakapelekea makosa ya kimantiki kwa upande wa msomaji na zaidi yanakera kwa kuwa yanamlazimu msomaji atumie utashi wake ku kujudge ulichokuwa unamaanisha.

Kwamfano, ulipoweka kituo cha kwanza sio mahali sahihi. Unachoongea kabla na baada ya kituo cha kwanza ni mawazo 2 tofauti, kwahyo hakuna flow nzuri ya unachoongea..
 
Kwa mawazo yangu Mzee mtikila ni mwanasiasa mzuri ila shida yae ni kiogeugeu.Anaweza kuwasifia wapinzani arafu badaae akawageuka na kuwatukana mpaka anaajikuta anapoteza muelekeo.Mfano kule tarime mpaka alipigwa mawe kwa uropokaji wake.Watu wanashindwa kuelewa kama ni mpinzani au anabeep.
 
mtikila is a hero, his contribution to the jurisprudence of the lega system of tanzania is ernomous,he derseves better treatment from any right think person in this country,he has fought alone against this gingatic ccm government,and he won,he is the champ,,,,LONG LIVE MTIKIRA.GOD BLESS YOU.
 
Jifunze kutumia alama za uandishi au punctuation marks wakati unapoandika. Makosa ya kiuandishi yanaweza yakapelekea makosa ya kimantiki kwa upande wa msomaji na zaidi yanakera kwa kuwa yanamlazimu msomaji atumie utashi wake ku kujudge ulichokuwa unamaanisha.

Kwamfano, ulipoweka kituo cha kwanza sio mahali sahihi. Unachoongea kabla na baada ya kituo cha kwanza ni mawazo 2 tofauti, kwahyo hakuna flow nzuri ya unachoongea..
mijitu mingine bana! Am not a journalist either an editor. Hizo ni taalum za watu jomba...
 
Back
Top Bottom