Katiba mpya ya chadema hatuitaki

Tunataka katiba mpya ya wananchi wote sio maslahi ya CHADEMA. Hii nchi tuna uchungu nayo. Tutapambana mpaka kufa lakini Chadema haishiki madaraka nchi hii. Waende wakachunge ngo'mbe.

Administrators tafadhali anzisheni site nyingine ya Jamiiforums for KIDS.
 
wana JF mnatumia maneno MAKALI SANA, mtanikatisha tamaa ku-post hoja nyingine nzito
 
...CDM na CUF (CCM academia),nani katengeneza rasimu ya Katiba? Umoja wa maimam nao umetengeneza rasimu ya katiba!!! ushauri wangu;tafuta tofauti ya rasimu ya katiba kama ya CUF na katiba sifuri ambayo CDM wanatoa wito wananchi binafs au kuoitia vyama vyao vya kisiasa,kijamii watoe.

matatizo ya kusoma juzuuu sana hayo...lazima urukwe na akili!
 
Naomba nimweke wazi kuwa chama cha chadema ni cha wananchi wote,lia pale tumeweka viongozi tu,kama wewe ulivyo nyumbani kwako unaitwa baba lakini ni mwana familia ya kwako?
 
...CDM na CUF (CCM academia),nani katengeneza rasimu ya Katiba? Umoja wa maimam nao umetengeneza rasimu ya katiba!!! ushauri wangu;tafuta tofauti ya rasimu ya katiba kama ya CUF na katiba sifuri ambayo CDM wanatoa wito wananchi binafs au kuoitia vyama vyao vya kisiasa,kijamii watoe.

matatizo ya kusoma juzuuu sana hayo...lazima urukwe na akili!

mkuu..... draft constitution should be proceeded by national constitution meeting...... sasa hiyo rasimu ya CUF ilipata mawazo kutoka kwa nani.....CDM hoja yao ni kutaka mihimili yote ikubali mabadiliko ya katiba ndipo process ya mabadiliko ianze ikiwamo matayarisho ya rasimu ya katiba
 
Charity boy ni werema.who is werema to take this country to hell? Ukisema katiba mpya kuna watu wanapata pressure yeye ni mmoja wapo, utasikia wanakwambia wananchi , wananchi gani hao tofauti na waliokwisha kuongea?? Maaskofu wanataka katiba mpya, cwt wanataka katiba mpya, waislamu wanataka katiba mpya, tucta/wafanyakazi wataka katiba mpya, wanazuoni wanataka katiba mpya, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wanataka katiba mpya, jaji samata, jaji warioba, jaji kisanga, jaji manento, jaji bomani,jaji ramadhani wanataka katiba mpya , media wanataka katiba mpya,chadema, cuf, nccr,tlp, udp wote wanataka katiba mpya, yeye ag ni nani hasa kuzuia katiba mpya na kwa malsahi ya nani hasa??? Anaogopa nini kuandikwa katiba mpya????? Je hofu hii inatoka wapi???
 
Malaria Sugu, naomba uongoze na kiji signature cha maneno yako yale ya taarab naona kuanzia umeanza kutumia user id mpya umesahau taarab zako za udini
Tunataka katiba mpya ya wananchi wote sio maslahi ya CHADEMA. Hii nchi tuna uchungu nayo. Tutapambana mpaka kufa lakini Chadema haishiki madaraka nchi hii. Waende wakachunge ngo'mbe.
 
Tunataka katiba mpya ya wananchi wote sio maslahi ya CHADEMA. Hii nchi tuna uchungu nayo. Tutapambana mpaka kufa lakini Chadema haishiki madaraka nchi hii. Waende wakachunge ngo'mbe.
Umetumwa................... MS in another name
 
wana JF mnatumia maneno MAKALI SANA, mtanikatisha tamaa ku-post hoja nyingine nzito
Wasio na busara hawatakiwi humu..................na ni kawaida yetu kuwakatisha tamaa hadi hapo watakapobadirika.................. na ikibidi ni kuwauwa kihoja tutafanya hivyo.................. na ukizidi MODS wataingilia kati
 
Oh kidogo niandike Bw/Bi kumbe umesema boy!

Labda twende polepole Unaposema ''Hatutakubali'', ''Hatuitaki'' una maana ya wewe na nani?

Chadema, CCM, CUF*(*kuna utata ka CUF ni chama cha upinzani kwa sasa) na kadhalika, mmoja wao akitawala anatawala kwa ridhaa ya wananchi walio wengi kwa mfumo wa demokrasia. Hivyo kusema kamwe ''hamtakubali'' itategemea kama ''watakaokubali'' watakuwa wengi kuliko ''mnaokataa'' basi hakuna jinsi itabidi Chadema watawale.

Ninachotaka tu uchaguzi uwe wa huru na wa haki ili tuweze kupima kwa urahisi kati ya nyinyi mnaokataa kamwe Chadema wasitawale na wale wanokubali Chadema atawale nani atakuwa ameshinda kwa haki. Kuweza kupima uhaki na uhuru wa uchaguzi basi wale marefa lazima wawe huru. Wasitokane na ''Nyinyi'' ambao mnasema ''hamtakubali''.

Hayo na mengine ndiyo chimbuko kwa nini mimi binafsi naunga mkono kuandika katiba upya.
 
nakushauri upime maneno uliyosema kisha uchukue hatua. Katika majadiliano jaribu kuwa pragmatic. Maneno uliyosema hayaonyeshi uzalendo hata kidogo. Tumeshatoka kwa mfumo wa ukiritimba wa chama kimoja. Chama chochote kikipata ridhaa ya walio wengi kina haki ya kutawala. CCM, CUF, CHADEMA, TLP si vyama kutoka mbinguni/ahera. Ni mifumo iliyoanzishwa na binadamu kutafuta ukubali (mandate) ya wananchi kutawala. Vyama hushindana kwa njia ya sera na kura atayekubarika kwa wananchi ndiyo hutawala nchi.

Wana JF hawakuelewi uanaposema ''nyinyi'' ndiyo wenye uchungu na nchi una maana gani? Kuna mantiki ya ubaguzi kwenye maneno yako. Mtu aweza aelewe kuwa ukiwa mwanachama wa chama kingine zaidi ya kile cha ''nyinyi'' huna uchungu na nchi! Mfano sitoi huu mfano kwa sababu mimi ni mwanachama wa chadema hapana (mimi ni mwanachama wa CCM - sifichi. Nitabadili msimamo wangu mara tu chama chetu kitakapokataa mchakato wa katiba mpya nimekibeba lakini kwa hili utakuwa ndiyo mwisho) tuendelee na point yetu. DR. Slaa akiwa mbunge amesaidia sana nchi kuibua wizi uliokithiri wa fedha za uma, Mwakyembe na wenzake walipambana na ufisadi ndani ya chama chetu hadi waziri mkuu na mawaziri wengine wakajiuzuru.

Wapambanaji ni wengi siwezi kuwataja wote. Wanatoka katika itikadi tofauti za kisiasa na vyama, wote wana uchungu na nchi. Hivyo kusema ''NYINYI'' tu ndio wenye uchungu na nchi unawachanganya wana JF na kwa kweli ni kama unawatukana.

Unaposema waende wakachunge Ng'ombe una maana gani? Nikuelewe kwamba unawadharau wachunga ng'ombe? Wachunga ng'ombe ni sehemu ya wakulima wa Tanzania ambao wanaishi vijijini kama sikosei wako 80%. Kama uko mjini ka mimi tuko 20%, na ndio wazazi wetu hao! Wana JF wakuelewe kwamba unadharau wazazi wako? Una maana mkulima hawezi kuwa na mchango wa kuendesha nchi?

Ukisoma kitabu cha governor Mtei (bahati mbaya tena naye ni Chadema) anasema alikuwa mchunga kondoo hadi akawa governor wakati wa Nyerere (muasisi wa chama chetu - CCM). Watu karibu wote rejea zao ni hawa wachunga ng'ombe na wakulima unaoonyesha kuwa dharau sana. Ndio wapiga kura walio wengi wanakiingiza chama chetu madarakani kila wakati. Na kwa kweli ndio wapiga kura walio wengi wanaoweza kukiingiza madarakani chama cha watani wetu wa jadi (Chadema). Si tabia njema kwa kijana (umesema Charityboy) mdogo kama wewe kuwadharau wazee wako.

Mwisho: Chadema hawajaleta rasimu ya katiba ya nchi alichowakilisha Mh. Mnyika ni pendekezo la namna ya kurasimisha mjadala na mchakato wa katiba mpya ambao unalenga kushirikisha wadau wote wa Tanzania. Mimi ningependa tutumie neno wadau badala ya wananchi wote. Nitakuambia kwa nini. Zaidi ya asimia 45 ya watanzania ni watoto, hata tukipiga kura hawatahusika. Lakini kwa kupitia wadau wao mahitaji yao yatazingatiwa kwenye katiba ipasavyo.

Ukielewa haya inatosha. Ukiwa jasiri basi weka kathread ka-kuapologize!
 
Oh kidogo niandike Bw/Bi kumbe umesema boy!

Labda twende polepole Unaposema ''Hatutakubali'', ''Hatuitaki'' una maana ya wewe na nani?

Chadema, CCM, CUF*(*kuna utata ka CUF ni chama cha upinzani kwa sasa) na kadhalika, mmoja wao akitawala anatawala kwa ridhaa ya wananchi walio wengi kwa mfumo wa demokrasia. Hivyo kusema kamwe ''hamtakubali'' itategemea kama ''watakaokubali'' watakuwa wengi kuliko ''mnaokataa'' basi hakuna jinsi itabidi Chadema watawale.

Ninachotaka tu uchaguzi uwe wa huru na wa haki ili tuweze kupima kwa urahisi kati ya nyinyi mnaokataa kamwe Chadema wasitawale na wale wanokubali Chadema atawale nani atakuwa ameshinda kwa haki. Kuweza kupima uhaki na uhuru wa uchaguzi basi wale marefa lazima wawe huru. Wasitokane na ''Nyinyi'' ambao mnasema ''hamtakubali''.

Hayo na mengine ndiyo chimbuko kwa nini mimi binafsi naunga mkono kuandika katiba upya.
 
Administrators tafadhali anzisheni site nyingine ya Jamiiforums for KIDS.

Hahahahahahahah LOL! kwa maoni yangu hii hata kwa watoto haifai. Hii inabidi ipelekwe kwenye Jamii Forums for Taahiras

Kweli charity Boy hatuitakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom