Katiba Mpya: Serekali za Majimbo Ziwepo, Zanzibar Tuachane Nayo- Tubaki na Tanganyika Yetu

Ukombozi Sasa

Member
Nov 5, 2010
17
10
Katika Mchakato wa katiba mpya mimi moja kwa moja naunga mkono uwepo wa serikali za majimbo. Tunaweza kugawanya Tanganyika katika majimbo matano au sita ya kiuchumi, na jamaa wa visiwani hatuwahitaji, lakini kama watatungangania basi wakubali kutokuwa nchi bali kuwa eneo la Federal Government na hivyo kuongeza idadi ya majimbo Unguja ikawa jimbo moja na Pemba la pili, kitu kinachoitwa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kikabakia kwenye vitabu vya historia......Kwanza wabaki kivyao hawatusaidii chochote ...............

Kwa kuwepo na serikali ya majimbo ni dhahiri kuwa tutakuwa na maendeleo ya haraka kwa maana majimbo yatakuwa na madaraka zaidi katika maamuzi ya kiuchumi, pili serikali ya kitaifa yaani Federal itakuwa na majukumu machache katika kuleta maendeleo na hivyo kuwa na ufanisi zaidi. Si hili tu bali pia kutadumisha demokrasia zaidi na kuboresha usalama wa nchi zaidi kwa kuwa na vyombo vya usalama vyenye mwiinglio mdogo wa kisiasa. Uchumi utapanuka kwa kasi kwa kinachopatikana katika jimbo kitabaki katika maendelea ya jimbo husika, na asilimia fualni itakwenda kwenye serekali kuu ili kusaidia kuboresha usalama wa nchi nzima na kuboresha miundo mbinu ya kitaifa...

Natoa Hoja
 
Mimi naungana kabisa na hoja yako, maana sasa JK amefeli kuongoza nchi, he has completed finished in leadership ethics to the maximum, hana mpya.Serikali ya majimbo ndio sululisho la matatizo. Kuhusu zanzibar, hawa jamaa tuachane nao kabisa huu muungano is a parasite kwetu watanganyika tunataka Tanganyika.
 
Mimi naungana kabisa na hoja yako, maana sasa JK amefeli kuongoza nchi, he has completed finished in leadership ethics to the maximum, hana mpya.Serikali ya majimbo ndio sululisho la matatizo. Kuhusu zanzibar, hawa jamaa tuachane nao kabisa huu muungano is a parasite kwetu watanganyika tunataka Tanganyika.

Serikali ya majimbo sawa .Muungano uimalishwe tuwe na serikali moja .Zanzibar iwe na majimbo mawili pemba na zanzibar yenyewe,Bara kuwe na majimbo kumi
 
Naunga hoja kwa 50% tu,kwa nn...?Jaman UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU,ama si kweli?Asiwadanganye mtu, waungwana huungana na watwana hutengana.Sitaki kuamini kuwa wazo la Mwl na Karume ndo limekuwa vumbi kiasi hiki,hivi we unaedai kunyonywa na zanzibar,leo hii ukiitwa mbele za watu ueleze kivipi unyanyonywa na muungano unalo la kusema au mkumbo tu?Kule China wanausemi NO EVIDENCE NO RIGHT TO SPEAK,so take care ktk hilo.Binafsi sikatai umuhmu wa federal government ila napinga anguko la muungano kwa sera za kikasuku.Issue hapa ni kufunga mkanda tupate katiba mpya itakayotatua kero zote za muungano kwa kuzingatia sera za kukuza uchumi,kudumisha utamadun na kuimarisha siasa.Mungu ibarik Tanzania Mungu ubarik muungano Mungu ibariki Afrika.Naomba kuwasilisha hoja
 
Mimi nakataa kuwa nchi hii ni ndogo kama wasira anavyokejeli wanaounga mkono serkali za majimbo. Hili ndio suluhisho la matatizo yote ya ukata wa serkali kila kitu kiko centralised daresslaam. Pamoja na kuwa na local government nchi hii inaendeshwa na mtu mmoja tu kwa matakwa na hisia badala ya uhalisia wa mambo . Serkali ya majimbo itaconsolidate efforts na kupanga uendelezaji wa raslimali. Kazi ya serkali kuu iwe ni kuregulate policy na kuingilia kati mdororo wa maendeleo ktk eneo husika. Leo tra wanakusanya kodi kila mahali. Kwanza hawatuambii wapi wakusanya nyingi na wapi ni mzigo wa taifa tufike mahali tuwe wazi kila jimbo litumie mazingira yake kujiendeleza. Mambo yacentral gov. Kushikilia madaraka yote ni kuharibu maendeleo ya nchi ndo unaona mtu akifisidi arusha anapelekwa mtwara. Kama tutakuwa majimbo uzururaji huu usio na tija kwa taifa hautakuwepo. Tuachane na mawazo mgando ya akina wassira ambayo kwa miaka hamsini yameshindwa kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu
 
Namuunga mkono mwandishi.
tuseme hamuwafaham waznz wao hawataki muungano!
kwanini munganganie?

hawatakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom