Katiba mpya ni sawa na kupindua nchi - Nimrod Mkono

Dah, aisee huyu Nyerere alifaa kuwa candindate wa PhD ya heshima hata kama amekufa! Alikuwa anaona mbali sana. Yaani wale aliowakataa ndio wengi wao wanatuharibia nchi!

huyu mkono ni kama bidhaa ya kichina...... Ukimtilia maanani utapata dhambi na kumtukana bure acha debe tupu litike...
 
Mkono ni Mwanasheria? - wenzetu wa Kenya ''wamepindua nchi'' na so far so good....
 
Mie sijaelewa ina maana rais na wabunge wameapa kuitetea na kuilinda hata pale wanapoona kuwa maslahi y wananchi yamegandamizwa? Au mpaka wakati gani jamani, mbona wanaweka viraka kwenye hiyo katiba wanayoitetea, je siyo kuisaliti? Nijuzeni wana JF
 
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?

Kenya wamebadili katiba na nchi haijapinduliwa.
 
Huyu ni fisadi mwingine aliyelipwa Shilingi bilioni nane na BoT kwa kazi ambayo alishindwa kuisema ni kazi gani aliyoifanya hadi kustahili kulipwa mapesa mengi kiasi kile. Hata rate yake aliyokuwa anacharge per hour alishindwa kuitolea maelezo maana ilikuwa ni ya kifisadi fisadi tu.
 
hiivi huyu mbunge haoni aibu kwa wananchi wake? huyu nae ni NGUULI FISADI amesema hivo kwa kuwa anfahamu hakuna wa cha kumfanya.............kweeeeli tufumbe mach tusali.
 
kizazi ni kipindi cha miaka thelasini, watu na waamini kuwa kizazi kinaweza kubadili historia kutoka pale watu hawatamki juu ya katiba hata leo wanatamka ..... hawa watamkao ndio watakaobadili katiba na kama ni mapinduzi basi haya ya katiba hayatakuja ghafla.... kama nyakati za Nuhu maji yalijaa ndoo na mwishowe mapipa yalielea juu ya maji ..hii ni kusema walioyatamani maji wakaaelea juu yake...ili mradi tunasali au kuswali......madliko yapo.
 
Naipinduke tu! Tuone huo upande wa pili maana upande huu wanafaidi wao tu!
 
Ngoja tuwaone wabunge wa ccm kama watapinga katiba mpya ili tujue kabisa kumbe ma mp's wa ccm wako pale kwa manufaa yao na sio wananchi
 
hiivi huyu mbunge haoni aibu kwa wananchi wake? huyu nae ni NGUULI FISADI amesema hivo kwa kuwa anfahamu hakuna wa cha kumfanya.............kweeeeli tufumbe mach tusali.

kama ma¥¤$& na wajinga wangekuwa wanapangwa kwa grade huyu angekuwa first grade tena ambayo ni "gud quality"
 
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?
Mkonoooo! ukiona watu wanaanza kuweweseka basi ujue jinamizi la maovu waliyotenda linaanza kuwaandama! Mkono, Werema na kombani they are now hunted by the Ghosts of those whom they mistreated hereafter are referred to "watanzania". na kuwashauri tu They better prepare themselves to face the fact that by hooks and grooks the new Constitution is coming! there is no where to run!
 
Hivi tunahitaji Katiba Mpya (New Constitution) au Mabadiliko/Maongezo ya Katiba (Amendments)?.....Mi nadhani tunahitaji kubadilisha vile vipengele ambavyo havifai (kama vipengele vya uchaguzi etc etc)...ila kupata katiba mpya sio shughuli ndogo, katiba ina vitu vingi sana.

Labda watu waulizwe wanataka hiyo katiba mpya iwe na vitu gani, nahisi wengi wao watashindwa kulist vitu zaidi ya 10. Sasa kwa nini upate katiba mpya badala ya kubadilisha hivyo vipengele kumi 10?
 
Mkonoooo! ukiona watu wanaanza kuweweseka basi ujue jinamizi la maovu waliyotenda linaanza kuwaandama! Mkono, Werema na kombani they are now hunted by the Ghosts of those whom they mistreated hereafter are referred to "watanzania". na kuwashauri tu They better prepare themselves to face the fact that by hooks and grooks the new Constitution is coming! there is no where to run!

mkuu ... Tanzanian's zombies will arrive very soon...... the first victims will be the likes of C.Kombani.., F.Werema.., N.Mkono..., and MS
 
Kwa maoni yangu, habari fupi iliyotolewa juu kinachodaiwa kusemwa na Mh Mkono ni fupi sana kuweza kubaini ni nini hasa alichokusudia na hoja zipi alizokuwa anajenga. Ningemuomba mhariri kwa hisani yake atutolee habari hiyo kwa urefu ili tuwe na haki ya kumkosoa au kumuunga mkono Mkono kadili ya upeo wetu na misimamo yetu.

Kwa upande mwingine, sijaridhika na namna baadhi ya wachangiaji walivyokosa subira kuvumilia hoja tofauti na zao. Nionavyo mimi si lazima wanachama wote wa forum hii kuwa na msiomamo mmoja juu ya mabadiliko ya katiba. Wengine wanaweza kuona kwamba katiba iliyopo ina mapungufu mengi ambayo hayawezi kurekebishwa zaidi ya kuifuta na kuandika nyingine. Wengine wanaweza kuwa na mtizamo kama wa mh. Mkono kwamba kuifuta katiba mpya ni sawa na kupindua Constititional Order tuliyonayo na kuleta mfumo na utaratibu mwingine kabisa.

Kwa wale waliobahatika kukaa katika darasa za sheria watakuwa wamekutana na falsafa nyingi kinzani juu ya maana na nafasi ya katiba katika nchi. Wapo wanatizama katiba kama mama wa sheria na mamlaka zote za nchi. Kwamba kufutwa kwa katiba iliyopo huja tu pale panapokuwa mabadiliko ya msingi sana yanayofanya kanuni na miongozo iliyomo katika katiba na sheria pamoja na mfumo mzima wa kisiasa kupitwa na wakati. Katika sehemu kubwa ya kihistoria, baadhi ya wanafalsafa wa sheria na katiba wanasema, kufutwa kwa katiba na kuandikwa mpya hutokea pale dola iliyopo inang'olewa madarakani, kama ilivyokuwa wakati wa kuondolewa kwa dola za kikoloni. Kwa mitazamo yao, mapungufu mengine ya kikatiba yanaweza kuondolewa kwa marekebisho ambayo huendana na aidha kufutwa kwa baadhi ya vifungu katika katiba na kuandikwa vingine bora zaidi au kuongezwa vifungu vingine kadili vitakavyohitajika.

Jambo la kujiuliza hapa ni je kuna mabadiliko gani ya msingi yaliyotokea Tanzania yanayoifanya Katiba iliyopo kupitwa na wakati? Mmoja kati ya magwiji wakubwa wa sheria ya siasa na katiba Prof Issa Shivji analijibu suala hili kwa kuanisha mabadiliko mbalimbali kama vile kuondolewa azimio la Arusha na kuanzishwa mfumo vya uchumi huria na kuanzishwa mfumo wa vyama vingi badala ya mfumo wa chama kimoja. Maoni ya PROF Shivji pia yanajitokeza katika Repoti ya Utafiti wa Tume ya Nyalali kuhusiana na kuingia au kutoingia kwa Tanzania katika mfumo wa vyama vingi.

Ikumbukwe kwamba kabla Tanzania hatujaingia katika mfumo wa vyama vingi, katiba yetu ilifanyiwa marekebisho ya msingi kupitia Marekebisho ya 8 ya Katiba na baadae ya 9 hadi 12. Marekebisho hayo kwa kiasi fulani yalipunguza mapungufu ya kikatiba yaliyotokana na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi lakini mapungufu yangali yanaonekana. Ni kutokana na ukweli huo kwamba baadhi ya wanazuoni wanaona mapungufu yaliyomo katika Katiba hayawezi kuisha kwa marekebisho, katika lugha ya marehemu Prof Haroub 'viraka". Lakini bado mtu anweza kujenga hoja kwamba pengine hata Tanzania tungeandika Katiba mpya mapungufu yangeendelea kuwepo kutegemeana na namna tulivyoiunda hio katiba kama vile matatizo hayo yangeisha kama marekebisho ya 8 yangefanyika kwa umakini zaidi na kuwashirikisha watu zaidi. Nini ni kweli na nini si sahihi inategemeana na namna tunavyojenga hoja na kufanya utafiti wa kutosha. Pia inategemeana na matashi ya watu.

Dhana ya katiba na nafasi yake katika jamii ni kitu kinachoumiza akili na kinahitaji kuangaliwa kwa jicho pevu. Katiba sio maandishi tu yaliyomo katika kitabu kinachoitwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977. Katiba ni zaidi ya hapo. Uganda ilikuwa ni nchi ya kwanza kuandika Katiba mpya wakati wa upepo wa vyama vingi. Lakini hatuwezi kusema kwamba Uganda ni ya kidemokrasia zaidi ya Tanzania au Kenya. Pia hatuwezi kusema kwamba matatizo ya kidemokrasia Uganda (kama yapo) yanasababishwa na Katiba yao mpya kutokuwa nzuri. Ninachomaanisha hapa ni kwamba tunapojadili katiba mpya tunapaswa kujadili kwa upana zaidi kwa kuingalia katiba iliyopo tukiihusisha na histria nzima ya siasa na uchumi wa nchi, maisha ya watanzania, mahusiano yetu ya kijamii na maadili kwa ujumla.

Kwa haya niliyosema sikuwa na lengo la kufanya hitimisho lolote bali kufanya madodoso ya hoja mbalimbali ili kupanuwa mawazo ya wachangiaji na uwigo wa mjadala kwa nia ya kuboresha zaidi. Kama kunasehemu nitakuwa nimewachanganya wbnaadhi ya wachangiaji hiyo itakuwa imetokana na mapungufu yangu katika lugha.
 
mkuu.... maono ya mapungufu ya katiba kwa watanzania wanayoijua katiba sio kitu cha kuficha ...... niambie tunatakiwa kuchukua jukumu la kuelimisha wasiojua ..., lakini kwa wale wanaojua katiba ya sasa ..... there is no way ya propaganda nyingi zinazohitajika eti kwamba tuangalie marekebisho yapi yanahitajika kuandika katiba mpya... take an example ....on the matter of human rights our constitution still holds for death penalty..... do we need it or we should abolish the so called capital punishment..... obvious and with no doubt Tanzanian constitution is "Obsolete" .... so what next.... we need no revisions or amendments.... we need a new draft constitution... forget about unfold coincidence with our fellow Kenyans.....whom we are getting in together in a so called federation.... this can humbly being referred as double coincidence of wants
 
Nimrod in kichaa wa sheria.. Katiba ni yetu... Wakati wa uchaguzi slaa alisema akishinda ataanza mchakato wa katiba mpya... Hilo halina ubishi sisi ndiyo watanzania na ndiyo wananchi tumeona mapungufu ya katiba yetu sasa tunataka tuiandike upya na kuondoa vile vyote visivyofaa...

Tanzania kwa pamoja tutabadilisha nchi na katiba yetu..
 
Uko sahihi kabisa ndugu yangu kwamba katiba yetu inayo mapungufu. Hoja niliyojaribu kuchokoza ni kama kila mapungufu yanahitaji katiba mpya? Lengo langu ni kuwataka wanamjadala kujenga hoja kwamba kuna mapungufu makubwa na ya msingi ambayo hayawezi kurekebishwa kwa marekebisho ("amendment"). Suala la hukumu ya kifo, kwa maoni yangu binafsi ni suala ambalo linaweza kuondolewa hata bila kurekebisha katiba. Katiba yenyewe haisemi kwamba muuwaji auwawe. Katiba inalinda haki ya kuishi. Haki hiyo hata hivyo sio absolute kwa mujibu wa katiba tuliyonayo. Inaweza kuondolewa kwa sheria ya Bunge kama kufanya hivyo ni lazima/mhimu katika kulinda maslahi ya umma. Kwa Tanzania, kuna makosa kama matatu ambayo yanawea kupelekea hukumu ya kifo: mauwaji ya makusudi na uhaini. Suala ni kama utashi wa watu wengi ni kukomesha adhabu ya kifo katika makosa yote? Hamna utafiti huria uliwahi kufanyika Tanzania na kutoa jibu la suala hili. Wakati wauwaji wa albino mwanza na shinyanga walivyohukumiwa kifo, idadi kubwa ya watu ilionesha kushabikia. Hata hivyo, hii haiwezi kumaanisha kwamba watanzania wengi wanapenda adhabu ya kifo katika makosa ya uuwaji wa makusudi iendelee. Yawezakana ikwa ni uhaba wa elimu ya haki za binaadamu kwao. Mhimu hapa ni kwamba kama adhabu hiyo bado inafaa au la ni maoni ya watu yatakayoamua sio maoni ya wasomi na wanaharakati wa haki za binaadamu pekee yako. Nikirudi katika mada, suala la adhabu ya kifo linaweza kufanyika bila kuigusa katiba kwa kurekebisha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Bado ninamaoni kwamba ili kuweka wazi umhimu wa katiba mpya na ili kuwashilikisha watu wengi katika mjadala huu wasomi na wasio wasomi bado ni mhimu kubainisha mapungufu ya msingi katika katiba yetu na mfumo mzima na kupendekeza namna tunavyotaka iwe.
 
Huyu Mbunge Alietoa Hoja Kweli ni Maskini wa Mawazo. Hii Inaonyesha Kitu Gani Mbunge Anachaguliwa Akiwa na Mawazo Kama Haya. Anyway Ndivyo Mafisadi Wanavyo Fikiria. Vichwa Maji, Ubinafsi na Udikteta.
 
Back
Top Bottom