Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni lazima sii hiyari-tudai vyote

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mkombozi, Nov 4, 2010.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana Jamaii

  Kwa tangu J3 sijapata usingizi kabisa hasa mara baada ya uchaguzi. Hii ni kutokana na kwamba nilikua na wasiwasi mkubwa hususani hatma ya kura yangu niliyopiga. Jana baada ya Dr Slaa kutoa tamko la mwenendo wa uchaguzi basi usingizi hakuja kabisa mpaka sasa hasubui hii. Dr Slaa jana alisema baadhi ya matokeo ya Urais yamechakachuliwa alitoa mfano kuna Jimbo ana kura 15,000 lakini Tume imetangaza 3,000. Ina maana kuna panga la kura 12,000. Inawezekana kura niliyopiga au uliyopiga ni miongozi mwa hizo 12,000. Hii inauma sana na inasikitisha. Pia ni kinyume na haki za binadamu kwa mojibu wa katiba ya sasa. Pia Dr Alisema kulikua na kata hewa ambazo hazipo physically.

  Kwa maana hiyo tutakubaliana na mtu mmoja aliyewahi kutamka kua SISIMU inaweza kutawala milele. Sasa basi nini kifanyike ili kuepusha haya? Mimi nadhani tukianzia na wabunge wote wa upinzani, vyama visivyo na wabunge, taasisi ya haki za binadamu, vyama vya kiraiya na makundi mbalimbali kutia msukumo wa kubadilisha katiba na kua na tume huru ya uchaguzi. Bila hivi viwili kufanyiwa kaza ili kua na katiba mpya kabisa na tume huru ya uchaguzi, swala la utawala wa raiya umma ni ndoto Tanzania. Napata uchungu sana.

  Katiba Mpya kabisa

  1.Itakayoruhusu kuchallenge matokeo yeyote yakiwemo ya urais Mahakamani
  2.Kumwondolea mkuu wa nji kinga
  3.Kupunguza madaraka mengi kwa mtu mmoja
  4.Kuwa na mgombea binafsi
  5.Kuwe na tume huru ya Upinzani
  6.Spika wa bunge na makamu wake wasiwe wanatoka chama kimoja

  Tume Huru Ya uchaguzi

  Tume isiwe inateuliwa na kuriport kwa mtu mmoja, pia wasimamizi wote wasiwe watumishi au wanachama wa chama chochote. Ikiwezekana hii tume iwe inawajibika kwa bunge na sio kwa mtu mmoja. Tume iruhusu matokeo ya ngazi zote kutangazwa kuanzia vituoni, katani, jimboni n.k.

  Makundi yaliyotajwa hapo juu, mvifanyie kazi hivi ili uchaguzi ujao uwe wa raiya/umma na sio kwa matakwa ya mtu Fulani. Bili hivi viwili kufanyiwa kazi uchakachuaji hautaisha kamwe
   
 2. c

  carmsigwa Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :tape:Hatuhitaji kuongea tunahitaji kutekeleza, saa ya ukombozi ni sasa hatuwezi kukubali nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 iamuliwe mambo yao na kikundi cha watu wasiozidi milioni 1.Mabadiriko ya katiba ni lazima angalia uchafu unao jitokeza kwenye katiba ya jamhuri haitambui serikali ya umoja wakitaifa wakati Tanzania visiwani hilo linatambulika, chama kinacho ongoza visiwani ndio hicho hicho kinacho ongoza jamhuri hivi unahitaji elimu yanamna gani kujua uchafu huu.
   
Loading...