Katiba mpya: Kikwete anachezea moto wa baadaye

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,709
... ambao waliujadili muswada huo na kuupitisha. Wangeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani.” Jakaya Kikwete.
Hii maana yake ni kwamba wabunge ni bora kuliko wananchi ambao ni wenye nchi? Wanaomshauri mwanangu Kikwete mbona wanazidi kumjengea historia chafu baadaye?
Angalia kituo kingine cha mwanangu Kikwete.

Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania, kwa ndugu wa marehemu wetu hao,”
Je wananchi wanahitaji rambi rambi au huduma? Je haya ndiyo maisha bora kwa watanzania wote aliyoahidi Kikwete?
“Nashukuru kwamba amani na utulivu vimerejea katika Manispaa ya Songea, nawapongeza viongozi wa ngazi zote na wananchi kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwezesha amani kupatikana,”
Kwa Kikwete waliokufa hawana thamani kwa vile walikuwa wakiandamana. Je hii ndiyo amani na mshikamano tunavyosikia Kikwete na wenzake wakiimba kila uchao?
Mnaipeleka wapi nchi yetu? Je mnajua kuna kesho na mambo hubadilika?
 
  • Thanks
Reactions: lum
Back
Top Bottom