KATIBA MPYA: Katiba ni Sheria Mama-Mchakato wa Kuandika Uongozwe na Sheria!!!!!!!!!!

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
Baada ya rais Kikwete kutamka ridhaa yake katika hotuba yake kwa taifa siku ya Ijumaa 31.12.2010, kuruhusu kuandikwa katiba mpya,na baada ya kuonekana wazi kwamba hoja ya kuandikwa katiba mpya sasa ni muafaka wa kitaifa; mimi nashawishika kuamini kwamba ya muhimu kufuata baada ya muafaka huu ni haya yafuatayo_;
1) Muafaka huu hauna budi upate nguvu ya sheria kwa bunge kuutungia sheria ya kuweka ridhaa hii kuwa muafaka wakisheria wa kitaifa; Siamini kwamba katika hatua hii, kama atakuwapo spika ama wabunge wa chama fulani chenye wabunge wengi bungeni kukwamisha jambo hili; hapa la msingi ni nguvu ya hoja yenye maslahi kwa taifa;
2) Sheria hiyo itaweka uhai wa kisheria na kutamka bayana njia zipi muafaka zitatumika kupata (a) Hadidu za reiea,yaani Terms of Reference, kuelekeza mambo ya kufanya, time frame, nk (b) Muundo wa chombo cha kusimamia (steering), (c) Muundo wa chombo cha kuhusisha wadau wote katika sekta zote za jamii, na hatimaye, kura ya maoni, na mwisho muswada kuwa sheria;
3) Nimempongeza rais Kikwete kwa kukubali kuandikwa katiba mpya, na kumwomba atumie bunge kusimamia mchakato,lakini naongeza angalizo kwamba njia anayoelekea kufuata inaondoa dhana nzima ya utashi wa kisiasa katika jambo hili lenye maslahi ya uhai wa taifa hili; dosari kubwa ninayoona ni kwamba bila taifa kuwa na nguvu ya sheria ya muafaka huu, njia gani yenye nguvu za kisheria itafuatwa kuongoza mchakato????; mpaka sasa inaonekana ni hisani ya Kikwete ndiyo inatawala-kile anachotaka ndicho kitafanyika, au la ndiyo basi!! Namna hii kweli kutafanyika kitu kabla ya 2015?????? Naaona giza totoro!!!!!!!!!!!
4) Kama ilivyokuwa kwa sheria ya uchaguzi ya mwaka jana wa 2010, walau kulikuwa na nguvu ya sheria, hata kama utekelezaji wake ulitawaliwa na uchakachuaji mwingi;
5) Bunge kama mhimili mtunga sheria zote katika nchi hii, kutokuipa nafasi ya kushiriki na kupata elimu ya kutosha toka mwanzo juu ya hoja hii ya msingi kwa uhai wa taifa hili ni kutoa nafasi ya athari za wazi huko mbeleni; kutanguliza dhana kwamba wapo wabunge wa chama fulani watakaokwamisha hoja hii katika hatua ambayo imekwishafikia si busara!!; mimi binafsi ninaamini wanaopinga hoja hii ni wachache wenye maslahi ya kifisadi-hawa siyo tishio kwa sabau siyo wengi bungeni; Inawezekana zaidi ya 70% ya wabunge wa sasa ni leimen katika hoja hii, lakini wakielimika watakuwa support kubwa sana!!!!;
6) Watanzania wa sekta zote wadau tukubali kuongozwa na hekima zaidi ya jazba na msisimko katika suala hili ambalo ni la kuweka uhai mpya ndani ya taifa letu!!!!; tusikubali kirahisi kuyumbishwa na makundi yenye maslahi za siri, vinginevyo ipo hatari ya taifa hili kusambaratika kama Urusi ya Soviet Union ya Yelsin!!!!!!!!!;
 
Back
Top Bottom