Katiba mpya itawafikia wenzetu vijijini?

Kanjunju

Member
Oct 8, 2010
92
6
Swali langu kwenu wana jf ni juu ya hii katiba kweli itawafikia mama zetu kule vijijini ili waweze kuona faida ya katiba mpya?kimsingi nimejifunza kitu tokea huu mchakato uanze ni watu wa mjini tu wanaozungumzia katiba lakini vijijin watu bado hawaelewi juu ya hilo.sasa tufanyeje kuwasaidia waliopo vijijini kutambua haki zao?
 
kwanza mchakato huo wa katiba umefikia wapi? mbona naona kimya na siskii muendelezo wa mchakato mzima wa katiba hiyo?
 
Mwandishi wa thread nadhani alikuwa anauliza kama mchakato wa kuunda katiba mpya utafika vijijini?

hapo nimeelewa. Nafikiri hata kwa mjini sidhani kama huo mchakato utafanywa na watu wengi.
Vijijini watashiriki kwa kupeleka maoni yao kwa wabunge wao.
 
Lazima tuchemshe bongo zetu tuone ni vipi elimu ya uraia-katiba itafikishwa hadi vitongojini ili wa-Tanzania wote waelewe, wajadili na kisha wachangie katiba wanayoitaka. Jadili Katiba Tanzania programme ni mradi umebuniwa na Tanzania Gender Accountability (TAGA); Women and Law East Africa-Tanzania na Rights Action Watch, kupeleka elimu ya katiba vitongojini ikiwanlenga wanawake na vijana. Kuwafikia wakina mama vijijini kunahitaji hatua zaidi ya kugawa nakala za Katiba ya sasa. Hapa jukwaani tumeonge sana na wengi wetu tumeelimika kiasi kwamba tukiulizwa tunataka nini kiwemo kwenye katiba mpya, na mchakato uwe vipi, tunaweza kusema kwa uhakika. Inabidi sisi wote tunaochangia humu kila mmoja achukue hatua ya kuto elimu ya katiba kwa ndugu, marafiki na jamaa zetu vijijini na mijini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom