Katiba mpya iruhusu maraisi wastaafu kushitakiwa:

Kimboko

Member
Nov 16, 2010
56
6
Ndugu zangu hii sasa inasikitisha sana.

Wakati wa nyerere waziri yoyote akiboronga anastaafishwa kwa manufaa ya umma, leo waziri akiborongo wizara hii anahamishiwa wizara nyingine.

Kwa nini kubebana huku tusikumalize kwa kuweka mikakati kwenye katiba mpya kwamba Raisi au waziri akifanya makosa yoyote akiwa madarakani ashugulikiwe na vyombo husika kama watu wengine siyo wanapelekwa watu chambo tu kama kina Mramba na Yona ili kuwapa wananchi matumaini kumbe hamna lolote ni changa la macho tu.

Hili mnalionaje wadau wa kurekebisha katiba maana hii siyo katiba mpya ni maboresho ya katiba ya zamani.
 
umenena....mm nitaanza kumshtaki, nyerere, mkapa na kikwete, halafu ndio kina lowasa na wengineo weeeeeengi tu
 
Mi nakubali hoja 100%, kwa rais ashitakiwe baada ya kumaliza muda wake, maana akifikishwa mahakamani akiwa madarakani inaweza kuyumbisha nch na pia kwa kuepusha kupandikiza mtu wake ili baadae asimshitaki katiba iongeze ziada kuwa mtu akiwa rais haruhusiwi kushika vyeo vikubwa kwenye chama chake km ukatibu mkuu au uenyekiti, na kwa upande wa waziri akizingua on the spot anastahafishwa then mahakamani
 
Ninakuunga mkono kwa asilimia 95. Vile vile wasipewe marupurupu kwa vile wanaiba sana mali za watanzania. Pensheni zao zitokane na makato ya mishahara yao kama wafanyakazi wengine wa umma!
 
Back
Top Bottom