Katiba mpya iharakishwe - Jaji Ramadhan

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Katiba mpya iharakishwe - Jaji Ramadhan Monday, 27 December 2010 19:58

Elias Sichalwe

JAJI Mkuu anayemaliza muda wake, Agustino Ramadhan amezungumzia tena umuhimu wa kuandikwa kwa katiba mpya, safari hii akitaka uundwaji wake uharakishwe ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi.

Ramadhan alishawahi kukaririwa akisema kuwa suala la katiba mpya linazungumzika, akiungana na wanasiasa wa kada mbalimbali, wanasheria na wanaharakati ambao walieleza kuwa suala hilo sasa haliepukiki.

Jana, Jaji Ramadhan, ambaye ameshamaliza muda wake, alikiambia Kituo cha Televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na katiba mpya. “Kuna umuhimu wa kubadilisha katiba ya nchi yetu ili kuondoa upungufu uliopo katika katiba ya sasa ambayo inalalamikiwa na wengi,|” alisema jaji Ramadhan.

Jaji Ramadhan alitoa mfano wa upungufu uliopo kwenye muda wa kustaafu wa jaji mkuu na majaji wengine akisema ni moja ya mambo yanayoweza kuangaliwa wakati wa kuandika katiba mpya. "Katiba inasema Jaji Mkuu atastaafu kwenye muda wanaostaafu majaji wengine. Muda huo ni miaka 65, huu unaweza kuwa upungufu mwingine kwenye katiba," alisema.

Kwa mujibu wa Jaji Radhaman, katiba ya sasa ina upungufu mkubwa ambao hauna budi kuangaliwa kwa jicho la kuusahihisha kwa maslahi ya Watanzania.

Jaji Ramadhan alisema kuna umuhimu wa kubadilisha katiba ili kukidhi mapungufu yaliyojitokeza katika katiba ya awali.
Suala la mabadiliko au kuandikwa katiba mpya limezungumziwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu.

Baadhi ya viongozi hao ni Rais wa Serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na majaji kadhaa ambao walishazungumzia umuhimu wa katiba mpya. Lakini msisitizo mkubwa uliwekwa na msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya, akitoa mfano wa mapungufu ya katiba ya sasa kuwa ni rais kupewa madaraka makubwa.
 
Hawa viongozi wa TZ hawaachi kunishangaza......yaani wakiisha kutoka madarakani ndiyo utawasikia wakipiga baragumu la kutetea haki lakini walipokuwa madarakani aidha walitetea udhalimu au walikaa kimya kama vile hawauoni yote hayo waliyafanya kwa minajili ya kulinda ugali wao wa wakati ule.............
 
Hawa viongozi wa TZ hawaachi kunishangaza......yaani wakiisha kutoka madarakani ndiyo utawasikia wakipiga baragumu la kutetea haki lakini walipokuwa madarakani aidha walitetea udhalimu au walikaa kimya kama vile hawauoni yote hayo waliyafanya kwa minajili ya kulinda ugali wao wa wakati ule.............


Wala usisikitike jumla jumla kwa yote hayo. Nako pia ndani ya lugha hiyo ya mwili wao kuna ujumbe MKUBWA sana kwetu wananchi kuusikiliza na kuufanyia kazi.

Ujumbe huo wa kimwili ni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hao viongozi wetu kunyamaza jii wawapo madarakani hata pale ambapo wanao wajibu wa kuzungumzia jambo kwa maslahi ya Umma wa Tanzania, lazima kuna 'MDUDU WA AJABU SANA' huwa anawakalia mgongoni kila waendako na kudhibiti kila wasemalo.

Sasa, nielewavyo mimi, kutafuta majibu juu ya hako 'ka-mdudu' sifa zake, maisha yake, mema,mabaya na mambo kama hayo ni kazi ya hii Forum ya 'Great Thinkers' kuyatafutia jawabu. Kwa KATIBA MPYA hako 'ka-Mdudu' kanaweza kufanywa awe rafiki wa mawazo huru????


Hebu tuanzie hapo, Ni 'mdudu' gani ambayo huwa unawatisha viongozi wetu wawapo madarakani hata wasiweze kuzungumza mawazo yao huru ilhali wanayo???
 
"Katiba inasema Jaji Mkuu atastaafu kwenye muda wanaostaafu majaji wengine. Muda huo ni miaka 65, huu unaweza kuwa upungufu mwingine kwenye katiba,"
sijakielewa hiki ki babu, yani kilichomuua yeye ni kwamba Katiba imem force aachie ngazi, au ana maana gani? Mbona hii ni self-serving concern? Na mbona hakusema mapungufu ya hiyo Katiba kabla hajastaafu?
 
Ni mnafiki mkubwa... he was supposed to push for it while in position, amenikera sana huyu baba

naona ile laana ya anglican zanzibar itammaliza
 
jaji ramadhani amenena -katiba mpya ndio suluhisho angalau ameongea je asingeongea??? ni kweli kuna mdudu anakuwa mgongoni kwao kuchunguza wanachosema -ukikaa vibaya mdudu anaweza kukutoa pumuzi ndio mana wanaogopa.
 
Lakini Ramadhani amesikika akisema waziwazi kuunga mkono malalamiko ya wananchi kuhusu katiba, kwa kuwa moto unaongezeka kasi na yeye anaachia ngazi, ameongelea masuala hayo mchana kweupe na hapo sio unafiki. Mnafiki ni Werema ambaye anadhani hawezi kuishi bila kusema ukweli bali kutetea uozo kuwafurahisha waajiri wake.
 
Back
Top Bottom