HISIA KALI
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 694
- 108
Rais Kikwete una kazi kubwa mbele yako. Uwe makini katika hili. Soma alama za nyakati.
Zaidi ya CDM hakuna chama kingine chochote kilichoomba kukutana na JK. Leo hii inakuwaje vilazimishiwe kwenda kuonana nae wakati hawakuwa hata wameandaa ajenda ambayo ingehitaji msaada wa JK! Kweli CCM ni Janga la Kitaifa.
Hii ya CCM ni sawa na kumuona jamaa anaelekea Ubungo ukamfuata wakati wewe ulikuwa huna mpango wa kwenda huko. Chadema ina sababu zake wanapinga mswada kusainiwa sasa CCM au CUF watakwenda na hoja gani, kama hoja yao ni kupinga sawa waunganishe hoja waende pamoja lakini kama wana hoja tofauti na Chadema waombe siku nyingine wakutane na rais hawakatazwi. Hii ni sawa na fujo za kisiasa, halafu toka lini CCM akawa masemaji wa vyama vingine?Hivi hoja walizonazo CHADEMA kukutana na JK ndio hoja za hivyo vyama vingine CCM wanaoshinikiza wahusishwe?
Hii michezo ya Kitoto CCM wanayofanya ishapitwa na wakati kama CCM wanataka na hivyo vyama vingine vishiriki pamoja waombe miadi na JK na sio kukurupuka eti kisa CDM... CCM wasipotumia busara huu mchakato katiba mpya itakuwa vurugu tupu..
Chonde chonde viongozi wa Chadema – katika mkutano wenu na JK kuhusu Katiba mpya, kamwe msikubali ujumuishe vyama vingine kama ilivyopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM (CC) kwa Rais Kikwete.
Ni vyema kila chama kikakutana na JK peke yake.
Hofu yangu ni kwamba pendekezo hili limetolewa ili kumsaidia JK kukabiliana na hoja za viongozi wa Chadema wtakaokwenda kukutana naye. Wajumbe wa CUF watakaokwenda, ambacho ni chama mshiriki wa CCM huko Zanzibar, wanaweza kuvuruga mkutano huo ukiwa wa pamoja na Chadema ikaonekana haina hoja.
Nasema hivyo kwa sababu tayari CCM inaonekana kuufanya Muungano kuwa ni mtaji wake mkubwa wa kisiasa katika suala la Katiba mpya kwa kuwapa Zanzibar uwakilishi sawa jambo ambalo CDM inalipinga kwa sababu ya kutokuwap pia kwa serikali ya "Tanganyika" katika Muungano.
Ingekuwapo serikali hiyo ya Tanganyika, uwakilishi wa namna hiyo ungekubalika na CDM.
Msifanye makosa CDM kujijumlisha na vyama vingine katika mkutano na JK – na hasa CUF – maana hawa CUF wako zaidi kwa masilahi ya Zanzibar na CCM.
Natoa tahadhari.
Mkuu katika hayo majadiliano kuna pande mbili tu,moja ni ya CDM na nyingine ni JK na hao 'wageni', wake bila hivyo CDM ni bora wafikirie strategy nyingine hiyo ya kukukutana nae waachane nayo..IIe ya kukutana, mwenyeji (JK) akaamua kuwa na wageni wake wengine wowote kuwalaki wageni wake rasmi Chadema!. Hao wageni wengine wanaweza kuwa CUF, NCCR Mageuzi, UDP na TLP!.
Vingine vimeshajadili na kupitisha maoni yao sasa viende kufanya nini wakati vilikubali kusoma muswada kwa mara ya pili ikimaanisha kuwa haviitaji mjadala zaidi. Hapo ni wabunge wa NCCR na chama cha Chadema. NCCR bado kama chama hakieleweki maana mpaka sasa hamna msimamo wa wazi wa chama, hata kutoka walitoka kwa utashi wa mtu mmoja mmoja sio chama mwanzoni walitoka wabunge wote wa chadema na wawili wa nccr kafulila na mkosamali. machali na yule mwanamke walibaki mpaka kesho yake waliposoma upepo.Kama suala ni kujadili katiba kwa nini vyama vyote visikutane pamoja kuliko kwenda kimojakimoja? acheni ubaguzi, THIS IS NOT A ONE MAN SHOW!
Well said, lakini kuhusu mkosamali nadhani asiwe pekeyake maana nccr wote walipinga bila kificho kwa hiyo wana sababu ya kuonana na rais. kama watatakiwa kuwakilishwa basi wanaweza wakamchagua yeyote kati yao wanne.Watanzania Tuwe wazalendo kwa Nchi yetu. Kwa nia njema, CUF wasi husishwe katika mkutano huo, watalaamu wa sheria ambao pia wamo katika Kamati ya Katiba Hasa Felix Mkosamali ( mb) NCCR MAGEUZI wahusishwe kwani walionekana kupinga mswaada huu mbovu tangu kwenye kamati na Hata kutoka Bungeni.