Katiba Mpya: CHADEMA msikubali mkutano wenu na JK kuhusisha vyama vingine, hasa CUF

Hivi hoja walizonazo CDM kukutana na JK ndio hoja za hivyo vyama vingine CCM wanaoshinikiza wahusishwe? hii michezo ya Kitoto CCM wanayofanya ishapitwa na wakati kama CCM wanataka na hivyo vyama vingine vishiriki pamoja waombe miadi na JK na sio kukurupuka eti kisa CDM..CCM wasipotumia busara huu mchakato katiba mpya itakuwa vurugu tupu..

Yaani it is ridiculous and disgusting, yaani eti CCM ndiyo imekuwa msemajiwa vyama pinzani. Maana hao wengine hawajaona umuhimu wa kuonana na JK, lakini CCM inawaombea kweli bongo tambarareeeeeeeeee!!!!!!!
 
Wewe KAMURA...

Kwa taarifa yako 70% ya WATANGANYIKA WANAITAKA NCHI YAO, TAIFA LA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI,SIO HILI LA MAGAMBA MAFISADI NA WAWEKEZAJI.. na ni CDM pekee ndio mkombozi anayebeba dhamana ya 70% ya wanaoitaka TANGANYIKA YAO, Iweje waungane na wale waliokuwa wanawabeza kule mjengoni? CCM & WAKE ZAKE wao wamepitisha sasa wakutane kwa hoja zipi?

Mlibeza MAGAMBA hatua ya MAKAMANDA kumuona JK MCHINA,Iweje leo muuone umuhimu wa huo mkutano? ACHANENI NA CDM KAMA ILIVYO, MSITUINGILIE KABISA MMELIANZISHA KUJIVUA GAMBA MAGAMBA YAMEGANDIA HAYAVULIKI,MNADANDIA YACYO WAHUSU...MALIZENI YENU NA UNAFIKI WENU
 
Hapo kwenye red (well said) - maelezo haya hapa chini nimeyaweka kwenye post nyingine

Kukutana na vyama vyote??? - Ili CCM na CUF wakapigilie msumari kuwa mchakato ni sahihi na vyama vingine kama TLP vikapokee posho na kuunga mkono hoja ya CCM na CUF. Hivyo wakija kuhesabu kura (si hoja) itaonekana ni CHADEMA tu ndiyo inayopinga huo mchakato. Magamba kwa faulo hawajambo!!!

Hata mimi nina maoni hayohayo sababu nao wakijumuika watadhoofisha kikao hicho
 
Kwa maoni yangu tayari CDM imeshajenga public image kuwa we dont only resort to vurugu. Hivyo hakuna sababu yoyot ya kukubali kudhalilishwa na jK. Suala hili litaleta mgogoro cdm.
 
Mkuu -- Nakuunga mkono 100 asilimia. Kila chama kiende kwa JK kivyake!
Zaidi ya CDM hakuna chama kingine chochote kilichoomba kukutana na JK. Leo hii inakuwaje vilazimishiwe kwenda kuonana nae wakati hawakuwa hata wameandaa ajenda ambayo ingehitaji msaada wa JK! Kweli CCM ni Janga la Kitaifa.
 
Hizo sarakasi za CCM, CDM wasizikubali kabisa maana nia yao ni kuvuruga maana wanajua CDM hawawezi kukubali tikitaka zao. Kama alivyosema mchangiaji mmoja CHADEMA MSIKUBALI KUSHIRIKI KIKAO NA JK MKIWA NA VYAMA VINGINE.
 
Zaidi ya CDM hakuna chama kingine chochote kilichoomba kukutana na JK. Leo hii inakuwaje vilazimishiwe kwenda kuonana nae wakati hawakuwa hata wameandaa ajenda ambayo ingehitaji msaada wa JK! Kweli CCM ni Janga la Kitaifa.

MJINGA HUTAWALIWA MWEREVU HUONGOZWA.....acha WAJINGA watawaliwe kwani JK ORIGINAL ALIPINGA SANA UJINGA... Lakini inashangaza leo tunaingia Miaka 50 tungali na MIJINGA MINGI.. DAWA NI BAKORA TU,watanyooka hawa..
 
Hawa watu walitofautiana Dodoma. CDM wakaanzisha hoja ya kukutana na JK. Sasa hawa wengine wanaenda kukutana na JK ili wakazungumze nini? Nini hoja yao? Ya CDM iko wazi.

Huu ni uhatarishaji wa makusudi wa amani ya nchi. Unajua CCM have nothing to loose on this agenda because they already know that they are exiting the leadership of the country. Hamuoni hata kwenye vikao vyao vya juu hoja ni CDM? Hamshangai chama kisicho na hoja zaidi ya kujadili wengine. Ukishaona taasisi imeacha kushughulikia mambo ya msingi bali kujadili watu basi ujue taasisi hiyo haina ajenda. Utagundua kuwa sasa wameacha kabisa kushughulikia magamba yao magumu mwilini wanashughulikia CDM. Wameacha kushughulikia uchumi wa nchi, sasa hoja ni kupinga maandamano ya CDM...wamekwisha!!!!! Hawajui jinsi wanavyozidi kutumia nguvu kuipinga CDM ndivyo umaarufu wa CDM Unavyozidi kupaa.

Hongera Magamba kwa kujichimbia kaburi wenyewe!
 
Wake up wele woote wanaoitakia mema nchi hii,ni dhahiri kikao cha MAGAMBA huko DOM ni kupanga mikakati namna ya kuiangusha CDM TU, Thats y wanaanza kuingilia mambo ya CDM wakiwa ktk mikutano yao....CDM Wabunge 23, wafuasi 30 milion... MAGAMBA HAMUIWEZI CDM,.
CDM JUU JUU ZAIDI...
 
Nani amewapumbaza watz,nani amewapa upofu watz,nani amewafanya watz kuwa wanyonge na watu wa kuonewa tu,nani kawaloga watu hawa,nani basi atoke na kusimama aseme yatosha basi.

Nani watz watamsikiliza atakaposema sasa watu wote tuseme inatosha, sasa basi, tuanze upya, upya enzi zile viongozi wanajiuzuru kwa rushwa,wanafungwa kwa ubathilifu,,,,nani?
 
Mi naomba cdm wawe waangalifu sana na vinywaji na vyakula hapo ikulu, CCM mafia wanaweza kuwafanya kama mwandosya na mwakyembe, tunawahitaji sana, tafadharini sana.
 
Chonde chonde viongozi wa Chadema – katika mkutano wenu na JK kuhusu Katiba mpya, kamwe msikubali ujumuishe vyama vingine kama ilivyopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM (CC) kwa Rais Kikwete. Ni vyema kila chama kikakutana na JK peke yake.

Hofu yangu ni kwamba pendekezo hili limetolewa ili kumsaidia JK kukabiliana na hoja za viongozi wa Chadema wtakaokwenda kukutana naye. Wajumbe wa CUF watakaokwenda, ambacho ni chama mshiriki wa CCM huko Zanzibar, wanaweza kuvuruga mkutano huo ukiwa wa pamoja na Chadema ikaonekana haina hoja.

Nasema hivyo kwa sababu tayari CCM inaonekana kuufanya Muungano kuwa ni mtaji wake mkubwa wa kisiasa katika suala la Katiba mpya kwa kuwapa Zanzibar uwakilishi sawa jambo ambalo CDM inalipinga kwa sababu ya kutokuwap pia kwa serikali ya "Tanganyika" katika Muungano.

Ingekuwapo serikali hiyo ya Tanganyika, uwakilishi wa namna hiyo ungekubalika na CDM.

Msifanye makosa CDM kujijumlisha na vyama vingine katika mkutano na JK – na hasa CUF – maana hawa CUF wako zaidi kwa masilahi ya Zanzibar na CCM.

Natoa tahadhari.
Kafiribangi,
"Beggars can not be chooses!", in this case Chadema are the beggars, they can neither choose or dictate terms!.
Kwa vile aliyekubali kukutana nao ni JK, atakapowatumia barua rasmi ya kukubali, anaweza kuwapa masharti ikiwemo ya kumtambua rasmi yeye kama rais, au asiwape masharti yoyote, ili kuwabembeleza wasije kususa!, ila siku ya siku.

IIe ya kukutana, mwenyeji (JK) akaamua kuwa na wageni wake wengine wowote kuwalaki wageni wake rasmi Chadema!. Hao wageni wengine wanaweza kuwa CUF, NCCR Mageuzi, UDP na TLP!.
 
Nyote vilaza mabongo lala msio na fikira.kwanini cuf isishiriki eti ccm b. Hiyo katiba itakuwa ni cdm, siku zote mvumbuzi ni mmoja lakini.hutokea wengine kupitia hicho.

CUF ni watanzania kina wabunge na madiwani na wenyeviti wa mitaa wengi kuliko hata cdm, cuf ni chama cha pili kuwa na wenyeviti wa mtaa wengi baada ya ccm.

Vyama vyote ni muhimu vishiriki kwani vina watu wengi nyuma. We jamaa kilaza halaf unaonekana mbaguzi. Toa pumba hapa maswala ya kitaifa cdm peke waongee kweli m.atako yanafikiri kama yamelewa
 
CHADEMA daima kitaongoza na wengine watafuata

Kimsingi CCM nao wanataka kuingia kwenye msafara,lakini hawajaomba rasmi,nashauri CHADEMA waende kivyao kwa sab tayari wana hoja mezani


Hivi vyama vingine bado havijaomba,wana haki ya kufanya hivyo,tatizo watakuwa na hoja?
 
Ni vizuri tujiandae kwa kila jambo litakalo tokea kwa maana hapa Tanzania kila jambo linaweza kutokea, hasa maamuzi ya kipuuzi. CDM waliomba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na sio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi. Vile vile CDM hakikuomba kwa niaba ya vyama vingine. Kwa maana kuwa katika utaratibu wa kutunga sheria mara baada ya mswada kupitishwa na Bunge,ili iwe sheria; Rais wa Jamhuri ni lazima akubali kwa kuweka sahihi yake. CDM kama chama, kinataka kumuonyesha mambo ya msingi ambayo yanaweza kumsaidia rais kuamua kutoweka sahihi yake na kuagiza hatua kadha wa kadha kuchukuliwa ili kuliwezesha taifa kuwa na mchakato madhubuti utakaowezesha kupata katiba bora.

Busara ya kawaida inamshinikiza Rais kushauriana na CDM kama kuna haja ya kuvishirikisha vyama vingine katika mkutano wao au la? CDM ndiyo inayoweza kuomba tena Rais kuwa katika hili wanakaribisha uwepo wa NCCR kwa kuzingatia kuwa katika hili chama cha NCCR kiliunga mkono msimamo wa CDM, uamuzi uliotoa picha sahihi kuwa ipo hoja ya msingi katika madai ya CDM.

Vyama kama TLP na UDP hawana hoja yeyote katika suala hili maana wanakubaliana naye ( rais na wabunge wake). Ingeeleweka kama vyama hivi vingekuwa upande wa rais katika mjadala huu dhidi ya CDM na NCCR.

Nafasi kama hii ikitolewa kwa msingi huu, hakuna haja kuikataa, lakini kama nia ni uvurugaji na upotoshaji, nadhani hakuna haja, umma uandaliwe kuchukua hatua na zamu hii tuunge mkono kidhati na sio kusemea kwenye jukwaa hili.

Naunga mkono hoja.
 
Tatitizo la CCM hawaamini kuwa CDM ni chama cha UPINZANI ndiyo maana wanawachukulia ki simple tu
Hapana Jk alikuwa tayari kukutana cdm peke yao hawa cc ndio wametoa wazo la vyama vingine viwepo hawajasema tu lkn naamini walitaka hasa cuf ndio wawepo,kinachonisikitisha ni kwamba naona km cc hawamuamini jk maana hawajui hasa cdm wanakwenda kuongea nini na wanaamini kwa hoja za cdm mkulu aweza badili mawazo, cc muacheni jk akutane na cdm kwani ht yeye aliridhia kwa moyo mweupe kukutana nao, vyama vingine nanyi tumieni busara hii ngoma c yenu msije kujipeleka ht mkiambiwa muende.
 
Ni vizuri tujiandae kwa kila jambo litakalo tokea kwa maana hapa Tanzania kila jambo linaweza kutokea, hasa maamuzi ya kipuuzi. CDM waliomba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na sio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi. Vile vile CDM hakikuomba kwa niaba ya vyama vingine. Kwa maana kuwa katika utaratibu wa kutunga sheria mara baada ya mswada kupitishwa na Bunge,ili iwe sheria; Rais wa Jamhuri ni lazima akubali kwa kuweka sahihi yake. CDM kama chama, kinataka kumuonyesha mambo ya msingi ambayo yanaweza kumsaidia rais kuamua kutoweka sahihi yake na kuagiza hatua kadha wa kadha kuchukuliwa ili kuliwezesha taifa kuwa na mchakato madhubuti utakaowezesha kupata katiba bora.

Busara ya kawaida inamshinikiza Rais kushauriana na CDM kama kuna haja ya kuvishirikisha vyama vingine katika mkutano wao au la? CDM ndiyo inayoweza kuomba tena Rais kuwa katika hili wanakaribisha uwepo wa NCCR kwa kuzingatia kuwa katika hili chama cha NCCR kiliunga mkono msimamo wa CDM, uamuzi uliotoa picha sahihi kuwa ipo hoja ya msingi katika madai ya CDM.

Vyama kama TLP na UDP hawana hoja yeyote katika suala hili maana wanakubaliana naye ( rais na wabunge wake). Ingeeleweka kama vyama hivi vingekuwa upande wa rais katika mjadala huu dhidi ya CDM na NCCR.

Nafasi kama hii ikitolewa kwa msingi huu, hakuna haja kuikataa, lakini kama nia ni uvurugaji na upotoshaji, nadhani hakuna haja, umma uandaliwe kuchukua hatua na zamu hii tuunge mkono kidhati na sio kusemea kwenye jukwaa hili.

Naunga mkono hoja.
 
Nukuu ya habari kutoka gazeti la mwananchi

''KAMATI Kuu (CC) ya CCM, imemwagiza Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akutane na vyama vyote vya siasa badala Chadema peke yake.

Kamati hiyo imesema ni muhimu hatua hiyo ya kuzungumzia muswada wa Katiba ikafanywa kwa umakini mkubwa kwa kuwa jambo hilo, linawagusa Watanzania wengi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana Mjini Dodoma kuwa Muswada wa Marekebisho ya Katiba ni moja ya mambo yaliyojadiliwa kwa kina katika kikao hicho cha Kamati Kuu.

Agizo la chama hicho limekuja baada ya Rais Kikwete kupokea na kukubali ombi la Chadema la kukutana naye ili kujadili suala la Katiba.

Chama kimempongeza mwenyekiti kwa hotuba yake nzuri kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Pamoja na kukubali akutane na Chadema, tumetahadharisha kuwa lazima kushirikisha na wajumbe wengine kutoka vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe Chadema pekee,'' alisema Nape.

Alisema CCM kinaamini kuwa njia ya majadiliano waliyoitumia Chadema katika kutafuta haki ni nzuri na fursa hiyo ikitumiwa vizuri, inaweza kuleta maelewano mazuri na faida kwa jamii''

Mwisho wa nukuu

Mimi nashangaa sana na hoja hii ya CCM kuwa vyama vingine vyote navyo vikutane na rais Kikwete. CHADEMA hawakubaliane na sheria ya utaratibu wa kupata katiba mpya ambao iliwakilishwa bunge na hatimaye pitishwa na wabunge wote CCM, CUF, TLP, na UDP.

Sasa kama wabunge wa hivi vyama walishapitisha hiyo sheria tena kwa nderemo na vigelegele sasa wanataka kujadili nini? Wao wasubiri tu Rais Kikwete asaini hiyo sheria maana walishamaliza kazi yao bungeni. Walivyoambia kuwa sheria hiyo ina matatizo makubwa hawakusikia.

CHADEMA wao wameona kuna matatizo makubwa ndio maana walipinga tangu mwanzoni na sasa wanataka kwenda kuongea na rais Kikwete ambaye ndiye pekee katiba ya sasa inampa mamlaka ya kusaini hiyo sheria na kuanza kutumika rasmi.

Hawa wa vyama vingine walishapitisha hiyo sheria bungeni na kufanya hivyo ina maana walishamwambia rais Kikwete atie sahihi hiyo sheria kwani kwao haina tatizo lolote. Sasa kama walishafanya hivyo hii CCM inataka nao waende kwenye mazungumzo na Rais Kikwete sasa mimi nashindwa kuelewa wataende kumwambia kitu gani Rais Kikwete tofauti na walichopisha bungeni?

Labda wanataka kwenda kumwambia kuwa asaini hiyo sheria jinsi ilivyo kitu ambacho itakuwa ni kurudia kile walichokwisha fanya tayari.

Halafu kikubwa sana cha kushangaza ni haya maneno kuwa vyama ni lazima kushirikisha na wajumbe wengine kutoka vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe Chadema pekee. Sasa mimi najiuliza ina maana hata CCM nao wanataka kushirikishwa kwenye haya mazungumzo?

 
Back
Top Bottom