Katiba haimtambui JK kwa hiyo CHADEMA wana haki ya kutomtambua kwa mujibu wa katiba

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Hebu angalieni ibara ya 41 katika katiba ya nchi kipengele cha 6 na 7 vinakinzana mwaka huu
41. (6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
:sad:
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Katiba imelazimishwa kumtambua Jk.. Maana hata na yenyewe inamtambua raisi aliyetokana na wananchi na si vinginevyo... JK hayuko pale kwa mujibu wa sheria bali de facto(kwa kutumia nguvu na kubaka demokrasia)...
CHADEMA wana haki ya kutambua baadhi ya matokeo ya ubunge ndio maana mengine yako mahakamani tayari... Mimi nadhani kipengele cha kutotambua matokeo ya uraisi ndio kero hapa kifutwe halafu mengine tutaongea baadae...
Kule jamaa wanachakachua lakini muhimili mmoja yaani serikali wamebaka mamlaka ya mahakama kwa kusema matokeo ya uraisi hayawezi kupelekwa mahakamani<ibara ya 41(7)>...
Mimi nashauri siku raisi anasoma hotuba pale bungeni ni lazma CHADEMA watoke kuonyesha nia yao ya dhati... Lakini kama watakuwepo basi lazma watakuwa na njia yao mbadala ya kukataa haya matokeo kama walivyodai watatupa msimamo mzima wa ligi ulivyokuwa na kilichotokea...

Watu wengi hawaelewi maana ya mtu anaposema hamtambui raisi maana wengine wanafikiri anakiuka sheria ya treason... Lakini La hasha CHADEMA wamekuwa wastaarabu saana maana maeneo mengine watu walishaanza kutembea barabarani kudai haki tumeona Shinyanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma ujiji kusema kwelli CHADEMA wametumia utaratib mzuri sana na kufuta ile dhana ya kuwa wanapenda fujo... Huu ni ustaarabu mwenye akili atafikiri ila aliyenyimwa akaombewe tuu!!!

Nawasilisha hoja
 
eliesikia hapo nimekupata sana.na naungana na wewe kwamba chadema wamekuwa wastaarabu saana maana haya matokeo ya uraisi ingekuwa ni nchi jirani ingekuwa mpaka leo ngumi zinapgwa lakini chadema sii wafujo ndo maana hawakuchochea fujo otherwise pasingekalikahapa so CHADEMA ina kila sbb ya kupongezwa! lakini kilichopo wangetulia tu na kuanza kujipanga zaidi ili 2015 sisiemu ipigwe chini! ila wakipoteza muda kupinga matokeo watajikuta wamebakia huko huko na hapo ndo sisiemu itawapigia cha kisigino! ni mtazamo tu!
 
Watanzania wengi wenye uzalendo wa kweli kama Dkt (phD) Slaa wanaamini kwa dhati kuwa kuna sintofahamu kubwa katika htimisho la kura za urais zilizomtangaza JK kama Rais wa JMT. But tulio wengi bado twasubiri tamko rasmi la CHADEMA ili taifa lijue na liishi na ukweli wakati tukijiandaa na mabadiliko makubwa 2015. Wito wangu kwa Dkt Slaa na CHADEMA epukeni mbinu zozote za kuwazuia kuueleza umma ukweli halisi wa kilichotokea 2010. Hii itasaidia kujua nini cha kufanya mbeleni. Binafsi nina imani kubwa na uadilifu wa Dkt Slaa na ujasiri wake pia. Nina amini hakuna kitakacho achwa kuwekwa hadharani soon. Come Dkt Slaa Tanzanians are waiting for you Dkt.
 
Hebu angalieni ibara ya 41 katika katiba ya nchi kipengele cha 6 na 7 vinakinzana mwaka huu
41. (6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
:sad:
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Katiba imelazimishwa kumtambua Jk.. Maana hata na yenyewe inamtambua raisi aliyetokana na wananchi na si vinginevyo... JK hayuko pale kwa mujibu wa sheria bali de facto(kwa kutumia nguvu na kubaka demokrasia)...
CHADEMA wana haki ya kutambua baadhi ya matokeo ya ubunge ndio maana mengine yako mahakamani tayari... Mimi nadhani kipengele cha kutotambua matokeo ya uraisi ndio kero hapa kifutwe halafu mengine tutaongea baadae...
Kule jamaa wanachakachua lakini muhimili mmoja yaani serikali wamebaka mamlaka ya mahakama kwa kusema matokeo ya uraisi hayawezi kupelekwa mahakamani<ibara ya 41(7)>...
Mimi nashauri siku raisi anasoma hotuba pale bungeni ni lazma CHADEMA watoke kuonyesha nia yao ya dhati... Lakini kama watakuwepo basi lazma watakuwa na njia yao mbadala ya kukataa haya matokeo kama walivyodai watatupa msimamo mzima wa ligi ulivyokuwa na kilichotokea...

Watu wengi hawaelewi maana ya mtu anaposema hamtambui raisi maana wengine wanafikiri anakiuka sheria ya treason... Lakini La hasha CHADEMA wamekuwa wastaarabu saana maana maeneo mengine watu walishaanza kutembea barabarani kudai haki tumeona Shinyanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma ujiji kusema kwelli CHADEMA wametumia utaratib mzuri sana na kufuta ile dhana ya kuwa wanapenda fujo... Huu ni ustaarabu mwenye akili atafikiri ila aliyenyimwa akaombewe tuu!!!

Nawasilisha hoja

Katiba yenyewe ilitungwa na CHENGE.
 
Kujipanga tayari kwa uchaguzi wa 2015 ni pamoja na kuhakikisha KATIBA MPYA inapatikana; short of that hakuna cha maana kwa watanzania kitakachopatikana kama uchaguzi utaendeshwa na katiba hii iliyopo!
 
Hebu angalieni ibara ya 41 katika katiba ya nchi kipengele cha 6 na 7 vinakinzana mwaka huu
41. (6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.:sad:
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Hii ibara ya 41 ina mapungufu mengi. Kipengele cha 6 hakijaweka wazi kuhusu kura. Kwamba.............amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombe mwingine yeyote.
Haitoshi tu kusema amepata kura nyingi zaidi, ilipashwa isomeke.....IWAPO TU AMEPATA KURA HALALI NYINGI KULIKO MGOMBEA MWINGINE YEYOTE.

Kusomeka kuwa KURA HALALI ingeliondoa hii dhana ya kuchakachua na hivyo kuwafanya NEC na vyama husika vya siasa kuwa makini na kura wanazopata kuwa lazima ushinde kwa kura nyingi ambazo ni HALALI,siyo wingi tu wa kura.
 
Back
Top Bottom