Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco ulitangaza interest yako lakini wewe uko kazini unasaidia kitu kwa CCM we all noticed na umekataa kukubali majibu ya Lissue ulikuwa very stressed baada ya majibu ya Lissu kuanzia sasa nimeujua u mnazi unalazimisha hoja .Umesomewa kabisa na neno tunapinga na bado ujue CCM walisha jiandaa sasa sijui wewe unalia lia nini mkuu .
 
Pasco,
Suala la katiba lilianza siku nyingi lakini likapata msukumo wa nguvu pale CDM walipolipeleka mahakama ya wananchi. Kosa ni pale walipokubali kuwa rais Kikwete bila ridhaa ya serikali au chama chake alipoamua kulisamimia na CDM wakatulia na kuamini hivyo. Technically hapa ndipo kosa la CDM lilipoanzia.

Kama bunge letu lingekuwa na 'fair play' yote uliyoeleza ndiyo yalipaswa kutokea na lawama dhidi ya CDM zingekuwa haki, kwa bahati mbaya bunge halifanyi kazi kwa kuzingatia sheria au kanuni hasa zinapokinzana na masilahi ya rais na spika ni mjumbe wa CC ya CCM. Anatumwa kutekeleza yale ya chama ni si ya wananchi.

Mswada uliporudishwa baada ya maoni kuleta mushkeli CDM waliuliza je umeondolewa au umefutwa? Nakumbuka PM Pinda alisema umerejeshwa kwenye kamati. Alipobanwa hakuwa na jibu clear na pengine wapinzani wakjua hoja imekufa. Hili nalo lilikuwa kosa kwasababu ilipaswa CDM wapate majibu yasiyo na njia panda.

Kutoka nje ya bunge baada ya kuwasilisha maoni ni jambo la kiungwana kwasababu leo tunajua kwanini walitoka nje, vinginevyo tungebaki kujiuliza wametimka tu je wanajua kwanini wametimka.Kutimka kwao ndiko kumeishtua jamii kuwa lipo jambo, jamii kama ya kwetu ambayo wengi hawana ufahamu mpaka kitakapotokea kishindo ambacho CDM wamekifanya.

Nadhani suala la katiba ni letu sote, CDM wanajaribu kutuwakilisha kwa kadri wanavyoweza wakiwa katika 'stress' ya hali ya juu sana.
Kwa vile katiba ni yetu sasa tujadili tunaiokoaje katiba yetu kwa kushirikiana na CDM ili isipokwe na wanyang'anyi!

Kama ilivyokuwa Nkrumah hall, Karmjee na Zanzibar sisi wenye katiba tusimame na kuwaambia hata kama wamepitisha sheria, sheria hiyo si ile tunayoitaka na tusme No! Tunauwezo wa kuwalazimisha watusikilize, tunasababu tunachokosa kwa sasa ni uthubutu.
Badala ya kuwalaumu CDM tufikirie tutajengaje uthubutu kwa raia wetu ambao wapo tayari

Mawazo ya chadema ndio yako sahihi zaidi ya wengine??

Je CCM siyo sehemu ya wananchi au ni chadema tu ndio sehemu ya wananchi??
 
Pascal wewe si unatoka TBC ambayo ni ya chama cha magamba unataka kutujaza ujinga wa TZ, kwani mambo mangapi ya msingi chadema wameya simamia na spika kwa kulinda maslahi yake amegoma kwa nguvu,CDM walicho amua ni sawa kabisa.Mungu anajua uhuru halisi wa watanzania atauleta lini tupo huru lkn hatupo huru.
 
Duh! utafikiri chadema ndio wanakuwakilisha zaidi wananchi?? wanatumikia matumbo yao braza..fikiri japo kidogo
 
Kwako Pasco,
Naomba nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kuandika thread juu ya CDM kukosea juu ya maamuzi yake lakini mwishoe unaishia kujua ukweli na kukubaliana na ukweli wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya CDM
Nianze kwa kukuuliza ndg Pasco umepitia vema maoni ya upinzani?
Kama umepitia je unakubaliana na hoja zilizopo au hukubaliani nazo?
Naomba unipe mapungufu ya speech ile halafu tuje tujikite katika njia iliyotumika kama ni sahihi.
Nahisi hiyo njia pekee ya kukusaidia Pasco ndugu yangu.
Sitalala leo kuhakikisha Pasco unaelewa kilichofanywa na CDM hakikuwa kosa bali ushujaa dhidi ya wananchi wenye kiu ya kweli dhidi ya katiba inakibeba chama kimoja na kuwapa nafasi mafisadi kutamalaki!!!!
 
Naweza kuwa natoka ne ya mada lakini naomba kujuzwa au kuelimishwa.

From CHADEMA, NCCR na wataka mabadiliko wengine yote.
  • Nini hasa kilitakiwa au kinatakiwa kufanyika ?
  • Assume CDM ndio wangekuwa na nchi na tuko atia hali hii ya kaitba tata hasa process gani zingefanyika. zingefanyika kivipi? washiriki wakuu wa kuandika na kukusanya maoni ya katiba mpya wangepatikana vipi ? Nini hsa kinatakiwa kufanyika tofauti na JK ( CCM )wanavyopendekeza? Jiulize na mswali mengine mengi yanyoendana na hayo.....
NB.
Mimi ni mmoja wa wataka mabdiliko( Sio ya Kisiasa tu) lakini so far niko gizani. Ebu wana Jf nifumbueni macho zaidi ni wapi CCM na Jk wanapokosea na ni upi ambao ni mwelekeo sahihi kutokana na baadhi ya maswali niliyouliza pale juu.

Kila jambo linaanza na 1,2,.... Huu muswada ulitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza. Maana ya kusoma muswada kwa mara ya kwanza ni kwamba unawekwa kwenye national gazzette na wananchi wanatoa maoni, baada ya kupata maoni (kwa utaratibu wa bunge) unasomwa kwa mara ya pili. Hatua hii inawapa wawakilishi wa wananchi (wabunge) kujadili kitu kizima kwa maana ya kupitia maoni ya wananchi na kuboresha ili usomwe kwa mara ya tatu - kupitishwa.

Now, kwa bahati mbaya ccm imekuwa inaendesha hii nchi kwa mazoea bila kusoma/kujali sheria na taratibu zilizopo! Huu muswada ilipelekwa bungeni mwezi March kwa njia 'DHARURA! (dharura ya nini kwenye katiba ya nchi?). Hata hivyo ulikataliwa kwa sababu ulikuwa mbovu mbovu, na mbaya zaidi ulikuwa umeendikwa kwa lugha ya kiingereza! Spika Makinda akatoa tamko utolewa uboroshwe na wapate maoni ya wananchi. Wakubwa kabla ya kuboresha na hata kuundika kwa kiswahili wakaamua kupata maoni chap chap Dar, Zanzibar na Dodoma kwa siku kama tatu tu! Mikoa mingine wakaachwa sijui wako Kenya?

Hata hivyo hatua hii ilikuwa pre-mature kwa sababu bado muswada ulikuwa kwa lugha ya kiingereza hivyo wananchi wengi wasingejua nini kimeandikwa. Wajumbe wa kamati walipoomba kwenda mikoa mingine walau 10 Spika akazuia. Muswada wa sasa umetafsiriwa week chache kabla ya bunge kuanza, na haujapata maoni ya wananchi kama taratibu zinavyoelekeza. Na unanekana kumpa rais nguvu ya kuamua katiba iweje akishirikiana na rais wa wanzibar na wakubwa wachache (i.e mwanasheria mkuu). Kwa kifupi huu naweza kuufananisha na waraka toka kwa Mugabe kwenda kwa Morgan Tsvangirai= umekaa vibaya sana huu muswada.
 
Duh! utafikiri chadema ndio wanakuwakilisha zaidi wananchi?? wanatumikia matumbo yao braza..fikiri japo kidogo

Hakuna mtu asiyetumikia tumbo na ndiyo maana ikaandikwa na asiye fanya kazi na asile.
Wanasiasa ndiyo kazi yao na ndiyo kula yao inatokea huko, ni dhambi kama hawatawatumikia kiuadilifu wananchi na kuruhusu uovu, ufisadi na mambo mengine mengi ambayo kwa nafasi zao wangeweza kuyazuia na badala yake wakayaruhusu kwa tamaa ya fedha ambalo wewe umeliita tumbo.
 
Pasco ulitangaza interest yako lakini wewe uko kazini unasaidia kitu kwa CCM we all noticed na umekataa kukubali majibu ya Lissue ulikuwa very stressed baada ya majibu ya Lissu kuanzia sasa nimeujua u mnazi unalazimisha hoja .Umesomewa kabisa na neno tunapinga na bado ujue CCM walisha jiandaa sasa sijui wewe unalia lia nini mkuu .

siku zote analazimisha hoja...nashukuru kuwa ulimona alivyokuwa stressed baada ya majbu na ndio maana akaleta hoja hii hapa akiwa bado na povu lile lile.........akae akijua kuwa wananchi walio wengi wanapinga utaratibu uliotumiwa na ccm A na B na pia kauli ya jk ya kujivisha madaraka kuhusu uuundwaji wa katiba juzi wakati anaongea na wazee wa ccm....kuna mtu amemuulia huko juu kuwa chadema ni nani? na kwa nini wanapinga? hajajibu.....la msingi hapa ccm walipaswa kusikiliza hoja za chadema na nccr na sio kulazimisha kama alivyofanya spika...
 
Kila jambo linaanza na 1,2,.... Huu muswada ulitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza. Maana ya kusoma muswada kwa mara ya kwanza ni kwamba unawekwa kwenye national gazzette na wananchi wanatoa maoni, baada ya kupata maoni (kwa utaratibu wa bunge) unasomwa kwa mara ya pili. Hatua hii inawapa wawakilishi wa wananchi (wabunge) kujadili kitu kizima kwa maana ya kupitia maoni ya wananchi na kuboresha ili usomwe kwa mara ya tatu - kupitishwa.

Now, kwa bahati mbaya ccm imekuwa inaendesha hii nchi kwa mazoea bila kusoma/kujali sheria na taratibu zilizopo! Huu muswada ilipelekwa bungeni mwezi March kwa njia 'DHARURA! (dharura ya nini kwenye katiba ya nchi?). Hata hivyo ulikataliwa kwa sababu ulikuwa mbovu mbovu, na mbaya zaidi ulikuwa umeendikwa kwa lugha ya kiingereza! Spika Makinda akatoa tamko utolewa uboroshwe na wapate maoni ya wananchi. Wakubwa kabla ya kuboresha na hata kuundika kwa kiswahili wakaamua kupata maoni chap chap Dar, Zanzibar na Dodoma kwa siku kama tatu tu! Mikoa mingine wakaachwa sijui wako Kenya?

Hata hivyo hatua hii ilikuwa pre-mature kwa sababu bado muswada ulikuwa kwa lugha ya kiingereza hivyo wananchi wengi wasingejua nini kimeandikwa. Wajumbe wa kamati walipoomba kwenda mikoa mingine walau 10 Spika akazuia. Muswada wa sasa umetafsiriwa week chache kabla ya bunge kuanza, na haujapata maoni ya wananchi kama taratibu zinavyoelekeza. Na unanekana kumpa rais nguvu ya kuamua katiba iweje akishirikiana na rais wa wanzibar na wakubwa wachache (i.e mwanasheria mkuu). Kwa kifupi huu naweza kuufananisha na waraka toka kwa Mugabe kwenda kwa Morgan Tsvangirai= umekaa vibaya sana huu muswada.

Ambaye hajakuelewa basi tena. Umesema kweli ilivyo.
 
Pasco my bro. Chadema has nothing to lose kikubwa kilichokuwa kinatafutwa na Chadema na wapinzani kinaelekea kupatikana katiba mpya ambayo CCM walikuwa hawataki, hadi sasa Chadema wanachezea kwenye eneo la adui wao. Kosa kubwa ambalo CCM wamelifanya (kwao) si kwa wananchi ni kukubali kuanzishwa kwa katiba mpya walikuwa hawana wazo hilo mwaka mmoja uliopita, wanachokifanya CCM ni kubadilisha eneo la kupigia faulo lakini faulo iko palepale.

CCM wanafuata nyayo za rais wa zamani wa Zambia Banda na chama chake cha MMD, chama cha upinzani Patriotic Front (PF) cha Sata kilishauri baadhi ya vifungu vya uchaguzi vibadilishwe wakakataa, leo Sata anatumia katiba hiyo hiyo kuwanyoa MMD. Hata CCM isidhani kuwa itatawala siku zote, na baada ya katiba kubadilishwa kwa kufuata matakwa yao huenda ikafanya chama kingine kiingie madarakani 2015 na kutumia vifungu CCM wanavyodhani ni vyao.
 
Mkuu Pasco rudi tetea hoja yako au kile ulochokuwa unawaambia cdm rudi ukifanye ,kama ulivyosema huo ndio uungwana.kimya chako hatukielewi hasa sisi
Tunaotafuta ukweli
 
asante sana umemaliza kila kitu,
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
 
Pasco my bro. Chadema has nothing to lose kikubwa kilichokuwa kinatafutwa na Chadema na wapinzani kinaelekea kupatikana katiba mpya ambayo CCM walikuwa hawataki, hadi sasa Chadema wanachezea kwenye eneo la adui wao. Kosa kubwa ambalo CCM wamelifanya (kwao) si kwa wananchi ni kukubali kuanzishwa kwa katiba mpya walikuwa hawana wazo hilo mwaka mmoja uliopita, wanachokifanya CCM ni kubadilisha eneo la kupigia faulo lakini faulo iko palepale.

CCM wanafuata nyayo za rais wa zamani wa Zambia Banda na chama chake cha MMD, chama cha upinzani Patriotic Front (PF) cha Sata kilishauri baadhi ya vifungu vya uchaguzi vibadilishwe wakakataa, leo Sata anatumia katiba hiyo hiyo kuwanyoa MMD. Hata CCM isidhani kuwa itatawala siku zote, na baada ya katiba kubadilishwa kwa kufuata matakwa yao huenda ikafanya chama kingine kiingie madarakani 2015 na kutumia vifungu wanavyodhani ni vyao.

Wakati chadema itakuwa inatawala hawataandaa hata katiba kama wanavyofanya ccm..wanavyopenda madaraka salale!

Ukweli ni kuwa chadema hawataki JK (rais) aunde tume ya kuchukua maoni ya wananchi ili kuunda katiba..

Lakini Slaa angekuwa rais angeunda tume (wangekuwa wanampongeza)

Tatizo la chadema siyo ccm ni JK period..
 
Mawazo ya chadema ndio yako sahihi zaidi ya wengine??
Je CCM siyo sehemu ya wananchi au ni chadema tu ndio sehemu ya wananchi??

Inawezekana mawazo ya CHADEMA yakawa na mapungufu, lakini kwa hakika mawazo, matendo ya CCM yametumaliza. Ukiondoa miaka ya uongozi wa Nyerere Tanzania imekuwa shamba la bibi. Na pale kiongozi mfano wa mkoa anakosea, au mayor au mkurugenzi wananchi wanashindwa kumuwajibisha kwa sababu katiba yetu ina urais wa kifalme. Maamuzi yote juu ya watanzania milioni 44 na ushee yako chini ya mtu mmoja, hakuna wa kumhoji wala kumzuia. Hili ndio chimbuko la balaa tulilonalo Tanzania leo hii. Nchi imegeuzwa miguu juu kichwa chini lakini wananchi hawana uwezo zaidi wa kulalamika maana wakubwa wote wanateuliwa na rais: mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugezi wa wilaya (DED) wakuregenzi wa mashirika, mkuu wa police.... rais yuko kila mahali. Na la kushtusha rais anaambiwa (kwenye katiba) ataamua kwa namna atakavyoona inafaa!!! i,e kujadiliana na watu EPA?

Ni muhimu kabisa tusifanye makosa kwenye huu muswada maana unaturudisha kule kule.
 
...Nitashangaa watu wanaodhani huu muswaada umepitishwa kwa nia njema kabisa. Kwahiyo, waliotofautiana nao wajikusanye na kushiriki, kama vile hakikutokea chochote cha tofauti.

...Kwa ufupi, kuna uhuni mwingi umetumika kwenye hii process, kila aliyefuatilia akiwa na akili timamu anafahamu. Ni as if, we are doing this for some people's benefit and not for the nation.

...Katiba ni kwa ajili ya watanzania wote, and yes, wapinzani ni watanzania pia. Walipaswa kusikilizwa, sio kubezwa na kupotoshwa kile walichokisema, regardless walikisemea wapi -kwenye kampeni au la- na wakati gani.

...Kwa ujinga huu, hata wao wakipata madaraka wataibadili. Si itasemwa iliyopo haifai.
 
Kwako Pasco,
Naomba nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kuandika thread juu ya CDM kukosea juu ya maamuzi yake lakini mwishoe unaishia kujua ukweli na kukubaliana na ukweli wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya CDM
Nianze kwa kukuuliza ndg Pasco umepitia vema maoni ya upinzani?
Kama umepitia je unakubaliana na hoja zilizopo au hukubaliani nazo?
Naomba unipe mapungufu ya speech ile halafu tuje tujikite katika njia iliyotumika kama ni sahihi.
Nahisi hiyo njia pekee ya kukusaidia Pasco ndugu yangu.
Sitalala leo kuhakikisha Pasco unaelewa kilichofanywa na CDM hakikuwa kosa bali ushujaa dhidi ya wananchi wenye kiu ya kweli dhidi ya katiba inakibeba chama kimoja na kuwapa nafasi mafisadi kutamalaki!!!!

ukijisikia kulala we lala tu...mpaka sasa ameshapata somo tosha si unajua dawa ya homa kali ni sindano japo inauma......ye mweyewe yuko hapa namuona lakini yuko kimya kajibu post moja ya jamaa aliyemtaja jina lake lote....
 
Chadema wangetumia kifungu cha 86 kusimamija hoja kuungwa mkono, wangetakiwa watoe sababu ya kuukata mswada huo usiwasilishwe kwa mara ya pili. Walitakiwa wawe na sababu ambazo zitawashawishi wabunge wengine wawaunge mkono. Sababu za mswada kutoungwa mkono zimo kwenye hotuba ya Lissu.

Sasa swali kwa wanaoamini ktk kifungu cha 86 ni: ni wabunge wangapi waliunga mkono hoja zilizopo kwenye hotuba ya lissu? Ukishapata jibu, jiulize swali lingine, ambalo ni je kama kifungu cha 86 kingetumika mswada ungesitishwa?
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.

....Hata Ngereja, Jailo, Luhanjo na Uttoh wanaonewa kwa sababu ya dini yao na sio ubadhirifu!
 
CDM wengi humu ni mbumbu wa sheria na watu wakufuata mkumbo tu. Wao wanamchukulia mh. Lisu kama Mungu na hakosei hata kidogo.

Mfano uliotoa kuhusu ushauri wake kwa mh Mbowe na kilichomtokea ni kielelezo cha imani ya kibubusa kwa mwanasheria huru kijana.

Utakachokipata humu ni matusi tu badala ya admission of mistakes.

kuwa mwanaharakati si lazima uwe mwana chadema.Hoja ya kikatinba ni hoja ya watanzania wote.Hivyo ukiona wanakupa changamoto ya utofauti na fikra za kiccm, si lazima uwatukane kuwa mbumbumbu wa kisheria, bali kubali nao wana hoja ya kimsingi ya kikatiba na utanzania.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom