Tatizo hapa si waziri, ambaye ana act kama Kasuku wa ku-echo yale yanayotolewa na bosi wake. Waziri wa katiba kwenye serikali ya ki -authoritarian ya CCM ni mtu mdogo sana aliyewekwa ili apate KULA huku akilinda masilahi ya mabwana zake.
Source kuu ya upupu huu ni CCM na kamati kuu yake ikiongozwa na genge la wapora mali za nchi ya (CC) ambao kwao hawa Tanzania kuwa na system iliyo free from political influence ni kuhatarisha masilahi yao (wao huita ya chama). CCM haina nia wala dhamira ya dhati ya kupata katiba mpya iliyotokana na wananchi bali wanavyotaka kufanya sasa ni kuirubuni jumiya ya kimataifa na wananchi ili ionekane kuwa kuna mabadiliko yametokana na wananchi na kuihalalishia CCM kuendelea michezo michafu wakati wa chaguzi na kuendelea kuwaamulia watanzania nani awaongoze hata kama hawamtaki. Katiba mpya iliyotokana na wananchi ni mwanzo wa mwisho wa viongozi wasiowajibika kwa wananchi na CCM 99% yao ni mfano.
Rejea kauli ya Mkapa - Si vema mabadiliko ya katiba yakaongozwa na wapinzani, serikali lazima ifikirie namna ya kubadili katiba, mantiki ya kauli kama hizi zimeanza kuonekana kwenye miswada ya kidikteta kama huu. Bila shinikizo kutoka kwa wananchi kwa style ya barua kama hizi na umma kusimama imara, CCM hawata na hawapo tayari kufanya lolote litakaloonekana ni kutishia ustawi wao wa kidikteta waliouzoea.
And sad enough ni kuwa kila kete ikikataa watavuruga mchezo. People need to get prepared for gud or for worse hawa watu wanalinda maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya taifa ila raia wakikomaa basi jumuia ya kimataifa itawapa tough. Nashukuru baraza la maaskofu kupitia hiyo Idara kwa msimamo wao huo maana mpaka hapo wamesha twist mchezo mpaka wakajipange tena. God is on our side hakuna kitakachoharibika!