KATIBA: Askofu Ruzoka amlima barua Waziri

kanisa likishasema basi hakuna wa kupinga!muswada umeshagonga mwamba!
Hakuhitajiki ushabiki katika swala hili.... Ni hekima na busara ndio zitawale na wala sio elimu ya mtu, cheo au madaraka ila matakwa ya watanzania wote bila kujali dini, kabila, rangi n.k
 
Nasubiri counter attack ya masheikh maana wamezoea maaskofu waanzishe na wao wapate cha kusema. Najua baadhi mtabisha but wait and see !
Kwenye jamii yoyote huwezi kukosa watu kama hao, ila cha msingi ni kujiuliza kwanini wapo hivyo na nini kilisababisha wawe hivyo. Huenda kuna aliewafikisha hapo kwa makusudi. Kuruhusu tofauti kama hizi kuendelea ni ujinga, na sio vizuri kuwacheka watu zaidi ya kuwaonyesha njia.
 
JPLETTER.jpg

Nimeisoma barua hiyo neno kwa neno, kama kijana, msomi mtanzania, nimejiona kuwa naisaliti nchi na wananchi (watanzania) wa nchi hii kwa kukaa kimya muda wote huu tangu jpili, huu mjadala ulipoanzia pale UDSM. Mimi na vijana wa umri wangu waliobahatika kupata elimu kama yangu kwa kukaa kwetu kimya hasa juu ya mswada kama huu ni usaliti wa hali ya juu. Leo asubuhi nimebahatika kufuatilia mjadala wa bunge yaliyojitokeza na yatakayotokea katika mjadala huu ni aina nyingine ya usaliti wa hali ya juu kwa watanzania wazazi/walezi wetu waliojinyima ili tusome.

Hii barua kwa mtu aliyebahatika kupata elimu kidogo tu kama uko upande wa wale waliondaa mswada huu basi kuliko utoe comments zako hasi na mawazo hafifu juu yake bora unyamaze kuliko kuendelea ku-justify usaliti wako kwa waliokusomesha ili uwe tochi yao wakati kama huu wa giza kuu.

Barua hii ni fupi yenye mistari michache lakini imebeba maudhui na mawazo yetu sote tuliosoma na wasiosoma, ni barua iliyotumwa kama tochi wakati huu wa giza, iwasidie wale wanaotaka kufanya yale ambayo ni kinyume na matakwa ya watanzania walio wengi ili waone njia sahihi.

Mungu tusaidie ili tuwe kweli msaada kwa nchi yetu na sio unafiki huu tulionao sasa.
 
mkifuatilia posts za wachangiaji wengine ni wazi kabisa wanafanya yale ambayo chama tawala wanatumia kuhakikisha wananchi wanachukia vyama vya upinzani vyenye nguvu na kuhakikisha kila institution inayo onyesha madhaifu ya chama tawala na serikali yake inakua discredited.

sasa hawa wachangiaji wanakuja na maneno kama Udini, Ukabila etc WAMETUMWA hawa, hawajaja humu JF kuchangia mada yoyote bali kuvuruga, kuchafua na kuwatoa watu kwenye mada za msingi zinazo tishia uwepo wa chama tawala na serikali yake.

mkiona mchangiaji posts zake nyingi hazina substance na anang'ang'ania kudhoofisha mada muacheni, msimjibu kitu! Wengine humu wamekuja MAKUSUDI kabisa kuharibu topics za maana bila kua na mchango wowote wa maana !
 
Guys I wish wote mngekuwa kama mimi, Ignore kupeng'e!! kwa nini mnamjibu??? thread tamu imeishaharibika!

ASKOFU big up ubarikiwe!
Lazima wajibiwe,tumegundua wengine wanahitaji brushfires.,BTW ni kuwaeleza kuhusu freedom of speech,maoni ni ya wananchi bila kuangalia dini.Otherwise hata hii posti yako nisingeijibu,na nyingine nyingi tu.
 
Mmmmmh jamani mambo ya shakuwa mambo,

Kama serikali itaendelea kukaidi maoni ya wananchi naona watakuwa wameruhusu wenyewe Nguvu ya umma ichukue hatamu katika kujenga katiba.....

heshima aliyokuwa aipate rais sasa hawezi kuipata tena kwani yeye keshaonekana janja yake ni ipi ...kuanzia sasa nairudisha heshma hyo kwa nguvu ya umma,katiba ijayo ni nguvu ya UMMA na si utashi wa JK ..Amina!
 
Mkuu Waberoya, uki-ignore unakosea; hawa wapo, wanahitaji kuelimishwa. A nice approach can help, you need to be patient usije ukabamiza pc yako kwa hasira.

Najua Kupeng'e anawakilisha kundi kubwa la namna yake, kama msomi huyu anaona Muswada hauna mapungufu hata kidogo, waza akipewa nchi huyu mwenzetu taifa litaenda wapi? Ni waziri/rais mtarajiwa huyu

Mkuu Maxence kuna watu wa kuelimishwa humu, lakini siyo wa type ya Kupeng'e

Kila siku watu wanapinga udini humu, he/she knows in and out na anafanya deliberately tu kuharibu mijadala.

Mtu wa aina hii kama woote wangekuwa wanajua kuwa post zao zinapotea wasingepoteza muda wao, kwa kufanya hivi tungeweza kuwaondoa akina Kupeng'e wengi mno.
 
Mkuu Maxence kuna watu wa kuelimishwa humu, lakini siyo wa type ya Kupeng'e

Kila siku watu wanapinga udini humu, he/she knows in and out na anafanya deliberately tu kuharibu mijadala.

Mtu wa aina hii kama woote wangekuwa wanajua kuwa post zao zinapotea wasingepoteza muda wao, kwa kufanya hivi tungeweza kuwaondoa akina Kupeng'e wengi mno.
Wako wengi kwenye jamii,kuwa ignore kwa namna unayosema humu JF siyo solution,solution ni kuwaonyesha kuwa hawana hoja.Kuna watu wenye uwezo wa kudeal nao bila shaka.
 
Lazima wajibiwe,tumegundua wengine wanahitaji brushfires.,BTW ni kuwaeleza kuhusu freedom of speech,maoni ni ya wananchi bila kuangalia dini.Otherwise hata hii posti yako nisingeijibu,na nyingine nyingi tu.

huwa hawaelewi hawa, hujajua tu? why hurt your feelings!! stay focus
 
Katiba ya Vatican muipange nyinyi hata ya nchi yetu Tanzania pia, hapana hii haikubaliki
Lazima kuwepo na independent pannel yenye kuwashirikisha wadau wa jamii ya watanzania na siyo maamuzi ya mwisho yawe ya mtu mmoja(Rais) ambaye ndiye mwenyekiti wa chama kilichoko madarakani kilichoingizwa madarakani na katiba hiyo hiyo tunayotaka kuibadili,huo ni mkorogo,tumia akili.
 
huwa hawaelewi hawa, hujajua tu? why hurt your feelings!! stay focus
Mkuu i dont go by feelings around here, otherwise the heat will be too much to be able to stay in this kitchen man.
Wanapodai kula na kipofu, maana yake ni na wewe kujifanya ni kipofu, halafu mnaelewana.
 
Askofu kaandika mambo objective yasiyojali itikadi na yenye maslahi kwa watanzania wote. tusibeze hoja alizotoa bila kujali itikadi yoyote
 
Haya Mkuu twende kwenye HOja

Muswada uliopelekwa bungeni una matatizo gani?

Mimi mbona nauona uko sawa?

Kupeng'e now you are talking.

Nimeusoma mswada najikuta na mashaka mengi kuliko matumaini.

1. Mswada unaitwa "constitutional review" sio mswada wa katiba mpya. Tanzania ya sasa inahitaji kanzu mpya, hii ya zamani ni kuahirisha matatizo tu.
2. Terms of Reference anatengeneza Rais wa JMT (sec 8). Rais ni binadamu mwenye mapungufu yake ni vipi akiamua kuleta ToR zenye kuumiza/kupendelea upande mmoja??
3. Tume ya katiba inateuliwa na Rais bila kuwathibitisha wateuliwa Bungeni (sec 6). Checks and balance ya kimagumashi ni kwa uteuzi wa waziri mkuu tu??
4. Tume itaripoti kwa Rais (Sec16). "Amlipaye mpiga zomari..........."
5. Rais atateua Bunge la Katiba - Constituent assembly (sec 21). Oh my God,

The Bill is all about the President, yaani tunarudi kule kule ambako kila kitu kumerundikwa kwa President (hiring and firing).
Sasa kama mswada umemweka kando mwananchi unadhani hiyo katiba itakuwaje?

Mwananchi atakuja kuingizwa kama Rubber Stamp au yale mwananchi akipendekeza Rais asipoyapenda yatanyofolewa.
 
Mkuu Maxence kuna watu wa kuelimishwa humu, lakini siyo wa type ya Kupeng'e

Kila siku watu wanapinga udini humu, he/she knows in and out na anafanya deliberately tu kuharibu mijadala.

Mtu wa aina hii kama woote wangekuwa wanajua kuwa post zao zinapotea wasingepoteza muda wao, kwa kufanya hivi tungeweza kuwaondoa akina Kupeng'e wengi mno.

Mkuu huyu anajua analolifanya yupo kikazi zaidi ya ufikiriavyo. Ila ameingia opposite sex toilet, hapa JF kila mtu anafikiri kwa kutumia ubongo wake, huwezi kumpata mtu kwa propaganda bali ni facts with supporting documents only otherwise you will be seen as a zombie.
 
Kwanini hajaandika barua yeye kama yeye? na kaamua kupitia TEC

Ulitaka aongee kama nani ? wakati huo ndio wadhifa wake MWENYEKITI
TUME YA HAKI NA AMANI (TEC)
, na hapa anatetea haki ya Watanzania na Kulina Amani.
 
mimi hapa sielewi... tatizo ni aliyeandika barua? dhehebu lake?? content ya letter? subject ya barua?? letterhead?? au kwamba muswada una matatizo??
 
Afadhali wenye akili zao wameamua kutoa mwongozo. Tusubiri upande wa pili wa wasio na akili wakija kuipinga barua hii tena kama kawaida yao bila ya kutoa maoni yao kuhusu muswada!

Huu ni ushahidi tosha kwamba kanisa katoliki linashirikiana na chadema
 
Back
Top Bottom