KATIBA: Askofu Ruzoka amlima barua Waziri

sitaki kuamini kama wachangiaji mada jf wote ni wazima. tujirekebishe UDINI ni sumu mbaya sana!
 
Ndugu,mara zaidi ya tano umerudia kuonesha kukerwa na kile unachodai kuwa ni askofu kuandika kwa niaba ya wananchi na si kwa niaba yake au wakatoliki wau wakristo. Which is a very geniune concern. Imenifanya nirudie tena na tena kusoma hii barua,na kujihofia mwenyewe kuwa "inawezekana nimeanza kupoteza uwezo wangu wa kuelewa sasa?" Hebu nirudie tena hapa:

HOFU NA MASHAKA YA WANANCHI KUHUSU MUSWADA WA MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA KWA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI YA MWAKA 2011
Kwa
Waziri wa Katiba na Sheria

Mheshimiwa Waziri,
Muswada wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi wa mwaka 2011 Namba 1 wa tarehe 11 Machi, 2011 umetangazwa katika siku chache zilizopita.

Baada ya kuusoma muswada huu tulishangazwa kuona kwamba mchakato wote unaanzia na kuishia kwa Rais na kwamba Chombo Kikuu cha kuratibu mchakato wote ni Tume itakayoteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala.

Tunatambua kwamba kilio cha kutaka Katiba mpya kilitokana na utashi mwema na pia hasira njema ya jamii ya Watanzania wakitaka mabadiliko yaliyo na hekima na utu.

Tunahofia kwamba maudhui na mwelekeo wa muswada wa marekebisho ya Katiba unaopelekwa Bungeni havitakidhi mahitaji mazito ya watu na huenda ukachochea hasira ambayo imekwisha jidhihirisha katika jamii yetu.

Tunakuomba ulisimamie zoezi la marekebisho ya katiba kwa hekima sana ukiongoza tafakari jadidi na elimu angavu itakayowezesha zoezi lote kuwa la mazungumzo ya kitaifa kweli kweli huku amani, maelewano na makubaliano vikilindwa sana katika wakati mgumu huu.

Tafadhali lipatie taifa muda wa kufaa na chombo huru kinachoaminika kuongoza wananchi kufikia makubaliano yatakayojenga msingi imara wa taifa letu kwa wakati ujao.

Askofu Mkuu Paulo Ruzoka
MWENYEKITI
TUME YA HAKI NA AMANI (TEC)
5/4/201
1
Sasa naomba twende pamoja tuelimishane tu.

  • Nime-highlight maeneo yote ambayo nadhani ndio likely zaidi kuwa yamekukera. Nikianza na title ya barua, kuna neno wananchi,ambalo umelalama sana juu ya uwepo wake. Ukiishia kusoma title peke yake - na hasa ukiwa na pre-judgement yako kwenye background ya uelewa wako conciously au sub-conciously - ni rahisi ku-arrive kwenye concern hizo. Lakini kama ni mtu makini na objective na ukajaribu kusoma CONTEXT ya barua hutasumbuka sana. Hakuna sehemu hata moja katika body ya barua inayoonesha TEC inawasemea watanzania kuhusu katiba,zaidi ya kuonesha genuine concern zao kama taasisi ndani ya jamii;yenye ueledi, iliyo responsible, iliyo relevant, iliyo pro-active, inayoona kesho ikijaribu kutoa mchango wake kuiasa serikali itende kwa umakini zaidi ili kuepusha madhara mbeleni. That should be commendable to any citizen with Taifa's best interest at heart! Na natarajia taasisi nyingine,zitachukua nafasi zao kutoa tamko walau.
  • Kuhusu "kilio cha katiba mpya...(cha)...jamii ya watanzania" . nani asiyejua ukweli huu? Chama tawala kilijifanya kutojua, waziri akajifanya kutojali,lakini hatimaye Rais akathibitisha kuwa wanajua kuhusu kilio hiki. Na hapa ndipo tulipofikia. Je kunahitajika research zaidi/tena kujua kuwa hiki ni kilio cha watanzania?
  • Kuhusu muswada "kutokidhi mahitaji mazito ya watu"...Wao kama TEC, katika utashi na weledi wao wameona kuwa haukidhi. N a wajituma kufikiri kuwa ukiwapelekea watu watu - ambao wamekwisha anza kuonesha hasira na kutoridhishwa - majibu yasiyokidhi kunauwezekani mkubwa wa kuchochea hasira. Kongamano la UDSM lilionesha hivyo, vyama vya siasa vimeona hivyo, mie pia nimeona hivyo. Hii ni hoja tu.Na aonae tofauti ana uhuru wote wa kuipinga na kutoa tamko pia. What's the problem?
  • Mwisho: Hivi nikisema wape watanzania haki wanayoidai. Naulizwa kwanini umesema?Kwanini umetusemea? Au kuna wananchi hawataki haki? AU kuna mtu au watu ni haramu kiasi cha kwamba hata wakikutakia kheri unaikataa? Kwa lipi? Kwamba kheri inaweza kugeuka balaa kwa kutegemea ni nani ameitoa?
SI MWENDO MZURI! TAFAKARI!

Basi Askofu Ruzoka kimeshinda nini kuandika kuwa Wananchi wa dhehebu la kikatoliki wanapinga mapendekezo ya katiba atumie neno la wananchi??
 
Mkuu,

Tofautisha kushirikisha maoni ya wananchi kwa kutumia taasisi za kidini na kuwakilisha maoni ya wananchi kupitia taasisi za dini. La kwanza ni kwamba wananchi wanashirikishwa katika utoaji wa maoni na la pili taasisi inatoa tamko lenye kuwakilisha kundi fulani la watu. Binafsi wananchi kushirikishwa ndio nachokitaka ila sio kwa kupitia utashi wa taasisi za kidini hilo tutakuwa tunaelekea kusiko na matokeo ya kama yanayotokea Ivory Coast hayako mbali maana kuna mahali yatafikia ukomo.

Nijuavyo mimi 'Commission for Justice and Peace' - Tume ya Haki na Amani - ya TEC ni mwavuli wa Tume ya Haki na Amani katika kila parokia. Tume hizo huwa zina wanachama wa makundi mbalimbali na inapotokea kuwasilisha maoni ya hayo makundi kitaifa, uwasilishwaji wake unafanywa chini ya mwenyekiti wake Askofu Ruzoka. Kwa hiyo, sijaona ni namna gani maoni haya yaliyotolewa hayawasilishi maoni ya wananchi. Labda kama wewe mwenyewe utatoa ushahidi kuwa hao wananchi hawakushirikishwa toka kwenye 'grassroots' - Jumuiya ndogondogo (Small Christian Communities).
 
Ndugu,mara zaidi ya tano umerudia kuonesha kukerwa na kile unachodai kuwa ni askofu kuandika kwa niaba ya wananchi na si kwa niaba yake au wakatoliki wau wakristo. Which is a very geniune concern. Imenifanya nirudie tena na tena kusoma hii barua,na kujihofia mwenyewe kuwa "inawezekana nimeanza kupoteza uwezo wangu wa kuelewa sasa?" Hebu nirudie tena hapa:

1
Sasa naomba twende pamoja tuelimishane tu.

  • Nime-highlight maeneo yote ambayo nadhani ndio likely zaidi kuwa yamekukera. Nikianza na title ya barua, kuna neno wananchi,ambalo umelalama sana juu ya uwepo wake. Ukiishia kusoma title peke yake - na hasa ukiwa na pre-judgement yako kwenye background ya uelewa wako conciously au sub-conciously - ni rahisi ku-arrive kwenye concern hizo. Lakini kama ni mtu makini na objective na ukajaribu kusoma CONTEXT ya barua hutasumbuka sana. Hakuna sehemu hata moja katika body ya barua inayoonesha TEC inawasemea watanzania kuhusu katiba,zaidi ya kuonesha genuine concern zao kama taasisi ndani ya jamii;yenye ueledi, iliyo responsible, iliyo relevant, iliyo pro-active, inayoona kesho ikijaribu kutoa mchango wake kuiasa serikali itende kwa umakini zaidi ili kuepusha madhara mbeleni. That should be commendable to any citizen with Taifa's best interest at heart! Na natarajia taasisi nyingine,zitachukua nafasi zao kutoa tamko walau.
  • Kuhusu "kilio cha katiba mpya...(cha)...jamii ya watanzania" . nani asiyejua ukweli huu? Chama tawala kilijifanya kutojua, waziri akajifanya kutojali,lakini hatimaye Rais akathibitisha kuwa wanajua kuhusu kilio hiki. Na hapa ndipo tulipofikia. Je kunahitajika research zaidi/tena kujua kuwa hiki ni kilio cha watanzania?
  • Kuhusu muswada "kutokidhi mahitaji mazito ya watu"...Wao kama TEC, katika utashi na weledi wao wameona kuwa haukidhi. N a wajituma kufikiri kuwa ukiwapelekea watu watu - ambao wamekwisha anza kuonesha hasira na kutoridhishwa - majibu yasiyokidhi kunauwezekani mkubwa wa kuchochea hasira. Kongamano la UDSM lilionesha hivyo, vyama vya siasa vimeona hivyo, mie pia nimeona hivyo. Hii ni hoja tu.Na aonae tofauti ana uhuru wote wa kuipinga na kutoa tamko pia. What's the problem?
  • Mwisho: Hivi nikisema wape watanzania haki wanayoidai. Naulizwa kwanini umesema?Kwanini umetusemea? Au kuna wananchi hawataki haki? AU kuna mtu au watu ni haramu kiasi cha kwamba hata wakikutakia kheri unaikataa? Kwa lipi? Kwamba kheri inaweza kugeuka balaa kwa kutegemea ni nani ameitoa?

SI MWENDO MZURI! TAFAKARI!

Mshindo, asante sana kwa mawazo yako mazuri. Uliyosema yanaeleweka vizuri sana! Keep it up!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom