kati ya hotuba bora kuwahi kutolewa na kikwete tangia aingie Madarakani ni ya 1,july,2012

simaye

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
426
214
Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 1, july, 2012 alitoa hotuba yake ya mwisho wa mwezi juu ya Mgomo wa Madaktari na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.Nilivutiwa zaidi namna alivyozungumzia mgomo wa madaktari unaoendelea hapa nchini na kwa kweli kama Madaktari wote walifuatilia watakuwa wameachana na mgomo na leo hii wako kazini. Kwanza Rais aliongea kwa busara pasipo kutumia ushabiki wa kisiasa ambao kwa kweli umekuwa ukikoroga hotuba zake nyingi hasa anapozungumzia masuala nyeti ya kitaifa kama jana..Pili amezungumza kwa hoja zinazoashiria ukweli juu ya uwezo wa nchi na madai ya madaktari.Ombi langu ni yeye kusisimamia namna ya kutoa hotuba kama rais pasipo kuingiza upambe wa kisiasa ambao mara nyingi huwa ni za kulazimisha ushindi hata kama suala lenyewe linoonesha kuwa wanaodai wana hoja za msingi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom