achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Ninakubaliana na wewe kuwa Dr Lick ni mchambuzi mzuri na huenda akawa na kipaji, kipaji ninachosema mimi nikipaji cha kusoma mambo kwenye mitandao na kuweza kuyaelezea yakaleta maana na mvuto. Kumbe ili uwe mchambuzimzuri lazima uwe mfuatiliaji wa soka uwanjani na kwenye vyombo vya habari kama magazeti, mitandao, TV na Redio. Zaidi ya yote uwe na uwezo wa kuchambua/kuchanganua soka kulingana na wakati. Suala la kwamba wengine wanabase kwenye mitandao ningesema Dr. Lick ndoo msomaji mzuri wa kwenye mtandao kuliko wengine hao na ndo maana anauwezo wa kuja na update hizo unazozisikia. Otherwise tupo pamoja.