Kasi ya kusaka urais CCM ni hatari kwa maendeleo

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
MBIO za kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete tayari zimeanza na zinakwenda kwa kasi kubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbio hizo zimeanza miezi michache baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana. Sio vibaya kwa wanasiasa kujiandaa kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa katika uchaguzi wa mwaka 2015, lakini wasiwasi wangu ni kwamba mbio hizo ndani ya CCM zimewahi mno.

Kinachonipa shida ni kuwa mbio hizo zimeanza kabla hata chama hicho kilichoshinda uchaguzi wa mwaka jana serikali yake haijaanza kutekeleza ahadi mbalimbali kilichoahidi kwa wananchi. Rais Jakaya Kikwete bado ana zaidi ya miaka minne na miezi kadhaa kabla ya kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Kwa maana hiyo, kuanza kwa mbio za kumrithi Rais Kikwete kwa sasa ni kumkwamisha asiiongoze nchi
 
Umesema kweli. Lakini lile kundi ambalo lina nia ya kuchukua madaraka kwa ajili ya kufanya ufisadi na kulipiza kisasi ndilo linalojipanga na kuyumbisha serikali ili hata ikiwezekana uchaguzi ufanyike kabla hata ya 2015.
 
Back
Top Bottom