KASI YA KUKUA KWA CDM NA KUPOROMOKA KWA CCM: Tathimini Ya Matokeo Ya Uchaguzi Uliopita Wa Kata 29..!

Nafikiri kila Mtanzania anayejua na kuona ambacho kinafanyika kuanzia kwa kwa chaguzi za ndani za CCM hadi kwenye chaguzi ndogo zinazoendelea haitaji kuelezwa wapi kuna tatizo.

Hili liko wazi kabisa na hasa tatizo kubwa la msingi ni RUSHWA ambayo kwa CCM sasa hivi ni sehemu ya mkakati usio rasimi lakini unakubaliwa na wahusika wengi kama mkakati wa ushindi.

Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na chombo chochote iwe TAKUKURU, NEC, au Serikali yenyewe, hili ni tatizo kubwa sana.

Kumbuka kuwa hata watu ambao wamekamatwa wakiwa na shahada za wapiga kura kinyume na utaratibu tena ikiwa ni wakati wa harakati za uchaguzi NEC na Serikali wanasema sio kosa, hii maanake nini, ni kwamba wamehalalisha uchafu wa kununua kadi za wapiga kura na kuzitumia kidri itakavyowezekana kupata ushindi, wote ni mashhidi wa haya tunayaona kila siku.

Tukiacha hilo, CCM ikishirikiana na vyombo vya dola huwadhuru na kwapiga na hata kuwaumiza wafuasi au watu wanaounga mkono vyama vya upinzani hususani CDM kwa sasa.

J
e hii hali ya vitisho vya namna hii kwa wapiga kura unaona ni tatizo dogo hili, Tume ya uchaguzi (NEC), Serikali, Polisi hupata taarifa lakini mara zote hakuna hatua ambazo zimechukuliwa.

Mimi nafikiri turuhusu akili zetu kuyatambua haya na mengine kama matatizo sugu kabisa yanavuruga kwa sehemu kubwa mfumo mzima wa upigaji kura.

Kama tutabaki tu kujifanya hatuyajui haya kumbuka hii ni nchi yetu sote na siku moja wote tunaweza kuwa wahanga wa matokeo mabaya ya vitendo hivi ambavyo wote tunaonekana kuvifumbia macho aidha kwa makusudi au kwa kutokujua.

Katika uwanja wa haki na usimamizi huru na upigaji kura wa wananchi wenyewe bila kutishwa na kuhongwa na kunyanyaswa hata CCM na Serikali wanalijua fika kwamba sio kata tu za Udiwani bali hata majimbo na Urais havipo mikononi mwao.

CDM kama chama kikuu cha upinzani wamevuna kabisa tena zaidi ya matarajio usijifunge kimawazo kwa kuangalia tu idadi ya viti vitano panua fikra zaidi kwa kuangali jinsi gani CDM wamejitanua zaidi na kujiotambulisha zaidi kwa wananchi hadi maeneo ya vijijini na kupata kura nyingi pamoja na vikwazo vingi vigumu vilivyopo njiani.

Hii ni hatua kubwa na lazima kama kweli tunapenda mabadiliko kiukweli na ya maana tutambue mafanikio ambayo CDM imeonyesha na kuyapata katika harakati za Kisiasa hapa nchini amabayo ktk historia ya nchi hakuna Chama cha upinzani ambacho kimewahi kukua na kuonyesha njia zenye mafanikio makubwa kama haya ambayo tunayashuhudia CDM ikifanya na kuifannya CCM ihangaike namna ambavyo hawaamini kama wako salama mda wowote.

Kila la kheri CDM, mmefanya kazi kubwa inayostahili pongezi, ongeza kasi na mikakati zaidi tunaona mafanikia ya jitihada zilizopo za kumkomboa mtanzani na wezi na wakoloni waliojificha chini ya mwavuli wa CCM na Serikali yake dhalimu.

Ni ukweli kuwa kama mwanzo ulikuwa na tatu lakini mwishowe ukawa na tano ni dhahiri kuwa kuna nyongeza.

Nikiwa mpenda mabadiliko siridhiki na matokeo haya kwa sababu mbili kubwa,mosi nguvu iliyotumika ikihusisha viongozi wakuu wa CDM hailingani na matokeo haya.

Pili ni idadi ya watu wanaohudhuria mikutano na kuishabikia hailingani pia na matokeo. Ni lazima tutafakari zaidi,there is a problem somewhere that need to be dealt with immediately.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom