KASI YA KUKUA KWA CDM NA KUPOROMOKA KWA CCM: Tathimini Ya Matokeo Ya Uchaguzi Uliopita Wa Kata 29..!

Kyamkwikwi

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
441
146
Habari JF GT,

Baada ya kuzisoma comments na posts nyingi mbalimbali humu na kwenye baadhi ya newspapers nikalazimika kuanza kutafiti kidogo ili nipate picha halisi ya mgawanyo wa kura katika kata mbalimbali. Kusema kweli kwa mtu yeyote makini anayejua kupima ukuaji wa taasisi au chama cha siasa atakubaliana na mimi kuwa unahitaji kupumbazika au kufyatuka akili kidogo ili kuweza kubeza kwa namna yoyote ile ukuaji huu wa chama cha CDM katika sehemu mbalimbali za nchi. Hakika hii hali bila ushabiki ni tishio kubwa sana kwa ustawi wa CCM na serikali yake. Pamoja na ukweli kwamba CDM imeifunika na kuiporomosha CCM kwa kulinda kata zake na kuinyanganya CCM kata nyingine tatu, ebu twende mbele zaidi tuyatathimini matokeo ya kila kata kwa kina zaidi. Mimi nimeanza na naendelea kufatilia maeneo mengine ili niweze kupata uhalisia wa kila kata, kusema kweli CCM kaa chonja CDM inawamaliza ebu jichunguze vinginevyo kwa margin hii mtajikuta shimoni mda si mrefu. Kama bado na huu mnauita ushindi wa kimbumga basi mtakuwa mmelogwa na bila shaka hakuna tena jambo litakaloweza kuwaamsha usingizini. Ebu Nape wasaidie vipofu wenzio japo na wewe uko kwenye kundi hilo hilo kwa jinsi nilivyo kusikia ukibwabwaja, lakini waambie ukweli kuwa jamani ee tumekwisha, sidhani kama kweli bado mnaamini habari za chama cha msimu, KALAGABAO....!!!!!

No.
KATA
JUMLA YA KURA
(BILA YA ZILIZOHARIBIKA)
CDM%
CCM%
WAPI
1. Rwezera
2582
36.13
50.70
Geita
2. Kilema Kusini
2894
25.43
27.54
TLP ilishinda -Kilmjaro
3. Nanjara Reheha
3498
67.75
32.25
Lindi
4. Mnero Miembeni
1567
8.81
52.20
"
5. Myovizi, Mbozi
3224
46.46
53.53
Mbozi na Momba
6. Mpapa, Momba
1213
25.56
74.44
"
7. Mahenge
1154
38.47
61.52
Morogoro
8. Mtibwa
4468
69.29
30.70
"
9. Daraja2
3743
58.59
35.37
Arusha
 
Prf.Jay aliimba unakwenda hatua10 mbele unarud2 nyuma na bado unajicfu ...mwacheni Nape wao,hawajuhi hesabu za ch+/ha-
 
Nape ndio anaonyesha asivyo jua ku-analyze mambooooo, tena hapa washukuru mungu, dafrari la wapiga kura ni lile lile la 2010, hakuna wapya hapo, sasa labda 2015 wasifanye usajili wa wapiga kura
 
ukizingatia matunda ya shule za kata nayo yananukia alafu daftari la kura likaboreka ndo wataelewa M4C ina maana gani
 
Chadema imeshuka sana M4C imefeli sana, mmetapanya viongozi wa kitaifa na wabunge kila kata ya uchaguzi, mnapata kata 5, je msingepeleka? ingekuwa aje?
 
Fragmented upinzani is our worst enemy......

Ndugu hakuna kitu kinachoitwa "Fragmented Upinzani" Kila chama ni chama cha siasa, kina sera zake na KINAKINZANA na wenzie. So huwa hakuna "UNITED UPINZANI" kila mmoja anatakiwa awe yeye ni yeye.
 
Chadema imeshuka sana M4C imefeli sana, mmetapanya viongozi wa kitaifa na wabunge kila kata ya uchaguzi, mnapata kata 5, je msingepeleka? ingekuwa aje?.....

Kwa nini unapendelea WASINGEPELEKA? Je ninyi mliopeleka imekuaje?
 
Ndugu

Hii ingekuwa tamu zaidi kama kwanza ungeleta matokeo ya kata zote 29
Pili katika jedwali lako ungeongeza column nyingi za kuonesha matokea ya 2010, tulinganishe nani ame-gain kiasi gani cha kura? na nani ame lose kiasi gani cha kura regardless kama ameshinda au ameshindwa.

Najua hata huko CCM kuna watu wenye akili nzuri wangeweza kuuona huo ukweli. Tatizo moja la CCM ni KUTOKUAMBIANA ukweli.
 
Nafikiri wakati CCM wanatakiwa kujitathmini kwa kwa nini wanapoteza, CDM wanatakiwa watathmini mafanikio waliofikia hadi sasa ambayo ni ishara njema kwao. Pili CDM wafanye analysis ya kwa nini bado wako hapo walipo ni si mbele zaidi, pengine kuna kasoro za hapa na pale zinahitaji krekebishwa ili kupiga hatua vizuri. Lakini so far so good for CDM vinginevyo tutakuwa tunaongea kishabiki tu kwa kuruhusu vichwa vyetu kuwa vya kufuga nywele tu badala ya kufikiri - nimemnukuu Werema, japo masikini hakujua wakati anasema hivyo kwamba alikuwa akitangaza alivyo yeye pamoja na wenzake, ushahidi ni mwingi wa kuthibitisha kwamba Werema kichwa chake ni cha kufuga nywele tu.............!!
 
Je ni yapi matokeo ya mwanafunzi asiyefanya homework yake?

And WHY are WE tempted in trying to RESUSCITATE CCM?
 
Nafikiri ni vyema ukasoma na kuelewa vizuri mleta mada alichoandika....kwa kukusaidia amesema bado anaendele kufuatilia kwa kata zingine sasa sijui hapo unataka nini zaidi kama wewe una tofauti na alichoweka mpinge kwa data si kulalamika...!!

Kata 9 tu, are they representative samples to all wards in the country?
 
Back
Top Bottom