Kashifa ya mabilioni kufichwa uswisi;watanzani 27 wahusishwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,323
Watanzania 27 wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara ndio wamebainika kumiliki mabilioni ya fedha nchini Uswisi huku mmoja wao akimiliki Dola za kimarekani 56 milioni sawa na sh 89.6 bilioni za kitanzania.Kiasi cha fedha kinachomilikiwa na watanzania hao ni Dola za kimarekani 186 milioni ambapo ni sawa na zaidi ya sh 300 bilioni za kitanzania.

Taarifa zinasema kigogo mmoja anamiliki sh 90 bilioni na wengine wanne ni kama ifuatavyo.Mmoja dola 30 milioni(sh 48 bilioni),mwingine Dola 20 milioni( sh 32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni ambazo ni sawa na sh 16 bilioni.

Katika orodha hiyo wamo pia wafanyabiashara wanaomiliki kati ya Dola miloni 2 mpaka Dola milioni 7,kadhalika wamo waliowahi kuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza ambapo akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kila mmoja.

Taarifa zaidi zinasema fedha hizo ziliwekwa kwenye account za vigogo hao kwa mara ya mwisho mwaka 2005.

Source:Mwananchi online la tarhe 18/08/2012.
 
Watanzania 27 wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara ndio wamebainika kumiliki mabilioni ya fedha nchini Uswisi huku mmoja wao akimiliki Dola za kimarekani 56 milioni sawa na sh 89.6 bilioni za kitanzania.Kiasi cha fedha kinachomilikiwa na watanzania hao ni Dola za kimarekani 186 milioni ambapo ni sawa na zaidi ya sh 300 bilioni za kitanzania.

Taarifa zinasema kigogo mmoja anamiliki sh 90 bilioni na wengine wanne ni kama ifuatavyo.Mmoja dola 30 milioni(sh 48 bilioni),mwingine Dola 20 milioni( sh 32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni ambazo ni sawa na sh 16 bilioni.

Katika orodha hiyo wamo pia wafanyabiashara wanaomiliki kati ya Doli miloni 2 mpaka Dola milioni 7,kadhalika wamo waliowahi kuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza ambapo akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kila mmoja.

Taarifa zaidi zinasema fedha hizo ziliwekwa kwenye account za vigogo hao kwa mara ya mwisho mwaka 2005.
Here comes Ben again
 
Kwani wakitajwa hadharani ni dhambi? ili tuwajue wahujumu uchumu.. au wanaogopa watafungiwa kama mwanahalisi.
 
hivi wanajamii wenzangu pesa hizo kama zingekuwa kwenye mabenki yetu ya hapa tanzania si tungeweza hata kukopeshwa sisi tukajikwamua na umaskini huu,sasa kule walikoziweka zinafanya kazi gani? Wawe na huruma na sisi watanzania wenzao maskini..........
 
Mwaka 2005 ndo izo ela zmewekwa? inamaana enzi za mkapa? duh apa changa la macho ndo lnaanzia
 
Back
Top Bottom